Tuesday, 6 May 2014

FAHAMU KUHUSU KIZAZI


KITAALAMU kizazi kina majina yake ya asili kama vile ‘Hystera’ na ‘womb’. Jina uterus limetokana na neno la lugha ya Kilatini.
Kizazi ni sehemu muhimu ambayo vichocheo au ‘Hormone’ za mwanamke huelekezwa huko na kuanza kuonyesha mabadiliko dhahiri.

Kizazi kipo katikati ya nyonga kwa chini ya kibofu cha mkojo na nyuma ya mfuko wa haja kubwa.
Umbo la kizazi ni kama pia, kizazi cha mwanamke aliyefikia umri wa kuzaa kina urefu wa sentimeta 7.6, upana wa sentimeta 4.5 na kuta zake zina unene wa sentimeta 3.0 na kinalalia kwa mbele.

Mwanamke ambaye siyo mjamzito 
kizazi chake kina uzito wa gramu 60. Kizazi kimegawanyika katika sehemu kuu nne, kwanza kuna mgongo,
mfuko wa kizazi, shingo ya kizazi na mlango wa ndani wa kizazi.
Kizazi pia kimegawanyika katika tabaka tatu, kwanza ni tabaka ya ndani liitwalo ‘Endometrium,’  kazi ya tabaka hii ni ambapo mimba inajikita na damu ya hedhi inatokea hapo, endapo kizazi kitakuwa kinasafishwa mara kwa mara husababisha kutokea makovu na kushikamana kwa kizazi. Vilevile anaweza kupata tatizo kubwa litakalosababisha kupoteza siku zake na kukosa uzazi hali iitwayo ‘Asherman’s syndrome.’
Mzunguko wa hedhi wa mwanamke 
unaendeshwa na kizazi na urefu wa kati ya siku 21 hadi 35.
Kila mwanamke ana urefu wa mzunguko wake.
 Kizazi kinapokaa katikati ya nyonga hushikiliwa na viungo mbalimbali pande zote. Kwa kawaida kizazi kitaalamu kimelala katika mlalo uitwao ‘Anteversion and Anteflexion’.
Tunaposema 
‘Anteversion’ ni pale kizazi kinalalia kwa mbele, kinaegemea kwa mbele na kinaegemea kibofu cha mkojo.
 ‘Anteflexion’ ni pale kizazi kinalalia kona za mirija ya uzazi na mfuko wa haja kubwa. Wanawake wengi kizazi hukaa sawa ila wapo ambao hukaa vibaya na kuwasababishia baadhi ya matatizo ambayo tutakuja kuyaona katika makala zijazo.

MATATIZO MBALIMBALI YA KIZAZI
Kizazi kinaweza kukaa vibaya na kugeuka kwa nyuma na kumfanya mwanamke apate maumivu ya kiuno, mgongo na tumbo upande wa chini.
Maumivu haya husambaa hadi miguuni, hali hii ina vyanzo vyake ambavyo tutakuja kuona.
Kizazi 
pia kinaweza kulalia kwa mbele kupita kiasi na kumsababishia mwanamke maumivu ya chini ya tumbo, kupata haja ndogo mara kwa mara na maumivu wakati wa kukojoa.
Vilevile kupata maumivu wakati wa hedhi na maambukizi ya mkojo au Yutiai isiyoisha, maumivu wakati wa tendo la ndoa na mkojo kutoka kidogokidogo na maumivu.
Matatizo mengine 
yanayotokea katika kizazi ni kama vile kushuka kwa kizazi, saratani ya shingo ya kizazi, saratani ya kizazi, uvimbe ndani ya kizazi, kuta za uzazi kuongezeka ukubwa, maambukizi ndani ya kizazi na makovu ndani ya kizazi.
Maambukizi ya ndani ya kizazi pia yanaweza kusambaa hadi katika mirija ya uzazi na kuleta athari kama tulivyoona katika makala zilizopita.

UCHUNGUZI WA TATIZO
Matatizo ya kizazi yapo mengi sana kama mtakavyoanza kuona katika mfululizo huu. Matatizo mengine yanaweza kuwa ni kasoro za kuzaliwa nazo lakini nyingine hutokea kadiri maisha yanavyoendelea.
Uchunguzi wa matatizo haya hufanyika katika hospitali za wilaya na mikoa na katika kliniki za magonjwa ya kinamama. Vipimo vya mkojo, damu na Ultrasaund na kuangalia mlango wa shingo ya uzazi hufanyika.

Related Posts:

  • FAHAMU JINSI YA KUSHINDWA KUSHIKA MIMBA (INFERTILITY) KUNA njia au aina mbili za wanawake kushindwa kushika mimba au kwa maneno rahisi, ugumba kitaalamu Infertility,  ambao unatambuliwa kitabibu. Aina moja huitwa kitaalamu kama Secondary Infertility na aina nyin… Read More
  • MAGONJWA NYEMELEZI KWA WANAWAKE - 2-3 MPENDWA msomaji, leo nitaendelea kuelezea kuhusu magonjwa nyemelezi kwa wanawake tukimalizia na mkanda wa jeshi. Tuwe pamoja... Mkanda wa jeshi mbali ya kuathiri sehemu za mishipa ya fahamu (neva), pia huweza kudhur… Read More
  • MAGONJWA NYEMELEZI KWA WANAWAKE-4-5 Mpenzi msomaji, naendelea kuelezea kuhusu magonjwa nyemelezi kwa wanawake, tuwe pamoja...Vimelea vya Pneumocystis jiroveci huathiri mfumo wa hewa.Fangasi huyu pia huweza kuathiri viungo vingine kama ini, wengu (spleen) na … Read More
  • KUTOKWA NA MAJIMAJI SEHEMU ZA SIRI Tatizo hili huwatokea wanawake na wanaume. Mwanaume hutokwa na majimaji katika njia ya mkojo, mwanamke hutokwa na majimaji haya katika njia ya mkojo au ukeni.Majimaji haya yanaweza kuwa mepesi au mazito, pia yanaweza kuw… Read More
  • KUZIBA KWA MIRIJA YA UZAZI Kuziba kwa mirija ya uzazi ya mwanamke ni tatizo kubwa na ndiyo linaloongoza kusababisha ugumba kwa mwanamke ingawa hata matatizo ya vichecheo au homoni pia huchangia.Wanawake wengi wanaohangaika kutafuta watoto hugundulik… Read More

0 comments:

Post a Comment