Tuesday, 29 April 2014

DAWA YA KUONDOWA CHUNUSI USONI





Unafahamu chunusi hutibika kwa Limau?

Limau lina tindikali aina ya citric ambayo inasaidia kuponya chunusi na vilevile

tunda hilo lina Vitamin C, ambayo ni muhimu kwa kuifanya ngozi iwe na afya

wakati alkali inayopatikana kwenye limau nayo husaidia kuua vijidudu

vinavyosababisha chunusi.Kunywa juisi ya limau kama chakula cha kwanza asubuhi kunaaminika kusadia kuboresha ngozi.Jinsi ya kutengeneza nyumbani mchanganyiko wa limau kwa ajili ya kutibu chunusi:

• Kwa kutumia pamba paka maji ya limau katika sehemu yenye chunusi na wacha kwa usiku kucha.
• Safisha kwa maji safi asubuhi inayofuata.
• Ingawa unaweza ukahisi kuwashwa wakati unapopatumia mchanganyiko huo juu ya ngozi mara ya kwanza, lakini

Baadaye hali hiyo huzoeleka. Au

1. Changanya maji ya limau ulioyakamu kutoka katika kipande kimoja cha limao na changanya na maji ya waridi (rose water) au asali nyepesi kwa kiwango hicho hicho.
2. Paka mchanganyiko huo kwenye sehemu za ngozi zenye chunusi na subiri kwa muda usiopungua nusu saa mpaka saa lizima.
3. Baadye osha kwa maji.

Mchanganyiko huu unapaswa kupakwa mara mbili kwa siku, bora utumiea asubuhi na jioni.

Muhimu:
Kutumia mchanganyiko huu hakuna madhara na ni wa asilia, lakini iwapo chunusi zinazidi au kuna vidonda vinavyoambatana na chunusi ni bora upate ushauri wa daktari kwanza

Related Posts:

  • UGONJWA WA GENITAL WARTS KWA WANAWAKE Ugonjwa wa Genital Warts ni hali ya kuota vinyama kwenye ngozi au utando laini unaozunguka maeneo ya siri, ni ugonjwa unaoenezwa kwa njia ya kujamiiana (sexually transmitted infection kifupi STI).Ugonjwa huu unaweza kuto… Read More
  • UGONJWA WA SARATANI YA NGOZI (MELANOMA) LEO tutachambua kwa undani saratani ya ngozi iitwayo Melanoma kwani saratani si tu kwamba ni ugonjwa hatari lakini pia ni ugonjwa unaompa mwanadamu mateso makali kutokana na maumivu anayoyapata. Maumivu hayo huyapata… Read More
  • KUTOKWA NA MAJIMAJI KWENYE MATITI (GALACTORRHEA) Tatizo hili husimama lenyewe kama ugonjwa ingawa pia inaweza kuwa ni dalili kama mwanamke ni mjamzito, ananyonyesha au ametoa mimba au ameharibikiwa na mimba.Kusimama kwake kama ugonjwa ni pale  yanapotoka wakati mwa… Read More
  • UJUWE UGONJWA UITWAO MKANDA WA JESHI (HERPES ZOSTER/SHINGLES). Kwa takribani miongo mitatu sasa, tumeshuhudia ongezeko kubwa la mlipuko wa ugonjwa wa mkanda wa jeshi linaloendana na ongezeko la hususani ugonjwa wa UKIMWI. Hali hii imefanya baadhi ya watu kuamini kuwa, ugonjwa huu… Read More
  • UGONJWA WA SARATANI YA NGOZI (MELANOMA)-2 WIKI iliyopita tulieleza jinsi ugonjwa huu unavyomuingia mtu na matatizo yake. Tulieleza dalili lakini nyingine ni tezi za mwili za kwenye makwapa na kwenye nyonga huvimba, mgonjwa atatokwa na uvimbe kwenye ngo… Read More

0 comments:

Post a Comment