Saturday, 27 September 2014

KUTAPIKA WAKATI WA UJA UZITO (EMESIS GRAVIDARUM)




Kutapika ni dalili inayojitokeza kwa mama mjamzito hasa kipindi cha awali ingawa tatizo la kutapika au kuhisi kichefuchefu linaweza kutokea katika maradhi mengine mbali mbali tofauti na ujauzito.
Hali ya kutapika kwa mama mjamzito imegawanyika katika makundi mawili.Kwanza ni kichefuchefu na kutapika wakati wa kipindi cha mwanzo cha ujauzito ( Early pregnancy) na pili ni kipindi baada ya hicho cha awali (Late pregnancy).

Morning sickness.
Tatizo hili hujitokeza miezi ya awali ya ujauzito. Mara nyingi haziendelei baada ya wiki ya 12. Mama anakuwa na kichefuchefu na anaweza kutapika hasa wakati wa asubuhi.

Hyperemesis gravidarum
Tatizo hili linaambatana na mama kuishiwa maji mwilini kwa kutema mate,kutapika na kushindwa kula na wakati mwingine hulazwa hospitali,

Kutapika kunakoendelea wakati wa ujauzito (late pregnancy) huwa ni muendelezo wa hali hiyo.Tangu mwanzoni hali ya awali (Early pregnancy) hutokea mimba inapokuwa chini ya miezi minne lakini hii hali ya pili ‘Late pregnancy inatokea mimba inapokuwa zaidi ya miezi minne.Hapa mama huendelea tu kutapika na vilevile inahusiana na dalili za magonjwa mengine kama dalili za awali za kifafa cha mimba.

Yapo magonjwa mengine yanayosababisha kichefuchefu na kutapika ambayo yanaweza kumpata mama mjamzito na asiye mjamzito.

Magonjwa haya ni kama vile minyoo, maambukizi ya njia ya mkojo(Urinary Track infections),magonjwa ya ini(Hepatitis),ugonjwa wa kisukari (pale sukari inapokuwa juu) (Ketoacidosis of Diabetes),mkojo kuingia katika mfumo wa damu(uraemia),ugonjwa wa kidole tumbo (Appendicitis),vidonda vya tumbo (peptic ulcer) kuziba kwa tumbo (Intestnal obstruction) matatizo ya nyonga kifuko cha mayai (Twisted Ovarian cyst) na uvimbe katika kizazi (uterine fibroid).

Inaaminika kutapika kunasababishwa na kuongeza kwa hormoni ya eostrojeni. Baadhi ya akina mama wanaotumia vidonge vya majira hupata dalili kama za mama mjamzito. Pia hormone ya HCG inaweza kusababisha tatizo hili.

Tatizo hili linaweza kutokea katika mimba ya kwanza tu,wengine hutokea ya pili au wengine hutokea mimba zote.

Hali ya kisaikolojia (psychogenic) pia huchangia kuamsha kichefuchefu kwa kutotamani baadhi ya vitu au vyakula au harufu.
Mama akiwa na hali hii hasa vyakula vya wanga hasa nyakati za usiku,asubuhi ataamka na njaa na kichefuchefu na kuanza kutapika na kuchoka

Chakula cha wanga kama wali na ugali ni muhimu kwani vinatia nguvu na joto,vilevile uwepo wa vitamini B za kutosha nao husaidia sana.

Tatizo hili la kichefuchefu na kutapika pia huchangiwa na mzio (Allergies ) mbalimbali na tumbo kutofanya kazi vizuri (Decreased gastric motility).

Ufanye nini
Mara nyingi kichefuchefu cha kawaida hakiitaji tiba yoyote.Hata hivyo kichefuchefu kikali zaidi kinaitaji matibabu ya haraka. Hivyo ni vyema ukiwahi hospitali.

Matibabu
Matibabu hutegemea dalili. Hata hivyo mgonjwa anaweza kuongezea maji na kupewa dawa za kuzuia kichefuchefu pamoja na kutapika.
Pia ni vyema mgonjwa akijitahidi kula hasa vyakula vya jamii ya wanga pale anapopata nafuu. Maji ni muhimu. Tena mara kwa mara. Hii itasaidia kupunguza uwezekano wa upungufu wa maji iwapo hali itajirudia.

0 comments:

Post a Comment