Sunday 4 May 2014

FAHAMU KUWA SI KILA MWENYE KIFUA KIKUU ANA MAAMBUKIZO YA V.V.U




MGONJWA MMOJA, MAGONJWA MAWILI
          

UKIMWI na kifua kikuu ni magonjwa mawili yanayosababisha vifo vingi, hivyo ni muhimu kuelewa uhusiano uliopo kati ya UKIMWI na Kifua kikuu.

 Virusi vya UKIMWI (V.V.U) Hupunguza kinga ya mwili na kuuacha mwili bila kinga ya kutosha dhidi ya magonjwa mbalimbali ukiwemo ugonjwa wa kifua kikuu.
Kifua kikuu ni ugonjwa wa kuambukiza unaojitokeza baada ya upungufu wa kinga mwilini.
          Kuanzia miaka ya 1990s upungufu wa kinga mwilini unaosababishwa na maambukizo ya virusi vya UKIMWI (v.v.u) umetokea kuwa ni sababu kubwa ya ongezeko la ugonjwa wa kifua kikuu hasa watu wenye umri kati ya miaka 15-49. Umri huu unafanana na ule wa wengi walioathirika na maambukizi ya  V.V.U
 

MUINGILIANO HUU UNASABABISHA MGONJWA MMOJA KUWA NA MAGONJWA MAWILI UNATHIBITIKA KATIKA TAKWIMU AMBAPO;












     ·      Asilimia 40-49 ya wagonjwa wa kifua kikuu hugunduliwa kuwa na VVU.
    ·      Wastani wa asilimia 30 ya vifo vitokanavyo na UKIMWI nchini husababishwa na kifua kikuu.
    ·      Mtu mwenye maambukizo ya VVU ana uwezekano wa mara 10 zaidi wa kuoata ugonjwa wa kifua kikuu ukilinganishwa na mtu ambaye hana VVU
    ·      Magonjwa ya kifua kikuu na UKIMWI yakijitokeza pamoja hali ya mgonjwa huathirika zaidi, iwapo magonjwa yote haya hayatotibiwa pamoja, mgonjwa huchelewa kupona na huenda akapoyeza maisha yake.
    

KWA MGONJWA WA KIFUA KIKUU.

Kutokana na uhusiano kati ya kifua kikuu na UKIMWI , wagonjwa wote wa kifua kikuu wanapaswa kutambua iwapo wana maambukizi ya VVU.

Huduma hii ya kupima VVU hupatikana katika kituo chako au utapewa rufaa upate huduma hii katika kituo chako cha huduma/tiba ya walioathirika na VVU Iwapo haipatikani. Ushauri nasaha na kupima


VVU –DIAGONOSTIC COUNSELING AND TESTING (DCT)
Huu ni ushauri nasaha elekezi ambao mhudumu wa afya humnasihi mgonjwa kuhusu hali yake na faidi yakufanya uamzi wa kupima VVU. Baada ya kupima mgonjwa anapata fursa ya kufaidika na huduma zilizopo hata kama hana maambukizi ya VVU.


FAHAMU KUWA SI KILA MWENYE KIFUA KIKUU ANA MAAMBUKIZI YA V.V.U.
·      Ukiwa hukugundukulika kuwa na VVU; hii ni habari njema kwako na utashauriwa kuendelea na ushauri nasaha wa hiari VCT ili kuendelea kuishi bila ya maambukizi ya VVU, pia kumbuka unahitaji kuendelea na tiba simamizi ya kifua kikuu ambayo ni lazima kumaliza bila kuacha hata dozi kimoja
·      Ikiwa umegundulika una VVU; Ni habari njema kwako pia kwani kuifahamu hali yako kutakupa nafasi kubwa ya kutumia huduma shirikishi zilizopo na kuboresha afya yako.

UCHUNGUZI ZAIDI WA DAMU
Vipimo vikionyesha una maambukizo ya VVU utafanyiwa vipimo zaidi vya damu ili kutambua kiwango cha upungufu wa kinga yako ya mwili na kiasi cha maambukizo ya VVU ulichonacho mwilini.
Vipimo hivi vinamsaidia Daktari wako kuweza kuamua kama akuanzishie dawa za kupunguza makaili ya maambukizo ya VVU kulingania na kigezo cha kitaifa cha kuanza dawa hizi.
       
DAWA ZA KUPUNGUZA MAKALI YA VVU.

Daktari ndie anayeamua kukuanzishia  dawa za kupunguza makali  ya VVU kulingana na vipimo.
Utapewa dawa za mseto ambazo utazitumia kila siku na kwa kipindi cha maisha yako yote bila kukosa dozi.

Dawa hizi zitaboresha kinga ya mwili wako na kukufanya uweze kuendelea kuwa na afya na kufanya shughuli zako za kawaida pamoja na dawa za kifua kikuu, dawa hizi zitakusaidia kupona kifua kikuu kwa haraka zaidi.
       
TIBA KAGAJI (PROPHYLAXIS)
Tiba hii hutolewa kwa mgonjwa wa UKIMWI au mwenye kifua kikuu/UKIMWI kujikinga na magonjwa nyemelezi.

KWA MGONJWA MWENYE MAAMBUKIZO YA VVU/UKIMWI
Maambukizi ya VVU hupunguza kinga ya mwili hivyo kumfanya alieathirika kuwa katika hatari ya kupata ugonjwa wa kifua kikuu wakati wowote.
Karibu asilimia 33 ya wenye VVU hugundulika kuwa na kifua kikuu, ni muhimu mwenye maambukizi ya virusi  vya UKIMWI kufanya uchunguzi wa kifua kikuu mara kwa mara.
      

 IWAPO UTAONYESHA UNA KIFUA KIKUU

Utaanzishiwa dawa za kifua kuu chini ya usimamizi, dawa hizi ni za mseto na utameza kila siku bila kukosa kwa muda wa miezi sita.
    
   Utachagua ni wapi utamezea dawa chini ya usimamizi, katika kituo cha huduma ya afya au katika jamii yako
        Dawa za kifua kikuu hutolewa bure bila malipo yoyote
        Baada ya kukamilisha matumizi ya dawa za kifua kikuu na kupona utaendelea na huduma za dawa za kupunguza makali ya VVU za ARVs ( ikiwa ulikuwa na Kifua kikuu pamoja na UKIWMI)

  
 BORESHA AFYA YAKO KAMA UNA KIFUA KIKUU AU KIFUA KIKUU/UKIMWI
          AMUA; mapema kufanya uchunguzi zaidi wa afya yako ili kufahamu kama una ugonjwa mmoja au magonjwa yote
      
TUMIA DAWA ZA MSETO;
 kila siku bila kukosa kama ulivyoelekezwa na wataalamu wa afya, wahi kutoa taarifa katika kituo chako cha huduma iwapo utakuwa na tatizo lolote wakati wa huduma.
          
LISHE;
 kula vyakula mchanganyiko kwani mwili wako unahitaji kuwa na nguvu, kujijenga na hasa kuijenga kinga ya mwili ili kusaidia dawa kupambana na vimelea vya magonjwa.
       
 JENGA TABIA
; ya kutafuta habari za elimu ya afya kwa kusoma Blog kama hii ya masuala ya afya, vyombo vya habari, majarida ya afya na kuhudhuria vipindi vya elimu ya afya katika kituo chako cha huduma.
         
JENGA MAHUSIANO
 ya kuwa karibu na wasimamizi wa kumeza dawa na wataalamu wa afya ili kupata elimu na ushauri kuhusu maendelea ya Afya yako.

“Pambana na kifua kikuu pambana na UKIMWI”
 

Pambana sasa

0 comments:

Post a Comment