FAIDA ZA KIAFYA ZA KULA NYANYA....
Hili ni tunda mashuhuri na lenye virutubisho ambalo kwa kawaida hutumika kama mbogamboga. Kwa wastani, watu hula takribani kilo 8 za nyanya kwa mwaka.
Nyanya zina aina mbalimbali za viasili vya kurutubisha na visivyorutubisha vinavyohusiana na faida kadha wa
kadha za kiafya. Hii inajumuisha lycopene, vitamini C,
A na K, potasiamu, na nyuzinyuzi.
Nyanya moja yenye ukubwa wa wastani inaweza
kutoa takribani nusu ya kiasi cha kila siku cha vitamini
C anachohitajika kupata mtu. Viasili mbalimbali vya
nyanya vinasadikika kufanya kazi pamoja kuleta
manufaa ya kiafya.
Hii ni pamoja na kusaidia kujenga afya ya meno, afya
ya mifupa, afya ya ngozi, afya ya nywele, kupunguza
shinikizo la damu (PB) na kupunguza viwango vya
lehemu pamoja na kupunguza hatari ya ugonjwa wa
moyo na saratani.
Baadhi ya vionjo vya nyanya kama vile lycopene
hufyonzwa kwa wepesi mwilini pale nyanya
zinapochemshwa, iwe kwa kuzipika au kuzichemsha.
Sasa huenda tunazijua faida za kula lishe kamili ya
kuleta afya ikiwa ni pamoja na kula matunda na
mbogamboga. Lakini wasichokijua watu wengi ni
kwamba juisi ya mbogamboga ndiyo inayosaidia
kudumisha urari (pH) muhimu wa haidrojeni ya mwili.
pH ina maana ya nguvu ya haidrojeni katika mizani ya
kupimia hali-asidi ya vitu mwilini. Ili mwili ufanye kazi
vizuri na kuweza kuendelea kuishi, lazima uwe na
vikemikali vinavyolipuka na vitu vya asidi ili
kutengeneza chumvi na kutoa umajimaji wenye nguvu
ya haidrojeni (ya baina ya 7 na 7.5) na uwe na kipimo
cha haidrojeni chenye urari kamili kwa sababu saba:
1. Kuulinda mwili dhidi ya uharibifu utokanao na
chembechembe za maradhi na kuukinga na uzee wa
kabla ya wakati.
2. Kuusaidia mwili kudumisha viwango vya lehemu
vyenye kuleta afya bora.
3. Kuweka msukumo wa damu katika kiwango bora cha afya.
4. Kuweka katika hali ya kawaida kikemikali cha
kusawazisha sukari ya damu (insulin) na kuzuia
ongezeko la uzito wa mwili linaloweza kuhatarisha afya.
5. Kuuwezesha moyo kufanya kazi vizuri.
6. Kuongeza uzalishaji wa nishati
7. Kudumisha mfumo wa kinga ya mwili, mfumo wa
umeng’enyaji, kudumisha afya ya viungo vya mwili na mifupa
0 comments:
Post a Comment