Ugonjwa wa Genital Warts ni hali ya kuota vinyama kwenye ngozi au utando laini unaozunguka maeneo ya siri, ni ugonjwa unaoenezwa kwa njia ya kujamiiana (sexually transmitted infection kifupi STI).
Ugonjwa huu unaweza kutokea kwenye uume, uke, mrija wa mkojo (urethra), shingo ya kizazi (cervix) au maeneo ya kuzunguka njia ya haja kubwa au ndani yake.
Ugonjwa huu unaweza kutokea kwenye uume, uke, mrija wa mkojo (urethra), shingo ya kizazi (cervix) au maeneo ya kuzunguka njia ya haja kubwa au ndani yake.
Ugonjwa huu husababishwa na jamii ya virusi wanaoitwa kitaalamu Human Papilloma Virus (HPV) ambavyo vipo zaidi ya aina 70 tofauti ingawa si wote wanaosababisha maradhi haya ya maeneo ya siri.
Baadhi ya aina nyingine za HPV husababisha kutokwa na vinyama kwenye ngozi inayozunguka sehemu nyingine za mwili kama vile kwenye mikono au miguu.
Baadhi ya aina nyingine za HPV husababisha kutokwa na vinyama kwenye ngozi inayozunguka sehemu nyingine za mwili kama vile kwenye mikono au miguu.
Baadhi ya aina za virusi wa HPV pia husababisha saratani ya shingo ya kizazi kitaalamu huitwa Carcinoma of the cervix kwa wanawake au saratani ya njia ya haja kubwa, kwa jinsia zote mbili.
Ugonjwa huu wa kuota vinyama sehemu nyeti umejitokeza kwa kasi kubwa na watu wengi waliopatwa na ugonjwa huu huwa hawaoneshi dalili zozote zile.
Ugonjwa huu wa kuota vinyama sehemu nyeti umejitokeza kwa kasi kubwa na watu wengi waliopatwa na ugonjwa huu huwa hawaoneshi dalili zozote zile.
Kwa upande wa wanawake, virusi wa HPV wana uwezo wa kusambaa mpaka maeneo ya ndani kabisa ya kuta za uke au shingo ya kizazi (cervics) bila dalili kujitokeza.
Kama tulivyotangulia kueleza hapo awali, maambukizi ya HPV husambaa kutoka kwa mtu mmoja mpaka mwingine kwa njia ya kujamiiana kunakohusisha njia ya haja kubwa, uke au ngono ya mdomoni.
Mara baada ya kuambukizwa, huweza kuchukua mpaka muda wa wiki sita hadi miezi 6 kwa ugonjwa wa kuota vinyama kujitokeza wazi, ingawa baadhi ya wagonjwa wanaweza kukaa hata miaka kadhaa bila kuwa na dalili yoyote ile.
0 comments:
Post a Comment