Saturday 3 May 2014

JUA KUHUSU SUMU KWENYE CHAKULA/ FOOD POISONING.




Ni jambo la kawaida sana kwa baadhi ya Watu kuumwa tumbo na kuhara  baada ya kula chakula Fulani,kuna watu hawali mboga, matunda, nyama au samaki wa aina Fulani kwasababu wakila Tumbo linauma,na wengine hata kutapika.
Wataalam wa afya wanasema hii husababishwa na hali ya mwili wa mtu kutokukubaliana na kitu Fulani kilicho katika chakula kile. inaweza kua ni kemikali ya asili iliyo katika chakula au ,aina fulani  ya vijidudu (vyenyemanufaa) Na wakati mwingine husababishwa na vijidududu viharibifu vilivyomo katika chakula.
Nitoe mfano :
Kaka yangu Deogratius hatumii kabisa mafuta ya pamba akila chakula kilichopikwa na mafuta ya pamba, naumwa sana tumbo na kuhara adi pale kile chakula kitakapoisha kabisa tumboni,
mara nyingi inamchukua siku mbili adi Tatu Tumbo langu kurudi katika hali ya kawaida.

Wengi mtakubaliana na mimi nikisema mara nyingi sana watu huumwa tumbo baada ya kula vyakula kwenye sherehe au hotelini. Na wengi hukwepa kula kachumbari,salads na matunda wanapokula nje ya nyumbani. Sababu inayofanya wakwepe kula salads na kachumbari ni kwa sababu hawaamini usafi wa mboga,matunda pamoja na mikono ya Yule aliyeandaa,na kwa sababu vyakula hivyo huliwa vibichi watu hawaamini usalama wake.

Hali ya kuumwa tumbo inayosababishwa na chakula huitwa kwa kitaalamu Food poisoning yaani Sumu ndani ya chakula



Maana ya food poisoning/ Sumu ndani ya chakula
Food poisoning ni ugonjwa unaosababishwa na ulaji na unywaji wa chakula chenye  viumbe waharibifu kama vile bacteria,virusi,au vimelea vya maradhi na wakati mwingine husababishwa na kemikali zinazopatikana ndani ya chakula fulaniau  katika samaki na mimea yenye sumu ya asili.
 
Mara Nyingi viumbe viharibifu hupatikana kwenye vyakula vibichi kama  nyama ,kuku,samaki na mayai na kwenye mboga za majani na matunda yasiooshwa  vizuri. lakini vinaweza kusambaa kwenye aina yoyote ya chakula. pia vinaweza kukua kutoka kwenye chakula chenyewe hasa pale chakula kinapotunzwa vibaya.
Lakini pia food poisoning huweza tokea pale mtu anashika chakula bila kuosha mikono,kwani kunauwezekano wa kubeba vijidudu waaribifu kutoka kwenye vyanzo vingine.
Baadhi ya Vijidudu vinavyosababisha food poisoning ni  Salmonella  na E coli.
Mara nyingi food poisoning si ugonjwa unaokuja  kwa nguvu, Kawaida  huisha wenyewe baada ya siku chache, baada ya mwili kuondokana na vijidududu vilivyosababisha ugonjwa au kuumwa huko. Lakini kuna aina ya food poisoning ambazo ni mbaya sana na zinaweza ata kuchukua maisha ya mtu,hivyo ni vyema kuwahi hospitali kwa ajili ya tiba.
Dalili za food poisoning
Dalili kuu ya food poisoning ni
ü kuhara.
ü lakini pia unaweza  kutapika,
ü kua na maumivu ya tumbo(kitaalamu hujulikana kama stomach flu).
ü Aidha dalili hizo mara nyingi huambatana na maumivu ya misuli, homa, kutetemeka mwili na kuhisi kuchoka.
Dalili hizi hutofautiana kati ya mtu na mtu kutokana na aina ya vijidududu wanaosababisha ugonjwa pamoja ya uwezo wa kinga zake za mwili kukabiliana na ugonjwa.
Hatua ya kuhara na kutapika, husaidia mwili kuondoa sumu au vijidudu vya maradhi katika mfumo wa mmeng’enyo wa chakula (digestive tract) na hivyo kuzizuia sumu au vijidudu vya maradhi kuingia katika mfumo wa damu.
Kuhara na kutapika kwingi husababisha mwili kuishiwa maji hivyo ni vyema kunywa maji mengi.Kukauka mdomo na koo, kuumwa kichwa na mkojo mchafu ni dalili za kuishiwa maji mwilini.
Watoto wadogo na wazee huishiwa maji mwilini kwa haraka sana, ni vyema kuwatizama kwa karibu wanapopata food poisoning.
Mama mjamzito anapohisi  kua amepata food poisoning ni vyema kwenda hosipitali haraka.Katika picha.
Bibi anaongezewa maji baada ya kuhara na kutapika kwa muda mrefu kulikosababishwa na uyoga wenye sumu.
Baadhi ya namna ambazo  vijidudu huingia kwenye chakula
  • Ni kawaida kabisa kukuta vijidudu vya maradhi katika utumbo wa wanyama ambao binadamu hutumia nyama yao, kama ng’ombe,kuku,samaki,mbuzi na nguruwe kutoka na ualisia wa vyakula wanavyokula.
Hivyo ni vyema kujua kwamba nyama ya utumbo huwa na vijidudu vingi vinavyoweza kuleta food poisoning.Wakati mwingine vijidudu hivyo husambaa kwenye sehemu nyingine au vipande vingine vya nyama wakati wa uandaaji wa nyama machinjioni.
  • Kama mboga na matunda zinamwagiliwa na maji machafu hasa yale yenye uchafu wa chooni au wa zizi basi vijidu hutoka kwenye maji hayo machafu na  huingia katika mboga na matunda, Pia endapo mboga na matunda vitaoshwa na maji machafu Vijidudu vitabaki kwenye mboga na matunda hayo.

  • Pale mtu anaposhika chakula kwa mikono michafu yenye vijidudu,vijidudu hubaki kwenye chakula.

Inzi anapotua kwenye kwenye chakula au uchafu wenye vijidudu huvibeba.na pale atakapotua kwenye chakula kisafi huacha vijidudu hivyo.

  • Wakati mwingine vijidudu hutoka hewani na kuingi kwenye chakula.kuna navaijidudu vingi sana hewani na baadhi huweza sababisha food poisoning pale wanapoingia kwenye chakula
Wakati mwingine ni ngumu kugundua umepata food poisoning, kwani mara nyingi ugonjwa huu hauji kwanguvu. Mara nyingi tumbo huuma na kisha kuhara,mara nyingi utasikia watu wakisema chakula kimewachafua tumbo.
Endapo unahisi au umepata dalili hizi ni vyema kuwauliza wale mliokula nao chakula hicho kama nao wanapata dalili hizo,hii itasaidia kujua kama umepata food poisoning ili uweze kuchukua hatua mapema.
Dalili za food poisoning huanza kujitokeza kati ya saa moja hadi matatu baada ya kula chakula kisichofaa, Na wakati mwingine mtu hawezi kujisikia vibaya  hadi siku chache  baadaye
Namna ya kuepuka food poisoning
Unaweza chukua hatua zifuatazo ili kuepukana au kupunguza uwezekano wakupata na food poisoning.
  • Osha mikono baada ya kutumia chooo,na kabla ya kushika chakula chochote.
  • Osha mboga na matunda vizuri
  • Epuka mboga za majani zilizolimwa karibu na sehem za taka au zinazomwagiwa maji machafu
  • Pika nyama vizuri na uakikishe imeiva vizuri
  • Unapoandaa utumbo ,hakikisha umeuosha vizuri,na upike kwa muda mrefu ili kuuwa vijidudu wote
  • Epuka kula chakula kilichokaa  wazi kwa muda mrefu (wale wenzangu tunaopenda kula safari vyakula vya madirishani vile)
  • Pasha moto vizuri kabla ya kula kipioro
  • Jokofu lako liwe na ubaridi wa nyuzi joto 40 na freezer iwe na 0
  • Epuka kutunza kiporo frijini zaidi ya siku nne,endapo unataka kikae zaidi ya apo basi kiweke kwenye freezer.
 
Mboga zilizopandwa katika mazingira safi

Watoto ni kundi ambalo liko katika hatari kubwa sana ya kupata food poisoning,ni jukumu la kila mzazi na kila mtu mwenye uelewa juu ya food poisoning kuchukua hatua ili kusaidia kuwaepusha watoto na tatizo hili kwa kuwafundisha na kuwapa ufahamu juu ya tatizo hili na pia kuwatizama kwa karibu.
Zingatia usafi. 

0 comments:

Post a Comment