Tuesday 6 May 2014

KUZIBA KWA MIRIJA YA UZAZI


Tatizo la kuziba kwa mirija ya mayai ya uzazi au mirija ya kupitishia mayai ya mwanamke ni mojawapo ya sababu kubwa za ugumba kwa mwanamke ambapo mwanamke anakosa uwezo wa kuzaa.

Mirija inapoziba yai linashindwa kukutana na mbegu ya mwanaume na kutungisha mimba.

Kitaalamu mirija ya mayai 
au ‘fallopian tubes’ pia huitwa ‘Oviducts’ au uterine tubes’ au Salpinges’.
Matatizo ya ugumba kwa mwanamke yana vyanzo vingi lakini kuziba kwa mirija ni tatizo kubwa ambalo huathiri wanawake wengi wenye tatizo hili. Katika makala yaliyopita tuliona uchunguzi wa kuthibitisha tatizo hili.

Aina ya uzibaji wa mirija
Kwa mujibu wa utafiti ambao umeshawahi kufanyika, asimilia 20 ya matatizo ya ugumba kwa wanawake husababishwa na tatizo la mirija ya uzazi.

Mirija inaweza kuziba upande wa mwisho jirani na vifuko vya mayai ‘Distal tubal occlusion’ na hii huhusiana zaidi na hali ya kuvimba mirija  ambayo tutakuja kuiona hapo baadaye na chanzo cha tatizo la mirija kuvimba husababishwa na maambukizi ya ‘Chlamydia Trachomatis.’

Mwanamke mwenye tatizo la kuvimba 
mirija au mirija kujaa huwa na maumivu upande wa kulia au kushoto au pande zote mbili chini ya tumbo na hupata maumivu baada ya tendo la ndoa na huwa hashiki mimba.
Tunaposema ugumba maana yake unatafuta ujauzito ndani ya mwaka mmoja bila ya mafanikio.

Aina ya pili ya uzibaji wa mirija ya uzazi 
ni kushikamana hiyo mirija hali iitwayo kitaalamu ‘Pelvic adhesions.’ 
Tatizo hili linasababishwa na jamii hiyohiyo ya vimelea ambavyo tumeshaviona hapo awali. Tatizo hili huwa siyo kali na mara chache mgonjwa hulalamika 

maumivu, kushikamana huku ni hali ya makovu ndani na nje ya mfumo wa uzazi, upande wa vidole kushika mayai hujikunja na wakati mwingine mrija wenyewe hukamatana na viungo vingine jirani hivyo kuzuia yai kupenya na kusafiri kwenye mrija. 

Wakati mwingine 
katika tatizo hili pia mrija unaweza kuwa wazi na kuruhusu yai kupenya.
Mirija inaweza kuziba sehemu ya kati ‘midsegment tubal osbsraction’ na hii inaweza kusababishwa na operesheni ya kufunga kizazi.

Mirija inaweza kuziba upande wa juu 
karibu na mfumo wa uzazi na chanzo kikuu ni maambukizi ndani ya kizazi hasa baada ya kutoa au kuharibika mimba.
Mirija inaweza kuziba kwa bahati mbaya baada ya upasuaji wa uzazi au kuondoa uvimbe.

Chanzo cha tatizo
Chanzo cha mirija kuziba ni maambukizi ndani ya kizazi au maambukizi ya viungo vya uzazi ‘Pelvic Inflammatory diseases’ au kwa kifupi ‘PID”. Ugonjwa 

huu wa PID 
siyo mzuri kwani utafiti unaonyesha kwamba asilimia 12 ya wanawake wanaopata ugumba kwa kuziba mirija wameugua PID na kutibiwa na kupona mara moja, waliougua PID zaidi ya mara tatu wana zaidi ya asilimia 53 ya kupata tatizo hili la kuziba mirija ya uzazi.

Dalili za ugonjwa huu wa PID 
ni maumivu ya tumbo chini ya kitovu mara kwa mara, kutokwa na uchafu ukeni aidha ukiwa na harufu au muwasho, maumivu wakati wa tendo la ndoa na siku za hedhi kuvurugika.
Maambukizi ndani ya tabaka la ndani la kizazi pia huchangia na dalili zake zinafanana na zile za PID.

Maambukizi 
pia unaweza kuyapata baada ya kujifungua au endapo utakuwa na ugonjwa wa kidole tumbo. Mirija pia inaweza kukatwa siyo tu kwa kufunga uzazi lakini hata endapo mimba itatunga na kukua kwenye mrija.

Nini cha kufanya? 
Tatizo hili la kuziba mirija ya mayai huchunguzwa kwa kina ili kujua aina ya uzibaji na hatua za kuchukua. Vipimo kama tulivyoviona katika toleo lililopita, mfano kipimo cha HSG ambapo dawa huingizwa katika kizazi na kupiga picha. Kipimo hiki hakizibui mrija bali kinaonyesha jinsi mrija ulivyo.

Kipimo cha Ultrasound au ‘Sonography’
huonyesha mrija kwa nje kama una kasoro zozote, aidha umevimba au la, Laparoscopy na vingine ambavyo daktari ataona vinafaa vifanyike.

Baada ya hapo 
tiba sahihi itafanyika kama ni kuzibua au upasuaji.
Endapo mirija itazibua na ikaziba tena, basi uwezekano wa kuizibua huwa mdogo na mshauri huwa ni upandikizaji au IVF.
Ni vema uwahi katika hospitali ya mkoa uwaone madaktari wa matatizo ya uzazi kwa uchunguzi wa kina na tiba. 


0 comments:

Post a Comment