Sunday, 4 May 2014

JE, UNAJUA NJIA MBALIMBALI ZA UZAZI WA MPANGO UNAZOWEZA KUTUMIA? CHAGUO NI LAKO!!!



 
Inakadiriwa wanawake 222,000,000 katika nchi 
 
zinazoendelea wangependa
 
 kuchelewa au kuacha kuzaa lakini hawatumii njia yoyote ile 
ya uzazi wa mpango.
 
Baadhi ya mbinu za uzazi wa mpango husaidia
 
kuzuia maambukizi ya VVU na magonjwa mengine ya zinaa.
 
Uzazi wa mpango unaruhusu watu kufikia idadi yao ya 
 
watoto wanaotaka  na
 
kuamua nafasi ya mimba moja na nyingine.

 
Vidonge vyakumeza vyenye vichocheo vya aina mbili.
 
Njia ya vidonge vyenye vichocheo vya aina mbili yaani 
 
Estrogen na Progesterone humezwa na mama kila siku kwa 
 
ajili ya kuziuia mimba.
 
Ni rahisi kutumia, mama anaweza kupata mimba mara 
 
atakapoacha kumeza vidonge hivi
 
Kwa baadhi ya wanawake matumizi ya vidonge hivi hasa 
 
katika miezi ya mwanzo, huweza
 
Kuleta maudhi kama vile mabadiliko
 
Katika mzinguko wa hedhi.
 
Njia hii ni ya uhakika na salama ikitumiwa
 
Kwa usahihi
 
Njia hii inaweza kutumiwa na mwanamke
Wa umri wowote ambaye ameishapata
 
Watoto au bado.
 
Husaidia kuziua aina Fulani za saratani,
 
Upungufu wa damu(madini joto),
 
Hupunguza maumivu ya tumbo wakati wa hedhi.
 
Na hufanya mzunguko wa hedhi kuwa katika mzunguko wa hedhi kuwa katika mpangilio
 
Mzuri.
 
Vidonge vya aina hii huweza kutumika
 
Kama njia ya dharura ya kuzuia mimba mara baada ya 
 
kujamiiana bila kinga

 
VIDONGE VYA KUMEZA VYENYE KICHOCHEO
 
CHA AINA MOJA.
 
Njia hii ni ya vidonge vyenye kichocheo cha aina
 
Moja cha (progesterone) na humezwa na mwanamke kila siku kwa ajiri ya kuzuia mimba.
 
Ni rahisi kutumia
Mwanamke anaweza kupata mimba mara atakapoacha 
 
kumeza vidonge hivi,
 
Njia hii inafaa kwa kina mama anayenyonyesha kuanzia wiki 
sita baada ya kujifungua,
 
Vidonge hivi vinaweza kutumika pia kama njia ya dharura ya kuzuia mimba mara baada ya kujamiiana bila kinga.



 
KONDOMU
 
Kondomu zinaweza kuzuia mimba na magonjwa yatokanayo na kujamiiana ikiwa ni pamoja na UKIMWI,
Kondomu ni rahisi kutumia, kondomu ni ya uhakika kwa 
 
usahihi.

 
NJIA ZA MAUMBILE
 
Hizi ni njia za uzazi wa mpango kwa mwanamke kwa 
 
kutumia kalenda, joto la mwili na kuangalia ili kufahamu siku za kuweza kupata mimba.
 
Katika njia hizi mwanamke hutambua siku anazoweza kupata mimba katika mzunguko wake wa hedhi na kuacha 
 
kujamiiana ili asipate mimba.
 
 Kwa kufahamu hivyo mwanamke na mwanaume wanaweza kuepuka kujamiiana au kujamiiana kwa kutumia kondomu,
 
Njia hizi ni za uhakika iwapo kutakuwepo ushirikiano wa karibu kati ya mwanamke na wanaume.
 
Uhakika wa njia hii katika kuzuia mimba sio wa kiwango cha 
juu.

 
NJIA ZA UZAZI WA MPANGO ZA KUWEKA UKENI
 
(jeli na vidonge vya povu) NA KIWAMBO.
 
Njia hizi zinajumuisha jeli, vidonge vya povu na kiwambo.
 
Mwanamke anaweka dawa jizi ukeni dakika chache kabla ya kujamiiana ili kuzuia mimba.
 
Njia hizi zina uwezo wa kuzuia mimba iwapo zinatumika kwa usahihi.
 
Uhakika wa njia hizi katika kuziia mimba sio wa kiwango cha juu.

 
NJIA YA UNYONYESHAJI BAADA YA KUJIFUNGUA.
 
Hii ni njia ya kuzuia mimba ambayo mwanamke anayenyosha anaweza kutumia kwa kipindi cha miezi sita ya kwanza 
 
mara baada ya kujifungua.
Njia hii ni ya uhakika endapo Mama;
· 
       Hatakaa zaidi ya masaa 4 bila kumnyonyesha mtoto wakati wa mchana na masaa 6 wakati wa usiku.
 
·       Mama ananyonyesha mtoto bila kumpa chakula kingine chochote kwa kipindi cha miezi 4 na 6 baada ya kuzaliwa.
·       Mama hajaanza kupata hedhi tena baada ya kujifungua.
·     
  Ni vyema mwanamke apange kuanza kutumia njia nyingine ya uzazi wa mpango pale atakapoacha kutumia njia hii ya 
 
unyonyeshaji.


 
SINDANO (DEPO PROVERA)
 
Hii ni njia ya uhakika na salama
 
Sindano moja huchomwa kila baada ya miezi mitatu.
Inaweza kutumiwa na mwanamke wa umri wowote ambaye 
 
tayari ameshapata watoto au bado.
Si rahisi kwa mteja kujulikana kama anatumia njia hii ya 
 
uzazi wa mpango.
 
Njia ya sindano ni salama kwa mama anayenyonyesha na ambaye ametimiza wiki 6 baada ya kujifungua
Huchukua wastani wa miezi4 hadi 9 kabla ya mwanamke 
 
anayeacha kutumia njia hii
Kupata mimba.
 
Mwanamke anaetumia njia hii anaweza kupata mabadiliko katika mzunguko wake wa hedhi
 
Pia, sindano inaweza kusaidia kupunguza maradhi ya 
 
saratani ya kizazi.

 
VIPANDIKIZI (NORPLANT)
 
Ni Njia ua uzazi wa mpango iliyo katika muundo wa mirija ya plastiki yenye kichocheo (homoni) kimoja 
 
(progesterone)
 
Vipandikizi huwekwa juu ya ngozi
Ya mkono wa mwanamke
 
Njia hii ni ya uhakika na inaweza kuzuia mimba kwa muda wa miaka MITANO au zaidi.
 
Vipandikizi vinaweza kuondolewa wakati wowote mwanamke anapoamua kupata mimba.
 
 Njia hii ni salama katika kipindi cha kunyonyesha kuanzia wiki  6 baada ya kujifungua,
 
Njia hii husaidia kupunguza matatizo ya upungufu wa damu na kutungwa mimba nje ya mji wa mimba.
 
Mwanamke anaetumia njia hii anaweza kupata mabadiliko katika mzunguko wake wa hedhi au kutokupata kabisa 
 
hedhi.
 
Aidha maumivu kidogo ya kichwa yanaweza kutokea.


 
LUPU (LOOP)
 
Ni kifaa kidogo cha plastiki ambacho huwekwa kwenye mji wa mimba ili mimba isitunge.
 
Njia hii ni ya uhakika na inaweza kuzuia mimba kwa kipindi cha miaka 12
 
Mwanamke anaweza kupata mimba mara tu anapoacha kutumia lupu.
 
Mwanamke anapaswa kugusa vinyuzi viwili vya lupu ukeni kila anapo maliza hedhi.
 
Njia hii haifai kwa mwanamke mwenye kujamiiana na mpenzi zaidi ya mmoja au mwenzi wake ana wapenzi 
 
wengi.

 
KUFUNGA KIZAZI MWANAUME
 
Hii ni njia ya kidumu ua uzazi wa mpango kwa mwanaume,
Njia hii hutumika wakati mke/mwenzi na mwanaume au mwanamke kwa hiari yake/yao wameridhika na idadi ya 
 
watoto walio nao.
Hii  njia ni ya uhakika na salama inayohitaji
 
Upangaji mdogo
Mteja hahitaji kulazwa hospitalini kabla au baada ya upasuaji.
 
Baada ya upasuaji mteja anashauriwa atumie njia nyingine ya uzazi wa mpango katika kipindi cha miezi 3 ya mwanzo.
 
Njia haitaathiri uwezo na hamu ya kijamiiana, Nguvu za kiume haziathiriki baada ya ufungaji wa kizazi kwa 
 
mwanaume.

 
KUFUNGA KIZAZI MWANAMKE.
 
Hii ni njia ya kudumu ya uzazi wa mpango kwa mwanamke,
 
Njia hii hutumika wakati wa mume/mwenzi na mke au mwanamke kwa hiari yake wameridhika na idadi ya watoto walio nao.
 
Hii ni njia ya uhakika na salama inayohitaji upasuaji mdogo.
Mteja hahitaji kulazwa hospitali kabla au baada ya 
 
upasuaji huu.
Mteja hahitaji kuhudhuria kliniki mara kwa mara.
 
Njia hii haiathiri uwezo na hamu ya kujamiiana. Mwanamke huendelea na kupata hedhi kama kawaida.


TAHADHARI
 
Kuna njia za uzazi wa mpango ambazo mwanamke anashauriwa kutozitumia akiwa na hali Fulani kiafya.
·        
Vidonge vya kumeza vyenye vichocheo aina mbilimbili 
 
(combined oral contraceptives) havishauriwi kwa 
 
mwanamke ambaye ni;
 
+ Mwenye umri wa miaka 35 na zaidi na    anavuta 
 
sigara.
+ mwenye matatizo ya shinikizo la damu
 
+ ananyinyesha katika miezi 6 baada ya kujifungua.
+ akiwa na matatizo ya moyo, mishipa ya
damu na pia magonjwa ya ini.
 
+Mwanamke akiwa na mimba .
+ Mwanamke mwenye kuumwa kichwa mara
kwa mara.

 
·       SINDANO (DEPO PROVERA)
 
Njia hii ya uzazi wa mpango haishariwi kutumiwa iwapo 
 
kama mwanamke;.
 
+ Ana matatizo ya shinikizo la damu (high blood pressure)
+ akiwa na matatizo ya moyo, mishipa ya
damu na pia magonjwa ya ini.
+ Mwanamke akiwa na mimba.

 
 LUPU (LOOP)
 
Njia hii ya uzazi wa mpango haishauriwi kutumia iwapo;
 
+ mwanamke ana uambukizo katika mji wa mimba au viungo 
vya uzazi
 
+ Mwanamke anajamiiana na wapenzi zaidi ya mmoja au endapo mwenzi wake anajamiiana na wapenzi wengi.
 
+ Mwanamke akiwa na mimba.
 
VIPANDIKIZI (NORPLANT)
 
Njia hii ya uzazi wa mpango haishauriwi kutumia iwapo;
 
+ Mwanamke ananyonyesha wiki 6 za mwanzo baada ya kijifungua.
+ mwanamke akiwa na mimba.

VIDONGE VYENYE KICHOCHEO CHA AINA MOJA 
 
(Progesterone).
 
Njia hii ya uzazi wa mpango haishauriwi kutumia iwapo;
 
+ Mwanamke ananyonyesha wiki 6 za mwanzo baada ya kijifungua.
+ mwanamke ana na matatizo magonjwa ya moyo, mishipa ya
Damu.
+ mwanamke akiwa na mimba

KWA MAELEZO ZAIDI YA NJIA HIZI ZA UZAZI WA MPANGO MUONE MUHUDUMU WA AFYA YA UZAZI NA WATOTO.

0 comments:

Post a Comment