Tuesday, 9 December 2014

KWA NINI WANAUME HUTOWA MAMILIONI YA MANII KATIKA TENDO LA NDOA WAKATI MBEGU INAYOHITAJIKA NI MBEGU MOJA TU?




Kwa wastani, mwanamme hutoa kiasi cha mbegu bilioni 525 katika maisha yake, na kwa kila mwezi hutoa mbegu hizo zisizopungua bilioni moja.

Kwa upande wa wanawake, wao huwa wamezaliwa na mayai milioni mbili ya uzazi, na wafikiapo wakati wa balehe, idadi kubwa ya mayai hayo hujifunga na kuacha mayai 450 tu ambayo huweza kukomaa na kuwa mayai yenye uwezo wa kutunga mimba.

Kulingana na utafiti mpya, tangu zama za kuwepo kwa jinsia za kiume na kike, jinsia ya kiume imekuwa na ushindani katika kutaka kupeleka mbegu zake za uzazi karibu na yai la kike. 

Katika ushindani huo msingi wake ni kwamba kufikisha mbegu za kiume karibu na yai la kike kunatoa uwezekano mkubwa zaidi wa kuungana na yai la kike na kutunga mimba. Hivyo jinsia ya kiume huitafuta fursa hiyo kwa kutia maanani kwamba ni “mimi naweza kufanya hivyo na si jirani yangu”.

Mashindano haya ni mabadiliko ya lazima kwa viumbe wa kiume wa aina zote. 

Iwapo mbegu ya mpinzani wako itafanikiwa kuungana na yai na kutunga mimba, hivyo fursa ya wewe kuendeleza vinasaba vyako kwa viumbe wengine hupotea. Katika vizazi vingi vilivyopita matokeo yamekuwa ni hayohayo:

kwamba nguvu za kuzaliana huenda kwa viumbe vya kiume vinavyotoa mbegu nyingi zaidi za uzazi, na hivyo kuweza kuendeleza vinasaba (genes) vyake.

Hivyo, vinasaba vya viumbe wanaotoa mbegu ndogo za uzazi hatimaye hutoweka katika jumuia ya viumbe husika na kubakia tu katika historia ya mabadiliko.

Kama lingekuwa ni suala la kutoa mbegu nyingi ni vizuri zaidi, basi wanyama wa aina zote wangekuwa na korodani kubwa ajabu katika jitihada za kutaka kushinda mashinano ya utoaji mbegu nyingi.

Hata hivyo, hilo pekee halitoshi, kwani idadi ya mbegu ni jambo muhimu pamoja na ukaribu wake na yai la kike.

Katika kulifanya yai la kike litunge mimba, si jambo tu la kutegemea manii nyingi unayotoa, bali ukaribu wa manii hayo na yai la kike ni jambo muhimu pia.

Jibu hili limetolewa na Scienceline, mradi wa Mpango wa Habari za Science, Afya na Mazingira wa Chuo Kikuu cha New York

0 comments:

Post a Comment