Wednesday 30 April 2014

FAIDA ZA KIAFYA ZIPATIKANAZO KWA KULA TUNDA LA PARACHICHI (AVOCADO)

Parachichi


Tunda  la  AVOCADO  ama  PARACHICHI  lina  faida  nyingi  kwa  afya  ya  mwanadamu.


Miongoni  mwa  faida  hizo  ni  pamoja  na  :
i.             Avocado  lina vitamini A,B na C   ambazo  zina  faida  lukuki  kwa   mwili wa  mwanadamu
ii.           Husaidia  kuimarisha guvu ya mwili na ubongo
iii.         Husaidia  kujenga neva na fahamu
iv.         Husaidia  kujenga mifupa na kuipa nguvu
v.           Husaidia  kuleta kuona vizuri
vi.         Husaidia  kupiga  vita ukosefu wa damu (anaemia)
vii.       Husaidia  kufanya kazi  ya  kuondoa nywele zinazoanguka.
viii.     Husaidia kukuza nywele zinazodumaa (dandruf)
ix.         Husaidia kutuliza maumivu pindi inapopakwa au kusuguliwa sehemu yenye maumivu
x.           Majani ya  avocado   yakichemshwa kama chai na kunywewa husaidia kuondoa matatizo mbalimbali  ya mwili  kama  vile  uchovu,udhaifu,kujisikia ovyo,kuumwa kichwa, kuumwa Koo (throat),tumbo Mapafu,uvimbe, vidonda mdomoni (kwa kutafuna majani)

Mbegu  ya  Parachichi.

·       Mbegu  ya  parachichi  iliyo  kaangwa  na  kusagwa  husaidia  kutibu   tatizo  la Kukwama kwa mkojo
JINSI  YA  KUTUMIA  PARACHICHI  KAMA  DAWA  YA  KUTIBU  TATIZO  LA  KUKWAMA  KWA  MKOJO.
Koroga vijiko 2 vya chai vya  unga wa  mbegu  ya  parachichi  katika maji ya moto kikombe kimoja.
MATUMIZI
Tumia  kunywa  kikombe  kimoja  mara  mbili  kwa  siku  asubuhi  na  jioni  hadi  pale  tatizo  lako  litakapo  malizika.
xi.         Tunda  la  parachichi  husaidia  kutoa uric acidmwilini  inayo  sababishwa  na  ulaji  wa  nyama  nyekundu.

0 comments:

Post a Comment