Sunday, 4 May 2014

DALILI NA ISHARA ZA UJAUZITO










Dalili za ujauzito hutofautiana kati ya mwanamke na mwanamke, ingawa kuchelewa au kukosa hedhi ni dalili moja muhimu sana
Ni muhimu kuzitambua na kuzifahamu dalili hizi kwa sababu zinaweza kusaidia kuelezea au kutofautisha matatizo mengine mbali ya ujauzito.
Hebu sasa tuangalie dalili na ishara za Ujauzito:
  • Kutokwa damu kidogo ukeni wakati kiumbe kikipandikizwa kwenye mfuko wa uzazi, ingawa siyo wanawake wote hupatwa na dalili hii
  • Kukosa hedhi, hii ni moja ya dalili kubwa za ujauzito
  • Maumivu ya matiti na kuvimba matiti (huweza kutokea kati ya wiki ya 1 hadi ya 2)
  • Uchovu, wanawake wengi hujihisi uchovu na hali ya kutopenda kufanya lolote.
  • Kupoteza ladha au kuhisi ladha ya chuma mdomoni
  • Kuongezeka kwa hisia ya harufu, kipindi cha ujauzito wanawake wengi huongezeka hisia ya harufu
  • Kichefuchefu na kutapika
  • Maumivu ya kichwa
  • Kizunguzungu
  • Kukojoa mara kwa mara (hasa kati ya wiki 6-8)
  • Kubadilika rangi kwa ngozi inayozunguka chuchu kuwa nyeusi
  • Kutamani baadhi ya vyakula na kuchukia vingine
  • Kupanuka kwa mfuko wa uzazi
  • Tumbo kujaa au kuvimbiwa
  • Kununa na kukasirika haraka
  • Kiungulila au kupata choo kigumu
  • Kolostramu kuanza kutoka kwenye matiti
  • Kuongezeka uzito
  • Kuweza kupapasa mtoto (palpation of the baby)
  • Kulainika na kuvimba kwa shingo ya uzazi (Hegars sign) - kuanzia wiki ya 6
  • Shingo ya uzazi kubadilika rangi kuwa ya samawati kutokana na msongamano wa damu katika mishipa ya vena. Ishara hii huitwa pia Chadwick's sign
Dalili nyingine ni pamoja na
  • Mstari wima mweusi hutokea tumboni kuanzia chini ya kitovu (linea nigra)
  • Mama kuhisi mtoto akicheza (kuanzia wiki ya 20)
  • Maumivu ya mgongo hasa mimba ikishakuwa kubwa.
  • Kipimo cha mimba kuwa chanya (positive).
  • Kusikia mapigo ya moyo ya mtoto
  • Mtoto kuonekana kwenye kipimo cha ultrasound

Related Posts:

  • KUTOKWA NA MAJIMAJI SEHEMU ZA SIRI Tatizo hili huwatokea wanawake na wanaume. Mwanaume hutokwa na majimaji katika njia ya mkojo, mwanamke hutokwa na majimaji haya katika njia ya mkojo au ukeni.Majimaji haya yanaweza kuwa mepesi au mazito, pia yanaweza kuwa… Read More
  • MATATIZO YANAYOSABABISHA MWANAMKE ASISHIKE MIMBA MWANAMKE kutoshika mimba kumegawanyika katika makundi makubwa mawili. Kwanza ni hali iitwayo ‘primary Infertility’ ambapo mwanamke hana historia ya kupata ujauzito. Pili kuna hali iitwayo ‘Sekondari Infertility’, hapa m… Read More
  • MAGONJWA NYEMELEZI KWA WANAWAKE- 6 Ugonjwa huu huanza ghafla na dalili zake ni kama homa kali, kikohozi, maumivu wakati wa kupumua, baridi na kutetemeka. Ugonjwa wa Ngozi:Huu husababishwa na vimelea vya Staphylococcus aureus.Vimelea hivi huishi katika mw… Read More
  • SABABU ZA TATIZO LA KUTOPATA MIMBA - 2 Mpenzi msomaji, naendelea kuelezea sababu za mwanamke kutoweza kupata ujauzito. Tuwe pamoja...Wanaume wengi wanashindwa kumpa mimba mwanamke kutokana na kutumia dawa  hovyohovyo au kuwa na matatizo ya tezi za thyroid… Read More
  • SABABU ZA TATIZO LA KUTOPATA MIMBA - 3 Naendelea kuelezea mambo yanayosababisha mwanamke kutopata mimba. Endelea... Kipimo cha upevushaji wa mayai kupima mirija ya uzazi, upasuaji mdogo kwenye tumbo na kumulika ndani ya mwili wake pia kipimo cha Ultrasound kit… Read More

0 comments:

Post a Comment