Sunday, 4 May 2014

ATHARI ZA KUTOA MIMBA





ATHARI ZA KUTOA MIMBA

 
“NISEME?” Aliniuliza binti mmoja, tena kwa
hofu kubwa wakati namhoji juu ya matatizo
yawapatayo baadhi ya wasichana
wanaodiriki kutoa mimba, hasa kienyeji,
ikimaanisha bila ya kupitia kwa madaktari
wenye taaluma sahihi ya uzazi na magonjwa
 
ya wanawake.

Binti huyu alivuta pumzi, akawa kimya.
Ndipo akasema; “matatizo hayo yamenisibu
mimi mwenyewe, nimeghilibiwa na kijana
mmoja na pesa zake ya kuwa nizae nae
ndipo atakaponioa. Kwa akili ya kitoto na
tamaa ya vyote, pesa na kuolewa, nikakubali
 
kushika mimba.

“Mwenzangu akaniaga anasafiri mimba
ikiwa miezi mitatu. Lakini baada ya muda
akanitumia ujumbe kuwa hiyo mimba si
 
yake, mimi ni mhuni tu nisieaminika na
nitafute wa kumpa mimba hiyo “Moyo
ulinipasuka, nilichoamua ni kuitoa mimba
 
 
kwa kumeza vidonge kibao vya klorokwini.
Nilipatwa na uchungu mkali, mimba
ikapuruchuka nikapoteza fahamu nikajikuta
 
siku ya tatu hospitalini nikiwa na hali mbaya.
Niliponea chupuchupu kufa, na najutia
kitendo hicho kwani sasa ni miaka sita
sijashika mimba tena. Je, utanisaidiaje mzee
 
wangu?”

 
Tatizo la utoaji mimba hapa nchini ni kubwa
sana ingawa bado utafiti unaendelea
 
kufanyika.
 
Imegundulika kuwa kati ya mimba 100
zinazoharibika, 80 zinatokana na wanawake
‘kuzichokonoa’ wenyewe na hizi ndizo
ninazozizungumzia.

 
Zile mimba ambazo zinaharibika zenyewe,
wahusika wanapofika hospitalini
husafishwa na wengine wanalazimika
kufanyiwa upasuaji na maisha yakaendelea
 
bila tabu.
Kadhalika katika wodi ya dharura ya
wanawake imegundulika kuwa nusu ya
idadi ya mimba zimeharibika kwa kutolewa
 
kienyeji.

 
Kati ya watoto 100,000 wanaozaliwa, 454
hufa kutokana na uchokonolewaji
(abortion) wa mimba ambao ni sawa na
asilimia 16-19, na hufuatiwa na vifo.
Madhara ya utoaji mimba
 
Madhara yanayoambatana na utoaji mimba
ni vifo, kupoteza damu nyingi, kifafa cha
uzazi na maambukizi hatarishi katika mfuko
wa uzazi au mirija ya uzazi.

Haya yote yanaambatana na homa kali na
maumivu makali, kutunga usaha kwenye
kizazi na kulazimika kufanyiwa upasuaji wa
dharura au haraka kitaalamu; kikubwa mara
 
nyingi ni kifo.

Mhusika kama akipona kutokana na athari
ya kuichokonoa mimba visivyo au kwa
nguvu sana, wakati mwingine husababisha
 
uharibifu wa mfuko wa uzazi na mirija yake,
na hubakiwa na makovu kwenye ile ngozi
laini ya mfuko wa uzazi, ambayo
humsababishia maumivu makali
anapokaribia siku zake za hedhi ama
kuupoteza mzunguuko wake.
 
 Hii ni kwa
 
muda mrefu au milele. Kitaalamu wanaita ni
kupoteza heshima ya uzazi (quality of life).
Athari nyingine ni kufungwa kwa kizazi,
kwamba mirija ya uzazi ikijifunga basi
mwanamke huyo hawezi tena kuzaa
 
maishani mwake.
 
Kutokana na kujifunga kwa mirija ya uzazi,
athari ni kuwa mbegu ya yai la mwanaume
ambayo ni ndogo hujipenyeza na kuingia,
na mbegu ya yai la mwanamke ambayo ni
 
kubwa hupita na yanapokutana kusabibisha
mimba kutunga nje ya kizazi, ambayo
kitaalamu huitwa “ectopic pregnancy”.
Kwa kuwa mimba hiyo iko nje ya mazingira
 
ya kawaida, inaweza ikapasuka na kupoteza
damu nyingi na kusababisha kifo na
ikiwahiwa ni kufanyiwa upasuaji na
kulifunga eneo hilo.

 
 
Athari nyingine ni ugumba ambao kitaalamu
unajulikana kama “infertility”. Hali hii
inatokana na uharibifu wa mazingira ya
mpango wa mfuko wa uzazi na hasa kwa
uchokonoaji wa mimba, hivyo kufungwa
kwa kizazi, pengine hedhi inakoma na kwa
kutopata hedhi wanawake wengi
huchanganyikiwa.

 
Tatizo hili la ugumba huwa linasababishwa
na kukwanguliwa kwa ile ngozi laini
inayozunguka tumbo la uzazi.
Kukwanguliwa huko kunatokana na ama
vifaa vinavyotumiwa kuichokonoa mimba
hiyo au madawa makali.

Athari nyingine kama uchokonoaji umepita
kiasi na kufikia kwenye utumbo mkubwa
huathirika na kusababisha utumbo
kutobolewa na kuwekwa mrija wa kutolea
choo kikubwa.
Vile vile hali hiyo usababisha ugandaji wa
damu kwenye mishipa ya fahamu kuelekea
kwenye ubongo. Hii ni hatari mno, kwani
inasababisha mhusika kuwa na hali kama ya
kiharusi.

Kutokana na athari hizo na hasa ugumba,
wanawake hupatwa na msongo mzito wa
mawazo na kuchanganyikiwa kisaikolojia,
hivyo huanza kuwa na tabia za ajabu za
hasira na hata chuki kwa wenzao wenye
watoto na hata kuwachukia watoto wa
wenzao pasipo sababu za msingi. Wanajihisi
wamekosa ule ubora wa kuitwa
mwanamke.
Hapa nchini, sheria inayoruhusu kutoa
mimba haipo, hivyo jambo hili ni kosa na
hivyo hufanywa kwa kificho, pengine katika
mazingira yasiyofaa, kukosa ujuzi wa
kitaalamu na vifaa visivyo sahihi.
Wakati mwingine ni wasichana wenyewe
hushawishiana jinsi ya kutoa mimba na
kusasabisha madhara yote haya.

Baadhi ya wasichana baada ya kukumbwa
na tatizo la ugumba hujifariji kuwa ati
wamebaki na uzuri wao na hapo hujiingiza
kwenye biashara haramu ya kuuza miili yao
na kujiweka kwenye hatari ya maambukizi
ya magonjwa ya ngono na kupata ukimwi
pia.

Kutoa mimba huleta ulemavu wa maisha,
kutokuzaa kabisa na ni kifo. Natoa rai kwa
wanawake wote waachane na tabia hiyo ya
kuzichokonoa mimba, na waachane na
kubeba mimba wasizozipanga, pia waepuke
tamaa za maisha ya starehe kwani
zinawatumbukiza kwenye majanga.

0 comments:

Post a Comment