Sunday, 31 August 2014

MAUMIVU CHINI YA KITOVU KWA WANAWAKE NA WANAUME-2




Wiki iliyopita nilianza mada hii ambayo leo nitahitimisha. Maumivu chini ya kitovu hutokea kama ifuatavyo: Yapo yale ya chini ya kitovu katikati, kushoto na kulia.
Kwa wanawake maumivu ya kushoto na kulia yapo ya aina mbili. Kuna yale ambayo yanakuwa upande mmoja lakini husambaa kwa urefu wa sentimita mpaka nne na inaweza ikawa upande mmoja au pande zote mbili lakini yapo mengine chini ya kitovu ambayo yanaweza yakawa upande mmoja au pande zote mbili bila kusambaa kwa marefu.
Kuna maumivu mengine chini ya kitovu huwapata wanawake wakati wanaposhiriki tendo la ndoa kwa ndani ya uke au chini ya kitovu.
Pia yapo ambayo huwapata wanawake wakati wameinama, wakati wa kunyanyua vitu vizito, wakicheka au kuimba na wakati mwingine wakiwa wamelala kifudifudi.
Maumivu chini ya kitovu ambayo yanaambatana na tumbo kujaa gesi, miungurumo ya tumbo, maumivu ya kiuno, kichomi kifuani kuelekea mgongoni, uchovu wa mara kwa mara na maumivu ya kichwa huashiria tatizo la vidonda vya tumbo. Hii ni kwa jinsi zote yaani wanawake na wanaume. Kwa hiyo ni vema ukapata vipimo vya tatizo hilo na tiba.
Maumivu chini ya kitovu wakati wa hedhi huashiria tatizo ambalo kitaalamu linaitwa Dysmenorhea. Kuna Primary Dysmenorhea na Secondary Dysmenorhea. Primary Dysmenorhea huwakumba wasichana wadogo ambao wapo chini ya miaka ishirini na hasa ambao bado hawajashika ujauzito wa kwanza.
Hii inatokana na kemikali aina ya prostaglandin ambayo hutumwa kwenye mji wa mimba na husinyaza kipenyo cha mishipa ya damu ya mji wa mimba kitu ambacho husababisha mgandamizo mkubwa wakati wa hedhi kwa kuwa damu hupita nyingi wakati kipenyo au njia ya damu huwa kidogo.
Secondary Dysmenorhea huwakumba akinamama ambao tayari wanakuwa wameshajifungua mtoto mmoja au zaidi lakini wanapatwa na maumivu makali wakati wa hedhi, jambo ambalo hakuwa nalo siku za nyuma.

0 comments:

Post a Comment