Faida ya kutafuna mbegu za tikiti maji
TIKITI MAJI ni moja ya matunda yanayolimwa sana
katika maeneo mbalimbali nchini Tanzania tofauti na miaka iliyopita.
Hii inaashiria kwamba tunda la tikiti maji linaliwa
sana katika maeneo hayo kutokana na faida
inayopatikana kwenye tunda hilo.
Pamoja na kuongezeka kuliwa kwa tunda la tikiti maji
lakini wengi wa wateja wanaokula tunda hilo huwa
hawajui faida ya mbegu za tunda hilo.
Kutokana hali hiyo wengi wanaokula tikiti maji
wanatema mbegu hizo na huenda wengi walikuwa na
imani potofu inayokataza kula mbegu za tunda.
Hivyo badala ya kuzitafuna mbegu hizo wengi
huzitema na kuona ni kitu kisicho na faida yoyote
katika mwili wa binadamu.
Lakini mbegu hizo zinatakiwa kutafunwa wakati
unapokula tunda lenyewe na hii ni kutokana na faida zake kiafya.
Unapokula tunda la tikiti maji unachotakiwa kufanya ni
kuzitoa mbegu zake na kuziweka kwenye chombo
kimoja mpaka zichipue yaani kuanza kutoa mizizi.
Baada ya hapo unatakiwa uzikaushe tayari kwa
kuzitumia kutoka na faida hizi zifuatazo:
Mbegu za tikiti maji zina protini nyingi hivyo kuzitafuna
kunaweza kumpatia mlaji chanzo cha protini.
Pia aunzi mmoja tu (takriban ujazo wa 1/8 wa
kikombe) inakupa virubutisho vya protini vya gramu 10.
Hii ni sawa sawa na kiwango kinachopatikana kutoka
katika yogati ya Kigiriki wakati wa kustaftahi.
Mbegu ‘zilizochipua’ zimemea na mara nyingi zina
virutubisho vya hali ya juu kuliko zile ambazo hazichipua.
Kuchipua kunaondoa mchanganyiko katika chakula
ambacho husababisha ugumu wa kufyonza
virutubisho vyote.
Mbegu za tikiti maji zilizochipua zikitafunwa huongeza
msongamano wa virutubisho na kusababisha urahisi
kumeng’enya chakula.
Kuhusu tikitimaji, mbegu hutolewa ngozi nyeusi ya juu
na kubaki ikifanana na mbegu zilivyo.
Katika mbegu za zamani hili halipatikana lakini
umegundulika kwamba kweli mbegu hizi zinaleta afya kwenye mlo.
Mbegu za tikiti maji zilizochepua zina protini, vitamin B,
Magnesia, na mafuta ambayo hayakoleza.
Wataalamu wa masuala ya chakula wanasema
mafuta yaliyokolezwa mara nyingi hayana viwango vya
lehemu na muasho na yanaondoa hatari ya kupata
ugonjwa wa moyo na kiharusi.
Kama umeshawahi kutafuna mbegu za matikiti maji
wakati ukila tunda hilo uligundua ladha yake ni sawa
na tunda lenyewe.
Mbegu za matikiti maji ni sawa na mbegu za alizeti
kwa ladha, lakini haina lozi kubwa.
Zinakuwa na ladha nzuri zaidi zikiwa kwenye
kachumbari, iliyochanganywa pamoja au ukiila ikiwa mkononi mwako.
Jungu na mbegu nyingi ni nzuri kwa mwili wa
mwanadamu, lakini ukilinganisha ukubwa wa lishe
unaopatikana basi mbegu za matikiti maji zinaongoza.
0 comments:
Post a Comment