Tuesday, 29 April 2014

FAIDA ZA KIAFYA ZIPATIKANAZO KWA KUTUMIA MBOGA YA MCHICHA.


MCHICHA ni  mboga  maarufu miongoni  mwa  watanzania. Mbali  na  kutumiwa  kama  mboga, mchicha  ni  tiba  ya  matatizo  mbalimbali  ya  kiafya.


Kwa  mujibu  wa  tafiti  mbalimbali  za  kitaalamu, mchicha  huweza  kutibu   matatizo  yafuatayo :
i.             Kuumwa mgongo
ii.           Kusafisha njia ya mkojo
iii.         Kusafisha damu
iv.         Unatibu Magonjwa  ya  Figo
v.           Unatibu minyoo
vi.         Unatibu Baridi yabisi
vii.       Tezi la shingo
viii.     Homa
ix.         Kuongeza damu
x.           Unasaidia kupata haja ndogo kwa wingi
xi.         Unarutubisha  uwezo  wa  kuona  vizuri.


JINSI  YA  KUTUMIA  MCHICHA  KAMA  DAWA
MATAYARISHO
Chukua mchicha kilo 1  ya  mchicha, chemsha maji lita 2 na nusu. Yakichemka loweka mchicha kwa dakika 15. Tumia kikombe. Ni bora utumie yote kwa siku . Dozi ni siku 5


KAMA  UNATAKA  KUTIBU MGONGO: Chukua mchicha ponda. Chua mara 3 kwa siku. Usiku unapasha moto mchicha kisha unufunga mahali panapouma. Lala nao wakati vuguvugu la joto lake lenye maji ndani (dawa) ikiingia ndani fanyahivyo kwa siku 5, ukibadilisha kila siku (fresh)

KUTUMIA  MCHICHA  KAMA  TIBA  YA TEZI LA SHINGO Chukua mchicha kiasi kidogo, ponda, fungia shingoni pale penye uvimbe wakati unapolala kwa kitambaa, kwa muda wa siku 5.

0 comments:

Post a Comment