Sunday 4 May 2014

KUMBUKA CHANJO YA KIFUA KIKUU /(BCG) ITAMKINGA MTOTO DHIDI YA UGONJWA WA KIFUA KIKUU (TB)




KIFUA KIKUU (TB)

Kifua kikuu ni ugonjwa unaosababishwa na vimelea vya bacteria na kuenezwa kwa njia ya hewa. Mtu mwenye 
maambukizi ya kifua kifua kikuu akikohoa, kupiga chafya 

au kutema mate ovyo husambaza vijidudu hivyo hewa, 
huweza kumwabukiza mtu mwingine kama atakuwa hajaanza kutumia dozi ya kifua kikuu.

DALILI ZA KIFUA KIKUU (TB)

vKukohoa kwa muda wa wiki mbili au zaidi

vMaumivu ya kifua

vHoma za usiku

vKutoka jasho kwa wingi usiku

vKupungua uzito

vKukohoa damu

vKukosa hamu ya chakula na mwili kuwa dhaifu

    ATHARI ZA KIFUA KIKUU (TB)


vUgonjwa huweza kuenea kwenye viungo vingine vya mwili

vWatu wengine hupoteza maisha iwapo hawatapata tiba sahihi mapema

vWatu wengine huambukizwa ugonjwa katika muda mfupi

vWagonjwa wa kifua kikuu hawazezi kushiriki kikamilifu katika shughuli za maendelea

vMatibabu ya kifua kikuu huchua muda mrefu na ni gharama kubwa

KINGA


 
Ugonjwa huu unakingwa kwa chanjo ya kifua kikuu kwa kitaalamu (BCG) ambayo hutolewa mara tu motto anapozaliwa.

§  Ili kupunguza uwezekano wa kupata kifua kikuu zingatia yafuatayo;

  Kujenga na kuishi kwenye nyumba zinazoruhusu mzunguko kwa hewa ya kutosha (ziwe na madirisha makubwa ya kutosha)

Epuka kukaa kwenye msongamano wa watu wengi

Watoto wanyonyeshwe maziwa ya mama pekee kwa miezi sita na umlikiza kwa vyakula vyenye virutubisho ili kumjengea kinga imara

Kula vyakula vyenye lishe bora

 Kutotema mate na makohozi ovyo ili kuziua usambaaji wa bacteria wasababishao Kifua kikuu.


RATIBA YA CHANJO


Chanjo ya kifua kikuu hutolewa baada ya motto kuzaliwa au anapofika kliniki kwa mara ya kwanza

Iwapo kovu kwa motto halijajitokeza chanjo irudiwe katika kipindi cha miezi 3.



TIBA YA KIFUA KIKUU (TB)


  Ugonjwa wa kifua kikuu unatibika.

Matibabu yake huchukua muda mrefu wa miezi 6 hadi 8 na ni ya gharama kubwa.

Inashauriwa mgonjwa awahi matibabu mapema kwenye vituo vya kutolewa huduma za kinga.

UJUMBE


vUgonjwa wa kifua kikuu ni hatari, hata hivyo unakingwa kwa chanjo.

vMzazi au mlezi hakikisha kila motto anapozaliwa anapata chanjo ya kuzuia kifua kii

 

Kumbuka chanjo ya kifua kikuu (BCG) Itamkinga mtoto dhidi ya ugonjwa wa kifua kikuu”

0 comments:

Post a Comment