Sunday 18 May 2014

AMARANTHUS -MCHICHA ASILI KWA AFYA BORA




Mchicha wa kipekee wa amaranthus sasa unapatikana toka Mombasa ukiwa katika hali ya unga,ukiwa umefungwa vizuri kwenye kifungashio maalum katika hali ya unga.

Mchicha huu ni lishe bora kwa mtu yeyote hasa usaidia ubongo kuwa mchangamfu(Brain activator), na ianimarisha na kuongeza kinga ya mwili,pia kutokana na ulimaji wa sasa wa michicha yetu ya leo si salama kutokana na kemikali nyingi zitumikazo katika ulimaji huo,hivyo kwa sasa mimi nimeamua kutumia lishe ya mchicha huu asili ambao unastawi sana uko sehemu za Mombasa na Malindi nchini Kenya.

Lishe hii utaitumia kama unavyotengeneza uji kwani unamimina maji vikombe viwili kwenye sufuria,kisha unaweka vijiko viwili vya unga huu na kukoroga na kubandika kwenye moto,ukianza kuchemka tuu unautoa ,utamimina kwenye kikombe na baada ya kupoa kidogo utakunywa lishe hii,nzuri kutumia baada ya kupata mlo.




Scientific name: Amaranthus viridis 

MAELEZO 

Kiswenya kithithe ni neno la Kigiryama linalomaanisha kwa kiswahili mchicha mdogo. 

Sababu ya kuitwa jina hili ni kwamba mboga hii ina majani madogo tena haikui sana kwenda juu. 

Kiswenya kithithe ni kama kiswenya kibomu lakini tofauti yake ni kwamba kiswenya kithithe kina majani madogo zaidi. 

Mmea wake ni mfupi sana kama robo futi. 

Mti wake unateleza na rangi yake ni mchanganyiko wa kijani na maji ya kunde. 

Mboga hii mara nyingi hupatikana wakati wa mvua nyingi ya mwaka na ya vuli kuanzia Aprili hadi karibu na Desemba. 

Kiswenya kithithe kinapopata maji kwa wingi utakuta ya kwamba mti wake uko na rangi ya kijani kibichi na pasipo na maji ya kutosha huonekana dhaifu, majani huanza kukauka na mti wake hugeuka kuwa mwekundu. 

Kina mama wanasema mboga hii ya kiswenya kithithe ni ya pili kwa utamu ikiwa ya kwanza ni kiswenya cha miya. 

IKOLOJIA/UKUZAJI 

Humea kando kando ya miji bila ya kupandwa kwenye mashamba hasa kwa maboma. 

Kiswenya kithithe hupatikana kwa wingi wakati wa mvua nyingi ya mwaka na ya vuli kuanzia mwezi wa nne hadi wa kumi. 

Hupandwa kutokana na mbegu au hata mti wake unakua vizuri unapopata maji vizuri humea ukipandwa. 

Inamea sehemu za Kilifi, Kwale, Mombasa na Malindi kwenye aina yoyote ya mchanga bila kupandwa kwenye shamba. 

Mboga hii unaweza kuipanda pia ukipenda kwa kumwaga punga zake shambani. 

MAANDALIZI NA UPISHI 

Kina mama husema kuwa mboga hii ni ya pili kwa utamu ikifuatia Kiswenya cha miya. 

Kina ladha tamu ya chachu ambayo haipatikani kwa vile viswenya vingine ambavyo ni baridi. 

Mboga hii kwa hivyo inaweza kupikwa mboga bila kitsanganyo na kula kwa ugali. 

Pia inaweza kuchanganywa na mabwe, mwangani, muzungi,tsafe na hata kiswenya kibomu. 

inaweza kupikwa pekee isipokuwa ina uchachu wa mbali. 

Upishi wake ni kama robo saa na ni mboga nyororo. 

MATUMIZI 

Ni mboga ambayo huliwa na wanyama. Kuku nao hudonadona majani yake. 

Ni rahisi kuikuza mboga hii iwapo kutakuwa na maji maji ya kutosha pale ambapo itaoteshwa.Kiswenya kithithe kinaweza kupandwa kwa kumwagamwaga punga zake bila mpangilio maalumu wakati punga hizi zitamea endapo 

uzao wake umekomaa na kukauka. 

Mboga hii unapo ila kila baada ya siku mbili huongeza damu mwilini na pia nguvu. 

Aina hii ya kiswenya haijawahi kupelekwa sokoni kuuzwa. 

Mboga hii haina madhara wala masharti yoyote.

0 comments:

Post a Comment