Sunday, 4 May 2014

CHANJO KWA SAFARI NITAJUAJE NI CHANJO GANI NICHANJE KABLA SIJASAFIRI KAMA NAKWENDA NJE YA NCHI?


Kwa nyakati hizi ambapo milipuko ya magonjwa na sharia za uzuiaje wa magonjwa umefanya watu waweze kupatiwa kinga ya 
 
chanjo kabla hawajaenda Nchi Husika kulinga na uwezekano wa kuambukiza ama kuambikiza magonjwa huko waendako.

 Tembelea kliniki ya safari, au kama ni kliniki
yako ya kawaida, na wao wanaweza
 
kukusaidia kuamua ni chanjo zipi
zinatakiwa katika safari yako. Ni vizuri zaidi
kama wewe utakwenda mapema kama
 
mwezi mmoja kabla ya safari lakini kama
unahitaji kwenda karibu zaidi na safari
bado ni vizuri kuliko kutokwenda. Kuna
mtandao wa mawasiliano kutumia anwani

ya (http://www.cdc.gov/) ambayo inaweza
kukupa wazo la chanjo na dawa
utakazohitaji. Hakikisha kuwa unaleta kadi
ya historia ya chanjo zako.


Daktari/Muuguzi/mtoa chanjo anawezaje kuamua na
 
kunichagulia nipewe  chanjo zipi?
 
Kuna faida, za kubuni/kujaribisha na
gharama za chanjo zote. Daktari au muuguzi
wako atakuchagulia chanjo yenye faida
 
(jinsi itakavyokupa kinga ili usiugue) kuzidi
zile za kubuni au kujaribisha na gharama za
chanjo hizo. Ni lazima uwaulize daktari na
muuguzi wako maswali juu ya kila chanjo.

Ni chanjo zipi daktari/muuuzi anaweza
kuamua kuzizungumza na mimi?
 
Kuna makundi mawili ya chanjo. Chanjo
ambazo ni za kawaida na kuzoeleka,
ambazo ni lazima uwe umepata hata kama
unasafiri au la, na zile ambazo unazihitaji
kupata wakati ukisafiri.
 
Chanjo za Kawaida au mara kwa mara
Kuna chanjo kadhaa ambazo zinajulikana
kama za kawaida na ambazo daktari au
 
muuguzi wako anaweza kukushauri
uzipate. Nyingi zake ulizipata ukiwa mtoto
mdogo.

Ni lazima upate chanjo ya Tetanus and
Diphtheria (Td) (Kifuaduro na
Pepopunda) kila baada ya miaka 5-10.
 
Ni lazima upate angalau chanjo 2 za
surua katika wakati fulani maishani
mwako.

Kama utasafiri kwenda mahali penye
ugonjwa wa kupooza viungo  polio ni
lazima upate chanjo ya nyongeza angalau
mara moja kama mtu mzima.
 
Kama una miaka zaidi ya 65 ni lazima
upate chanjo ya kichomi (pneumonia)
(pneumococcal).
 
Kama hujapata ugonjwa wa
tetekuwanga au chanjo yake, ni lazima
umwambie daktari au muuguzi wako.

Chanjo za Safari
Hepatitis A
 
Homa ya manjano imeenea sana na watu
huambukizwa kupitia chakula na maji.
Kama umezaliwa katika sehemu ya nchi
 
nyingine inawezekana uliwahi kuupata
ugonjwa huu ukiwa mtoto. Ukiwa mtoto
ugonjwa huu si mkubwa sana. Lakini
 
ukiupata ugonjwa huu ukiwa mtu mzima
utaugua sana na unaweza kufa. Unaweza
kutoa damu yako ili uchunguzwe kuona
 
kama ulishwahi kuupata ugonjwa huu
(mwulize daktari/muuguzi wako kwa
maelezo zaidi).

Kama ulishaugua ugonjwa huu ukiwa
mtoto, huwezi kuupata tena.  Kama hujui  na
hujafanya uchunguzi wa damu, ni lazima
 
upate chanjo kabla ya kusafiri. Unahitaji
chanjo moja kabla hujasafiri na hiyo
itakupa kinga wakati wa safari yako. Ni
 
lazima upate chanjo ya pili ndani ya miezi
6-12 baada ya chanjo ya kwanza na ndipo
utakuwa na kinga kwa maisha yako yote.

Homa ya Matumbo   -   Typhoid
 
Homa ya matumbo ni ugonjwa ambao kwa
kawaida huja kutokea katika chakula au
maji ambako kuna vimelea vibaya. Ugonjwa
 
huu huleta homa kali na maumivu sehemu
za tumbo na huweza kuwa ugonjwa
mkubwa sana na huleta kifo. Kama una
 
marafiki na ndugu una uwezekano
mkubwa wa kusafiri na kisha kuupata
ugonjwa huu. Kuna dawa ya kumeza na
 
sindano badala ya chanjo. Inachukua
angalau siku 7 kumeza dawa hizi na
unahitaji kuzimaliza kabla ya kuanza safari.
 
Dawa ya kumeza ina masharti magumu
kufuata.  Dawa hii ya kumeza hutoa kinga ya
miaka 5 kabla ya ewe kuhitaji kuitumia
 
tena. Ile ya sindano unapiga sindano moja
tu. Hii inakupa kinga ya miaka 2 kabla
hujahitajika kupiga tena nyingine.

Homa ya Uti wa mgongo  -  Menengitis

 
Homa ya uti wa mgongo ni maambukizo
yanayotokea kuzunguka ubongo. Watu
wengi huwa wamebeba vimelea vya aina
 
moja ambayo huweza kuupata ugonjwa
huu ndani ya mdomo na hauwafanyi kuwa
 
wagonjwa. Lakini, wakati mtu mwingine
anaupata kupitia kwenye njia ya kupitia
hewa tuvutayo, huenea (kama kikohozi) the
wahusika huwa wagonjwa taabani na kufa.
Kuna chanjo ya aina hii ya homa ya uti wa
mgongo.

Aina hii ya homa ya uti wa mgongo hususani
hujulikana sana sehemu fulani fulani za Africa
na kama unasafiri kwenda nchi hizi daktari/
 
muuguzi wako atakufahamisha juu ya
chanjo hii. Pia, kama wewe ni Muislamu na
huwa unaenda Kuhiji (k.m. Hijja) unaweza
 
kutakiwa kupata chanjo hii kwa sababu
ugonjwa huu unajulikana sana katika
mazingira haya. Katika sehemu nyingine
 
unaweza kuonyesha kama unakaa (unaishi)
na marafiki au ndugu, hususan kama
utakuwa pale kwa muda mrefu. Kuna
 
chanjo tofauti tofauti, umwulize daktari au
muuguzi wako muda halisi unaohitajika
kabla ya kupata  chanjo nyingine.

Mafua Makali  -  Flu
Mafua huleta homa, kikohozi, kuumwa na
kichwa na misuli kuuma wakati mwingine
huwa ugonjwa mkubwa. Katika nchi za
 
 
baridi hutokea wakati wa baridi (winter),
lakini katika nchi za tropiki au joto, mafua
hutokea mwaka mzima. Ni ugonjwa wa
 
kawaida sana kwa wasafiri. Kupata kinga
mtu anahitaji chanjo.  Chanjo hii ina kinga ya
mwaka mmoja.

Rabies  -  Kichaa cha Mbwa
 
Uganjwa wa kichaa cha mbwa ni ugonjwa
hatari sana ambao kwa kawaida huwapata
wanadamu kupitia kuumwa na mbwa.
 
Wanyama wengine wengi kama vile popo
na nyani, wanaweza pia kuambukiza
ugonjwa huu. Watu wote wanaoupata
 
ugonjwa huu wanakufa kutokana nao.
Kuna chanjo ya ugonjwa wa kichaa cha
 
mbwa kuuzuia endapo mtu ataumwa na
mbwa. Chanjo hii ni ghali na mtu anahitaji
angalau majuma matatu (chanjo 3 mbali
mbali) kukamilisha  chanjo hii.

Kama utasafiri kwa muda mrefu ni lazima
ufikirie kupata chanjo hizi. Watoto ni rahisi
kuumwa na mbwa na wao pia wanaweza
 
kupata chanjo hii. Endapo wewe utapata
chanjo hii kabla ya kusafiri au la, ukiumwa
na mnyama, hususan mbwa, ni lazima
 
ufanye haraka kusafisha sana mahali
ulipongatwa ukitumia maji na sabuni kwa
muda wa dakika kama tano hivi. Ni lazima
umwone daktari upesi iwezekanavyo baada
ya kungatwa.

Homa ya Manjano  -  Yellow Fever
Homa ya manjano hutokea sehemu za Africa
na Amerika ya Kusini. Ni ugonjwa hatari
 
sana na huleta kifo. Chanjo yake mara kwa
mara huhitajika safarini au huhitajika
endapo mtu anavuka toka nchi moja
 
kwenda nyingine. Mtu akipata chanjo hii,
atapewa kitabu cha njano ambacho
atakuwa anasafiri nacho ili kutoa ushahidi
 
wa chanjo yake. Watu hupata ugonjwa huu
kupitia kuumwa na mbu kwa hiyo
wajihadhari kuumwa na mbu.
Chanjo hii humpa mtu kinga
ya miaka 10 kabla hajalazimika kupata
chanjo nyingine.

 
Japanese Encephalitis
 
Ugonjwa huu umetokea Kusini-mashariki
mwa bara la Asia na Kusini mwa bara la
Asia. Watu hupata ugonjwa huu kutoka
kwa mbu, hususan sehemu za
 
mashambani ambapo kuna nguruwe. Kama
unatembelea sehemu zilizo nje ya miji mikuu
kwa zaidi ya mwezi mmoja, daktari/
muuguzi wako atakushauri chanjo hii.
 
Unahitaji angalau siku tatu tofauti za
sindano ambazo ni lazima ziwe zimetolewa
majuma machache kabla ya kusafiri ili
kuweza kuwa na kinga.

0 comments:

Post a Comment