Wednesday, 30 April 2014

MARADHI YA KUTOPATA CHOO KIURAHISI (CONSTIPATION):




UKOSEFU wa choo ni tatizo sugu miongoni mwa watu wengi. Bila kujua kuwa ni tatizo ambalo linahitaji tiba ya haraka, watu wengi hupuuzia na kuona siyo tatizo kubwa na ni hali ya kawaida. Ukosefu wa choo wa muda mrefu, huwa ndiyo chanzo cha magonjwa mengine hatari.

Mtu anapokosa choo kikubwa kwa siku kadhaa, uchafu hujikusanya tumboni na unapokosa sehemu ya kutokea hukimbilia kwenye damu na kuingia kwenye mfumo mzima wa damu. Uchafu huo unapoingia kwenye mfumo wa damu huwa sumu na chanzo cha maradhi mengine ambayo hujitokeza baadae na kuanza kumuathiri mtu, bila kujua chanzo chake.

Kwa kawaida mtu unapaswa kupata choo cha uhakika japo mara moja kwa siku, kutegemeana na mlo wake wa kila siku, unapokosa choo kwa siku nzima ili hali una kula milo yote kwa siku, elewa una tatizo katika mfumo wako wa kusaga chakula hivyo unapaswa kuchukua hatua haraka.

MTU MWENYE TATIZO HILI ANA DALILI GANI?
Mtu mwenye tatizo la ukosefu wa choo huwa na dalili kadhaa, ikiwemo kutumia nguvu na muda mwingi wakati wa kujisadia haja kubwa. Pili ulimi wake huwa na utandu mweupe na hutoa harufu mbaya mdomoni. Mtu huyu pia hukosa hamu ya chakula na wakati wote tumbo huwa limejaa.

NINI HUSABABISHA TATIZO?

Tatizo la ukosefu wa choo husababishwa zaidi na ulaji mbaya wa vyakula, kuacha kula matunda na mboga na staili mbaya ya maisha ikiwa ni pamoja na kutokunywa maji ya kutosha kwa siku.

NINI KIFANYIKE?
Ili kuondoa tatizo kabla halijawa sugu, fanya moja miongoni mwa haya yafuatayo: Kunywa maji ya uvuguvugu asubuhi mapema, kisha tembea tembea, baada ya muda utasikia haja ya kwenda chooni. Ili usifanye haraka na upate muda wa kutosha kujiandaa kwenda kazini, amka mapema zaidi. Kula kiasi cha kutosha cha salad ya mboga mboga na juisi ya matunda halisi asubuhi kabla ya kula chochote.

Kila siku kabla ya kwenda kulala, kunywa maji ya uvugu yaliyochanganywa na kijiko kimoja cha asali. Kunywa maji ya uvugu

yaliyochanganywa na limau asubuhi na mapema kabla hujala kitu chochote. Kunywa ‘castor Oil’ muda mfupi kabla ya kwenda kulala. Ili

kujiepusha kabisa na tatizo la ukosefu wa choo, jenga mazoea ya kunywa maji mengi, kula mboga na matunda kwa wingi kila siku na

kuacha kabisa ulaji wa vyakula vilivyoondolewa virutubisho kama vile mikate myeupe, ugali wa unga mweupe, keki vyakula vyenye sukari nyingi na vyakula vingine vitamu.

 MARADHI YA KUTOPATA CHOO (CONSTIPATION): 
 Haya ni maradhi ambayo mgonjwa huwa hapati choo kwa wepesi. Haja kubwa inaweza kutoka baada ya siku moja au mbili au zaidi na ikitoka huwa ni kigumu na hutoka kwa shida na wakati mwingine huwa kama

cha mbuzi. Wagonjwa wengine hupata maumivu wakati wa kwenda haja kubwa.
Mtu mwenye afya nzuri hupata haja kubwa kwa kiwango cha chini mara moja kwa siku. Na choo huwa laini na hutoka bila matatizo.

SABABU ZA MARADHI HUSIKA:
(1) Upungufu wa vitamini mwilini hasa vitamin B. 
(2) Maradhi ndani ya utumbo mpana. 
(3) Kula vitu vigumu na vikavu kama vile vyakula vya ngano. 
(4) Upungufu wa ulaji matunda na mboga. 
(5) Kutokunywa maji ya kutosha. 
(6) Upungufu wa fibre kwenye chakula zinazopatikana kwenye maganda ya mahindi. 
(7) Ukosefu wa kufanya mazoezi ya viungo.

TIBA: Kanuni ya kwanza:

Chukua glasi moja ya maziwa freshi baridi uchanganye na vijiko viwili vikubwa vya asali na kijiko kimoja kidogo cha mafuta ya habitsoda. Kunywa glasi moja kutwa mara mbili asubuhi na jioni. Dawa hii hufanya choo kuwa laini na kupata haja kubwa kwa wepesi.

Kanuni ya pili: 
Unga wa sanamaki kijiko kimoja kikubwa, Unga wa tangawizi kijiko kimoja kikubwa, Unga wa habasoda kijiko kimoja kikubwa, na Asali robo lita. Dawa hizi zote zichanganye pamoja kwa kukoroga kwa kijiko. Kula kijiko kimoja kutwa mara tatu.

Kanuni ya tatu: 
Asali robo lita, na Unga wa Arki susi vijiko vinne vikubwa. Kula vijiko viwili vikubwa kutwa mara mbili.

Kanuni ya nne: 
Kunywa kwa wingi maji ya kunywa ya kutosha na pia ule kwa wingi matunda na mboga.


Kanuni ya tano: 
Kula kila siku asubuhi tende saba kabla ya chakula cha asubuhi. Tende hufanya choo kuwa laini.

1 comments:

  1. Pia ata unywaji wa maziwa uliopindukia upelekea tatizo hilo

    ReplyDelete