Monday, 5 May 2014

MATATIZO YANAYOAMBATANA NA UKOMO WA HEDHI



UKOMO wa hedhi, ni kipindi ambacho mwanamke anaacha kuziona siku zake kama ilivyokuwa tangu anavunja ungo. Kitaalamu, hiki ni kipindi ambacho mwili wa mwanamke unaacha kuzalisha homoni za Estrogen na Testosteron ambazo ndizo zifanyazo kazi ya kupevusha mayai kila mwezi.

Mwili unapoacha kuzalisha homoni hizi ambapo kwa wastani huwa ni katika umri wa kuanzia miaka 40- 45 (wengine wanaweza kuwahi au kuchelewa), kuna mabadiliko mengi yanayotokea kwenye mwili wa binadamu ambayo humsababishia mhusika matatizo mbalimbali ya kiafya.
Yafuatayo ni baadhi ya matatizo yanayowakumba sana wanawake waliofikia au wanaokaribia kufikia ukomo wa hedhi.

Kupoteza msisimko wa mapenzi

Hili ni tatizo linalowasumbua wanawake wengi hasa wale ambao wapo katika ndoa. Kutokana na mwili kuacha kuzalisha homoni za Estrogen na Testosteron, atika kipindi hiki, mwanamke hukosa kabisa msisimko wa kimapenzi hata kama mumewe atajitahidi kumuandaa kwa kiasi gani.
Wengine hufikia hatua ya kuwachukia waume zao, jambo ambalo kama hakuna mwenye uelewa wa kinachotokea, huweza kusababisha matatizo makubwa kwenye ndoa.

 Mabadiliko ya kihisia

Wanawake wengi husumbuliwa na tatizo la mabadiliko ya kihisia katika kipindi hiki. Wengi hupandwa na hasira  kwa urahisi, hushambuliw ana msongo wa mawazo, mwili huishiwa nguvu na wengine hukumbwa na tatizo la kutojiamini.
Katika hatua hii, inabidi kuwasaidia wahusika kwa kuwafundisha mbinu za kupambana na msongo na kudhibiti hasira pamoja na mbinu za kujiamini upya sambamba na mazoezi ya viungo.

 Kukosa usingizi

Tatizo lingine ni kukosa usingizi ambapo mwanamke hujikuta akishindwa kulala mpaka usiku wa manane au wakati mwingine mpaka alfajiri.

0 comments:

Post a Comment