Mara nyingi
sana nimesikia kinamama wakijadiliana juu ya hili na kubadilishana uzoefu. Ingawa
nimesikia wengi wakiliongelea kinachoshangaza ni kwamba sijawahi kusikia
jibu
moja ambalo naweza sema ndilo jibu sahihi au laa basi kuambiwa kwamba hili
ndilo jibu sahihi na kupewa sababu
za kuridhisha .
Kwakua
lengo langu ni kuhakikisha afya ya umma na familia kwa ujumla iko vizuri, nimeamua
kufanya Utafiti binafsi
kwa kusoma vitabu ,majarida na kuongea na baadhi
ya madaktari wa watoto ninaowafahamu.
Si
kuishia hapo tu, nimeongea na akina mama waliolea watoto miaka ya zamani na
wanaolea watoto hivi sasa. Na haya ndio majibu niliyopata.
Majibu
kutoka taasisi za afya.
Taarifa
za wataalam wa afya kutoka kwenye taasisi zinazoaminika duniani kama
World health organization na Association of American Pedietrisions, zinasema
Mtoto mdogo kati ya siku moja hadi miezi sita (1-6)
Hatakiwi
kupewa maji wala chakula kingine chochote zaidi ya maziwa ya mama au maziwa
maalum ya watoto(baby formula) au maziwa ya Ngombe.
W.H.O
shirika la afya Wameelezea kwamba kiasi cha maji mtoto anachopata kwenye maziwa
kinatosha kabisa.
Kumpa
mtoto maji si salama kwani yataharibu uwezo wa mwili wa mtoto kunyonya
virutubisho kutoka kwenye
maziwa.
Maji pia
yatafanya mtoto ashibe na ashindwe kunywa maziwa kwa kiasi kinachohitajika, Mbaya
zaidi ni kwamba maji mengi kwa mtoto wakati mwingine huweza kuleta hali iitwayo
water intoxication,
Hali hii
huweza kumfanya mtoto azimie na wakati mwingine kuingia katika coma. Hali
hii huja pale ambapo wingi wa maji mwilini utapunguza kiasi cha sodium mwilini(low
sodium concentration).
Taarifa
inasema kwamba, ingawa unaweza kumpa mtoto maji baada ya miezi 6, wanashauri
mtoto apewe maji kidogo na kwa kipimo maalum hadi pale atakapo timiza mwaka
mmoja ambapo anaweza kunywa maji kwa kiasi
atakacho.
Majibu
kutoka kwa madaktari wetu.
Madaktari
wanne tofauti niliyobahatika kuongea nao, majibu yao yalifanana kwa kiasi
kikubwa.
Kwanza
waliunga mkono taarifa za World health organization (taarifa hapo juu) . Lakini
pili walikua na yao
Walisema
kwamba maziwa ya mama na formula zinamtosha mtoto endapo tu mtoto huyo anapewa
maziwa yanayomtosha kushiba na yenye virutubisho vyote.
Walieleza
kwamba kina mama wengi hawanyonyeshi mtoto hadi akashiba. Si kwasababu hawana
maziwa au hawataki bali ni kwasababu hawajui mtoto anaitaji maziwa kiasi gani
ili ashibe na anyonyeshe kwa muda gani ili mtoto apate kiasi hicho cha maziwa.
Na kwa sababu wakati mwingine maziwa ya
mama yenyewe hayana virutubisho vyakutosha kwani mama mwenyewe hali, au mwili
wake hauna virutubisho vyakutosha na wakati mwingine anapungukiwa baadhi ya
virutubisho .
Walisema
kua hali hii hufanya maziwa ya mama yasitoshe kabisa kwa mtoto na kulazimu
mtoto aanze kupewa uji mwepesi mapema kabla ya miezi sita ili kufidia lishe
yake.
Na Pale tu unapoanza kumpa mtoto chakula zaidi ya maziwa basi ni
vyema ukaanza kumpa maji kwani uji na vyakula kama hivyo huesabika kama vyakula
vigumu kwa mtoto.
Moja
alisema kwamba endapo mtu analazimika kumpa mtoto uji mapema basi ni
vyema mtoto afikishe angalao
miezi minne.
Mwingine
alisema kwamba, moja ya sababu zinazochangia kabisa kuwakataza kina mama kuwapa
watoto maji ni pamoja na uwezekano mkubwa wa mtoto kupata magonjwa
kutoka
kwenye maji ya kunywa.
Mara
nyingi maji hayawi safi na salama. Alinieleza kwamba, magonjwa ya tumbo
yanayoleta kuhara kwa mtoto ni moja kati ya magonjwa yanayosababisha vifo vya
watoto kwa h
haraka.
Majibu ya
Mama aliyelea watoto miaka ya 60 – 80
Mama huyu
aliyeanza kulea mtoto wake wakwanza mwaka 1967 alikua na haya yakusema.
Alisema
enzi zile walikua wanafundishwa namna ya kulisha mtoto kila wanapoenda kliniki.
Alisema
Walikua wakipewa karatasi yenye picha za vyakula na majina ya vyakula
hivyo na kuambiwa zaidi ya kunyonyesha ni lazima wawape watoto wao vyakula
hivyo.
Wakati mwingine walienda kwenye vikundi vya akinamama na kufundishwa
namna ya kuandaa vyakula hivyo kwaajili ya mtoto.
Alinieleza
kua vyakula hivyo viliwekwa kwa makundi,na kulikua na kundi lenye maji ya
kunywa na maji ya matunda.
Hivyo wao waliwapa watoto maji na maji ya matunda
kama kadi ilivyoelekeza, aliniambia kua walikua wakipewa karatasi hizo
miezi miwili baada ya kujifungua. (akimaanisha mtoto akiwa na miezi
miwili).
Kwa maana
hiyo, walianza kuwapa watoto uji, maji na maji ya matunda wakiwa na miezi
miwili.
Majibu ya
Mama anaelea watoto hivi leo.
Niliongea
na mama wawili tofauti, mmoja ana watoto wanne
na mwingine ana wawili.
Mwenye
watoto wanne, alisema watoto wake wote
walianza kunywa maji na uji mwepesi wakiwa na miezi miwili. Alisema kwamba
ingawa watoto wake walikunywa
maziwa bila shida aliona wazi kabisa kwamba
hawashibi na ndipo alipoamua kuongeza uji mwepesi kwenye lishe yao.
Alinieleza
kwamba huandaa uji huo na kisha kuuchuja na
kuhakikisha ni mwepesi kama maziwa
na kisha kumpa mtoto kwenye chuchu kama anavyompa maziwa.
Uji huo
huandaliwa kwa maziwa,maji na unga.
Mwenye
watoto wawili, alikua na haya
yakusema.
Alisema
kwamba watoto wake walikunywa maziwa tu hadi walipofikisha miezi 6. Pale
alipoona maziwa ya mama hayatoshi aliongeza maziwa ya ng’ombe ili kuhakikisha
mtoto anashiba.
Alinieleza
kwamba, ili kuhakikisha mtoto anakunywa maziwa kwa kipimo sahihi, alikamua
maziwa yake kwa kutumia pampu maalum na kuyaweka kwenye chupa ili apime
kipimo
sahihi. Na kwakua mtoto wake hushiba vizuri na wataalam husema mtoto asipewe
maji basi hakua na sababu yoyote ya kumpa mtoto maji kabla ya wakati
uliothibitishwa.
Mtizamo
wangu
Baada ya
kukusanya yote haya na kutafakari, nimegundua kwamba pale ambapo mtoto anapewa
chakula chochote zaidi ya maziwa basi ni sawa apewe maji kwa kiasi
Fulani,
kwani
tayari mwili wake unapokea chakula kigumu na huitaji maji zaidi.
Kwa
upande mwingine, sioni sababu ya kumpa mtoto maji endapo anapata maziwa katika
kiasi kilicho sahihi kwa mwili wake na anashiba.
Ila kinachonitia
wasiwasi ni uwezekano wa mtoto kupata maziwa yakutosha.
Kwa
maisha yetu ya kitanzania Gharama ya kumlea mtoto kwa kumpa maziwa ya
kopo ni kubwa sana na wazazi wengi hawawezi kumudu gharama hizo.
Gharama
za maziwa ya ng’ombe pia ziko juu na maziwa niyashida hasa kwenye miji mikubwa
hivyo ni ngumu kwa mwananchi wa kipato cha kawaida na cha chini kufidia lishe
ya mtoto kwa kuongeza maziwa hayo yakununua.
Hii
humlazimu mzazi kumuanzisha mtoto uji mapema ili kufidia lishe yake. Jambo
linalopelekea mtoto kula chakula kigumu na kunywa maji akiwa chini ya miezi
sita .
Hata
hivyo ni vyema kujua kwamba ingawa kuna kiasi au kipimo Fulani cha maziwa
ambacho mtoto anatakiwa kupewa si kweli kwamba watoto wote hushiba kwa kipimo
hicho.
Watoto
hutofautiana ukubwa wa mwili kitu ambacho hufanya hata kula yao itofautiane.
Kwa
mantiki hiyo basi ni wazi kwamba watoto wa rika moja si lazima wapewe kipimo
sawa cha maziwa, tofauti ya hatua tano juu ya kipimo cha kawaida huruhusiwa.
Ushauri
Wangu ni
kwamba pale ambapo mtoto anapewa chakula chochote zaidi ya maziwa basi ni sawa
apewe maji kwa kiasi Fulani,
kwani
tayari mwili wake unapokea chakula kigumu na huitaji maji zaidi ili kusaidia
uyeyushwaji
wa chakula katika mwili.
Kwa
upande mwingine, sioni sababu ya kumpa mtoto maji endapo anapata maziwa katika
kiasi kilicho sahihi kwa mwili wake na anashiba.
Kumbuka
tu kwamba ukosefu wa maji mwilini pia huzaa matatizo makubwa ya afya kwa mtoto.
MAJI NI
UHAI
Asante sana
ReplyDeleteHongera sana mtalaam umeongea kwa research na undani zaidi. Nimekuelewa sana. Ubarikiwe
ReplyDelete