Monday, 3 November 2014

FANYA MAMBO 5 ILI UWEZE KUJIKINGA NA MARADHI.



 1. Jitahidi kadiri uwezavyo kufanya mambo haya matatu: kula vizuri, kufanya mazoezi ya kutosha, na kupumzika vya kutosha.
 
 2. Dumisha usafi. Wataalamu wa afya husema kwamba kunawa mikono ndiyo njia bora ya kujikinga na magonjwa au kuepuka kueneza maambukizo.
 
 3. Hakikisha kwamba chakula mnachokula na familia yako ni salama. Hakikisha mikono yako na mahali unapotayarishia chakula ni safi. Pia, hakikisha kwamba unatumia maji safi kunawa mikono na kusafisha chakula. Kwa kuwa viini huzaana ndani ya chakula, pika nyama kabisa. Hifadhi vyakula vizuri.
 
 4. Katika maeneo ambayo magonjwa hatari huenezwa na wadudu wanaoruka, epuka kuwa nje usiku au mapema asubuhi wakati ambapo wadudu ni wengi. Jikinge kwa chandarua sikuzote.
 
 5. Kupata chanjo kunaweza kuimarisha mfumo wako wa kinga ili upambane na viini vinavyopatikana mahali unapoishi.

Related Posts:

  • MBINU ZA KUJIKINGA NA SARATANI YA MATITI SARATANI ya matiti ni moja kati ya aina za saratani zenye kuathiri wanawake wengi duniani, Tanzania ikiwemo. Kujikinga na ugonjwa huu hatari ni muhimu zaidi kuliko kupima na kujitambua kama tayari umeshakupata, hivyo kat… Read More
  • VYAKULA MUHIMU KWA WAJAWAZITO Kumbuka kwamba vyakula vyote vinaweza kuwa ni muhimu mwilini lakini huzidiana kulingana na mahitaji na hali ya mtu kwa wakati maalumu.Mahitaji ya madini na vitamini mwilini wakati wa ujauzito huwa ni makubwa, husus… Read More
  • AFYA: SUMU HUATHIRI WAUME,WATOTO WA WANAWAKE WANAOTUMIA MIKOROGO “Tunafanya kampeni ya kupambana na vipodozi vyenye sumu kwa sababu tatizo ni kubwa nchini.“Hadi sasa asilimia 52 ya Watanzania hutumia mkorogo. matokeo yake wengi wameathirika na wanashindwa kuacha.” Euphrasia ShayoKWA UF… Read More
  • VYAKULA VYA KUEPUKWA NA WAJA WAZITO Ili mtoto azaliwe akiwa na afya njema pamoja na akili timamu, akiwa tumboni lazima alishwe lishe bora na mlo sahihi. Mwenye jukumu la kutoa lishe bora na sahihi kwa kiumbe kilichomo tumboni ni mama. Anatakiwa kujua aina … Read More
  • VIUNGO VYA MBOGA VINAVYOWEZA KUOKOA MAISHA YAKO AFYA bora ndiyo msingi wa maisha ya kila binadamu, bila kuwa na afya bora hakuna maisha. Kwa sababu maradhi hukaa mbali na mtu mwenye afya bora na maradhi hukaa karibu na mtu mwenye afya mbovu. Lakini je, utawezaje kuwa … Read More

0 comments:

Post a Comment