Tatizo hili huwasumbua wanawake wengi walio katika umri wa kuzaa na baadhi ya wanawake ambao tayari wameshafikia ukomo wa kuzaa.
Kwa mwanamke aliyekwishafunga kupata hedhi kuendelea kupata damu ya
hedhi au kutokwa na damu ukeni bila ya mpangilio siyo hali ya kawaida.
Mwanamke anaanza kuvunja ungo kuanzia umri wa miaka 12 na hufikia ukomo kuanzia umri wa miaka 45. Kupatwa na damu ukeni chini ya umri wa miaka 40 kuna vyanzo vingi kama tutakavyoona.
Mwanamke anaanza kuvunja ungo kuanzia umri wa miaka 12 na hufikia ukomo kuanzia umri wa miaka 45. Kupatwa na damu ukeni chini ya umri wa miaka 40 kuna vyanzo vingi kama tutakavyoona.
Chanzo cha tatizo
Damu kutoka bila ya mpangilio kwa mwanamke ambaye hajakoma hedhi husababishwa na mabadiliko katika mfumo wa homoni endapo hazipo sawa ‘Hormonal Imalance.’ Uwepo wa uvimbe katika kizazi na matumizi ya dawa za homoni mfano sindano au vipandikizi. Kuweka kitanzi katika kizazi pia huwafanya wanawake wengine wapate hali hii ya kutokwa na damu bila mpangilio.
Mabadiliko ya mfumo wa homoni huweza pia kusababishwa na mshtuko wa mwili au hali ya mabadiliko ya mazingira.
Kuharibika kwa mimba pia ni mojawapo ya sababu kubwa. Mwanamke mwenye
umri wa zaidi ya miaka 45 kupata damu ukeni bila ya mpangilio ni vema
kuchunguza kwa undani kwani wana uwezekano mkubwa wa kuwa na saratani ya
kizazi au shingo ya uzazi.
Dalili za tatizo
Mwanamke hulalamika kuona siku za hedhi zaidi kuliko kawaida yake, au
kuona katikati ya mzunguko yaani aliona, ikaacha sasa inaanza tena.
Damu inaweza kuwa nyingi na mwanamke akabadilisha pedi mara nyingi
kuliko kawaida yake au akapata kidogokidogo lakini kwa muda mrefu.
Damu inaweza kuwa nyepesi au nyeusi au nzito na mabonge. Hutoa harufu isiyo ya kawaida endapo ata-bleed kwa muda mrefu.
Ikiwa na mabonge huambatana na maumivu.
Mgonjwa huchukua muda
mrefu hata zaidi ya majuma mawili akiwa anatokwa na damu, endapo
hatapata tiba haraka huanza kuumwa tumbo chini ya kitovu ikiwa ni dalili
za kupatwa na maambukizi ya kizazi kwa kuwa bakteria hupenda sana
mazingira ya damu.
Hali inapoendelea mwanamke hupoteza uwezo wa kushika mimba na
huathiri uzazi kwani hushindwa kufanya tendo la ndoa, homoni
zinavurugika na maambukizi ya kizazi huathiri mirija ya mayai.
Uvimbe wa Fibroid ukiwa ndani ya kizazi husababisha damu zitoke bila ya
mpangilio na kuzuia mimba kukua na hata ikiingia inaweza isiendelee.
Uchunguzi
Tatizo hili ni sugu na huleta athari
kubwa katika mfumo wa uzazi wa mwanamke hivyo ni vema uchunguzi wa kina
ukafanyika katika hospitali kubwa. Vipimo vya damu kuangalia mfumo wa
homoni, kipimo cha Ultrasound kuangalia kizazi na vifuko vya mayai pia
hufanyika.
Ushauri
Usidharau tatizo hili la kutokwa na damu bila mpangilio ukeni ukiwa bado binti au mtu mzima kwani madhara yake ni makubwa. Muone haraka daktari kwa uchunguzi na tiba.
Usidharau tatizo hili la kutokwa na damu bila mpangilio ukeni ukiwa bado binti au mtu mzima kwani madhara yake ni makubwa. Muone haraka daktari kwa uchunguzi na tiba.
0 comments:
Post a Comment