Thursday, 28 August 2014

UVIMBE KATIKA MFUKO WA KIZAZI (UTERINE FIBROID)-2



Wiki iliyopita utakumbuka nilianza kuzungumzia mada hii, leo nitaimalizia ili wiki ijayo nianze nyingine.
Niliishia kusema kwamba, mwanamke mwenye uvimbe anaweza kupata damu ya hedhi bila mpangilio hasa kama uvimbe huo upo ndani ya kizazi.
Utokaji huu wa damu ni kutokana na uvimbe kuharibu mishipa ya damu ndani ya tabaka la kizazi.
Damu inaweza kutoka nyingi mfululizo baada ya siku maalum ya hedhi kwisha au ikaendelea kutoka kidogokidogo baada ya zile siku za hedhi kwisha au ikaanza tena kutoka katikati ya mwezi baada ya kumaliza hedhi.
Mishipa ya damu inaweza kubanwa na uvimbe hivyo kuzuia mzunguko wa damu wa kizazi na kujikuta unapata maumivu makali ya tumbo chini ya kitovu au maumivu makali ya hedhi ambayo awali hukuwa nayo.
Utahisi kiuno kizito na chini ya kitovu kumejaa na kama uvimbe ni mkubwa utaumwa kiuno, maumivu yakasambaa mapajani na miguuni na kubana mishipa ya damu mikubwa ya miguuni na kujikuta miguu yote miwili au mmoja ukivimba, kibofu cha mkojo na mfuko wa haja kubwa vinaweza kubanwa na kusababisha kushindwa kupata haja kubwa vizuri na haja ndogo kwa shida.
Pia mirija ya figo inaweza kubanwa na figo kupata shida, hali hii kitaalam huitwa ‘Pressure effects’.
Mwanamke mwenye uvimbe huu pia hulalamika kupata ujauzito, na hii hasa hutegemea na jinsi ulivyobanwa, kama upo ndani ya kizazi na ni mkubwa, kama umebanwa karibu na mirija ya mayai au katika mlango wa kizazi.
Uchunguzi
Mgonjwa anaweza kuhisi kitu kizito katika kizazi au uvimbe unaweza kuwa mkubwa kama ujauzito kumbe siyo. Vipimo vinavyotumika zaidi ni Ultrasound na vingine inategemea na daktari atakavyoona inafaa.
Vipimo vingine ni vya damu na kudhibiti uambukizo ndani ya kizazi na utokaji damu bila ya mpangilio.

Madhara ya uvimbe
Kwa mama mjamzito anaweza kutokwa sana na damu kwa kizazi kushindwa kubanwa na kuzuia utokaji wa damu, mtoto anaweza kukaa vibaya ndani ya kizazi na uvimbe unaweza kubana njia ya kutokea mtoto. Hali hii inaweza kusababisha mama kuzaa kwa njia ya upasuaji.Kwa mwanamke ambaye hashiki mimba anaweza kushika mimba baada ya  kuondoa uvimbe. Kutokwa na damu mfululizo husababisha upungufu mkubwa wa damu mwilini.
Matibabu na ushauri
Hakuna dawa ya kutibu tatizo hili, tiba ya uvimbe wa aina hii ni upasuaji na kuuondoa, ukiwa mkubwa basi hata kizazi kitatolewa hasa kwa wale ambao hawana mpango wa kuzaa tena.
Mwanamke mwenye mpango wa kuzaa uvimbe utaondolewa kwa umakini mkubwa, bila ya kuumiza mirija ya uzazi. Tiba hupatikana katika hospitali za mikoa.

Dawa ya asili ya kutibu Uvimbe katika mfuko wa kizazi (UTERINE FIBROID) dawa ya asili ipo kwa mtu mwenye kuhitaji nitafute kwa wakati wako nipate kukutibia.

Related Posts:

  • ATHARI ZA MAAMBUKIZI KATIKA VIUNGO VYA UZAZI Maambukizi kitaalamu huitwa ‘Pelvic Inflammatory Diseases’. Maambukizi haya huwa sugu na huchukua muda mrefu mwanamke kupona endapo atakuwa na tatizo hili.Maambukizi hushambulia kizazi na mirija ya mayai na viungo jiran… Read More
  • MAUMIVU YA TUMBO YA MARA KWA MARA KWA WANAWAKE Wanawake wanaosumbuliwa na maumivu ya tumbo chini ya kitovu mara kwa mara hupata athari nyingi baadaye endapo kama hawatagundua chanzo cha maumivu hayo.Katika tumbo la mwanamke kuna mfumo wa kawaida wa tumbo ambao ni tumbo … Read More
  • MZUNGUKO WA HEDHI USIOPEVUSHA MAYAI (ANOVULATORY CYCLE) Katika makala zilizopita tuliwahi kuzungumzia kwa undani kuhusu mzunguko wa hedhi na jinsi mwanamke anavyoweza kupanga kupata ujauzito.Tuliona mpangilio wa kupata ujauzito huwa kwa mwanamke mwenye mzunguko unaopevusha may… Read More
  • KUVURUGIKA KWA MZUNGUKO WA HEDHI Mzunguko wa hedhi umegawanyika katika maeneo makuu mawili. Kuna ule unaopevusha mayai ‘Ovulatory Cycle’ na usiopevusha mayai ‘Anovulatory Cycle’. Aina hizi za mizunguko tutakuja kuziona kwa undani katika makala zijazo, l… Read More
  • MUHIMU KUJUWA WAKATI UNA MIMBA Wanawake wengi hujua wameshika mimba aghalabu wiki 3 baada kushika mimba. Mwili wenyewe utakuonyesha/utakutabiria kama:Hedhi yako itakoma/itakuwa nyepesiUtasikia uchefuchefu/utatapika (ugonjwa wa asubuhi – ‘morning sickness… Read More

0 comments:

Post a Comment