Hakikisha
unaoga kila siku ili kupunguza idadi ya
bakteria kwapani kwani husababisha kuweka harufu mbaya kwenye mwili hasa
majira ya joto kwa kuwa mara nyingi joto ndilo husababisha jasho na
harufu kwapani hivyo unahitaji kuoga mara mbili kila siku, unaweza
kutumia sabuni au anti-bacterial na maji ya moto.
Safisha nguo
katika maji ya moto na sabuni ya kuondoa uchafu na
mafuta, vaa mashati safi. Inapendekeza kuvaa mavazi yenye nyuzi za
asili, kama vile pamba na hariri ili kusaidia kunyonya unyevunyevu na
kuruhusu ngozi kupumua.
Wakati unafanya mazoezi, tumia nguo zenye vitambaa ambavyo vitanyonya unyevunyevu kwapani ili kuzuia harufu mbaya.
Vinega ‘siki’ na mafuta ya chai ‘ tea tree oil’
Apple cider siki na vinega nyeupe, hupunguza harufu kwapani. Ili kukabiliana na harufu, loweka pamba katika vinega, paka kwenye makwapa badala ya deodorant. Mbali na tiba hiyo, tumia tea tree oil, inaweza pia kuwa na manufaa kwa sababu ni anti-bacterial.

Limao
Kata limao au ndimu nusu kwa kisu. Paka kipande cha limao ulichokata kwenye kwapa lako na hakikisha unalisugua mpaka litoe maji yake. Weka kwapa lako lipate hewa ili hiyo juice ya limao uliyopaka ikauke.
Asidi citric katika maji ya limao inasaidia kutoa tezi ya jasho hivyo kuondoa harufu.
Makala hii ni kwa msaada wa Bongo urembo, wiki ijayo nitajibu maswali yenu yote, asanteni kwa kunisoma.

Asante sana
ReplyDeleteKaribu sana kaka yangu ndugu Rashid Mpilingi
ReplyDeleteThanks sana mtaalam
ReplyDelete