Saturday 3 May 2014

ATHARI ZA SIGARA KATIKA UGONJWA WA KISUKARI



Leo nazungumzia jinsi sigara, pombe,
vyakula na mfumo wa maisha wa mtu vinavyoweza kusababisha kisukari na kuleta madhara zaidi kwa mgonjwa wa kisukari,

Kuvuta sigara kuna madhara kwa kila mtu lakini kwa watu wenye kisukari au wanaokabiliwa na hatari ya ugonjwa huo, uvutaji sigara huwaletea madhara makubwa kiafya.

Wataalamu wanatueleza kuwa, wagonjwa wa kisukari ambao wanavuta sigara kiasi cha glucose kwenye damu zao huwa juu, hali ambayo husababisha ugonjwa huo usiweze 

kudhibitiwa kwa urahisi na kuwafanya wagonjwa wakabiliwe na hatari ya kupata madhara makubwa kama vile upofu, 
uharibifu wa neva, figo na matatizo ya moyo. Utafiti mpya 

uliofanywa katika chuo kikuu cha Polytechnics cha huko California nchini Marekani umeonyesha kuwa, nicotine 
mada inayopatikana kwenye sigara inapoingia kwenye damu 

ya mwanadamu, huongeza kiwango cha hemoglobin aina ya A1c kwa asilimia 34%. 

Mabadiliko hayo husababisha hali ya wagonjwa wa kisukari kuwa mbaya na kwa wale ambao hawana ugonjwa huo huwa katika hatari ya kupata kisukari.

Jumuiya ya Kisukari ya Marekani imeeleza kuwa, imeonekana kuwa akina mama wajawazito wenye kisukari ambao wanavuta sigara, wanakabiliwa na hatari ya kujifungua watoto kabla ya muda kutimia na watoto wao kufariki dunia.


Pia wagonjwa wa kisukari wenye kuvuta sigara hupata madhara makubwa na madogo, haraka zaidi kuliko wasiovuta sigara. Kwa bahati mbaya watu wengi hudhani 

kuwa kwa kuwa wanaugua kisukari ugonjwa huo utawasababishia kifo tu hata kama watavuta au kutovuta sigara, fikra ambayo si sawa.

Hii ni kwa sababu wagonjwa wa kisukari wanaovuta sigara, hata dawa za ugonjwa huo huwa haziwasaidii ipasavyo, na hivyo wanapaswa kutambua kuwa uvutaji sigara una mdhara makubwa kwa afya zao.

Chunguzi kadhaa zimeonyesha madhara ya pombe katika kudhibiti glucose kwa wagonjwa wenye kisukari na madhara hayo hutofautiana kwa kuzingatia pombe imenywewa wakati gani na mgonjwa.

Inapasa kufahamu kuwa, pombe inapoingia mwilini huvunjwa vunjwa kama mafuta, na matokeo yake ni kupatikana kalori nyingi. Kwa ajili hiyo unywaji pombe kwa wagonjwa wenye kisukari huweza kuongeza kiwango cha glucose katika damu.
Ijapokuwa kiwango cha wastani cha pombe kinaweza kuongeza kiwango cha sukari kwenye damu, pombe inaponywewa kwa wingi hupunguza sukari kwenye damu na hata baadhi ya wakati kupungua hadi kufikia kiwango cha hatari.

Baadhi ya pombe zenye ladha tamu huongeza carbohydrates mwilini na kuongeza kiwango cha sukari kwa wingi kwenye damu. Pombe pia kumuongeze mtu hamu ya kula, na kula chakula kingi huathiri kiwango cha sukari mwilini.

Baadhi ya wakati pombe huweza kuingiliana na utendaji wa dawa za kisukari hasa dawa za tembe au hata insulin. Pombe huweza kuongeza shinikizo la damu na madhara mengineyo mengi, hivyo wagonjwa wa kiuskari wanapaswa kutambua kuwa pombe si salama kwa afya zao.

Kuhusiana na muundo wa maisha unavyoathiri kisukari, wataalamu wanatuambua kuwa miongoni mwa mambo yanayosababisha mtu kupata ugonjwa huo ni unene wa 

kupindukia, kutoushughulisha mwili, chakula, mfadhaiko wa mawazo au stress na maisha ya mijini. Mafuta ya ziada mwilini husababisha wanaume wapate kisukari kwa asilimia 64 na wanawake kwa asilimia 77.

Kula vyakula na vinywaji vyenye sukari na mafuta huchangia kwa kiasi kikubwa kupatikana ugonjwa huo. Kwa kiwango hicho hicho wagonjwa wa kisukari hasa wenye 
kisukari aina ya pili, huweza kuathiriwa kwa kiasi kikubwa na muundo wa maisha wanaoishi pamoja na vyakula.
Kuushughulisha mwili na kufanya mazoezi pamoja na 
kutokula vyakula vyenye sukari na mafuta huweza hata kupunguza mahitajiao ya insulin kwa wagonjwa wa kisukari, na kuweza kudhibiti kabisa ugonjwa huo.

Naam ndugu wasomaji, natumai kuwa tumefaidika vya kutosha. Tukumbuke kuwa, afya ni kama mmea, na tusipoitunza vyema basi haitomea vizuri.

0 comments:

Post a Comment