Sunday, 31 August 2014

KUONDOA KABISA KIZAZI KWA WANAWAKE NA WANAUME



KUNA njia ya kufanya watu wasiweze kuzaa au kutunga mimba kabisa katika maisha yao.
Hii kwa maneno mengine tunaweza kusema ndiyo njia pekee ya kudumu na uhakika ya kuzuia mimba.Vasectomy ni njia ya upasuaji mdogo inayoweza kumfanya mwanaume asiwe na uwezo wa kumpa mimba mwanamke. 
Tubuligation ni njia ya kumfanya mwanamke asiwe na uwezo wa kushika mimba. Nji zote hizi hufanyika kwa njia ya upasuaji mdogo.
Mwanaume anafanyiwa upasuaji (yaani vasectomy) kwa kukata vibomba vinavyopitisha mbegu za kiume kutoka kwenye makende hadi kwenye uume. Upasuaji kwa mwanamke (yaani tubuligation) unahusisha kukatwa au kuzibwa kwa vibomba vinavyopitisha mayai kutoka kwenye mirija iitwayo  ovari hadi kwenye mfuko wa uzazi.
Baada ya upasuaji huu, ni vigumu mwanamke au mwanaume kurudishwa tena katika hali ya mwanzo ya kuweza kuzaa, kwa hivyo njia hii inatumiwa tu kwa sababu za kimatibabu au ikiwa mhusika amefikia uamuzi wa hakika kwamba hataki tena kupata watoto katika maisha yake.
NJIA NYINGINE YA KUZUIA MIMBA
Kuna njia nyingine za kuzuia mimba kama vile kitanzi au koili, ambacho kitaalam kinajulikana kama Intra-uterine device au IUD hutengenezwa kwa plastiki na shaba na hupachikwa kwenye mfuko wa uzazi na daktari au muuguzi kwa ajili ya kuzuia mwanamke kupata mimba.
Kitanzi au koili kinakadiriwa kuzuia mimba kwa asilimia 98 na 99. Na pindi kikitolewa asili ya uwezo wa wanamke wa kushika mimba anapofanya ngono, unarudi vilevile.
USHAURI
Hata hivyo, moja ya matatizo ya kitanzi ni kwamba vinaweza kuifanya hedhi yako kuwa nzito (damu kutoka nyingi) na pia huenda ukapatwa na maumivu, mara nyingine inaweza kutoka mahali kilipowekwa na kusukumwa nje ya mfuko wa uzazi.
Hivyo ni vyema kumuona daktari mara kwa mara ili kama imechomoka, ipachikwe tena vyema.
Kwa upande wa njia ya upasuaji ieleweke kuwa ni vigumu mwanamke au mwanaume kurudishwa tena katika hali ya mwanzo ya kuweza kuzaa, hivyo basi  njia hii inatumiwa tu kwa sababu za kimatibabu au ikiwa mhusika amefikia uamuzi wa hakika kwamba hataki kupata watoto.
NJIA YA ASILIA YA KUZUIA MIMBA
Njia hii ya asilia ya kuzuia mimba inahitaji umakini sana kuitumia. Kwani inafanya kazi tu ikiwa mwanamke anafanya mapenzi tu wakati ule ambao kiasilia hawezi kushika mimba.
Hii inawezekana kwa kutayarisha tarakimu za siku za hedhi na kupima hali ya joto la mwili. Njia hii inahitaji uangalifu na uzoefu mkubwa kwa vile ni ya kubahatisha, haipendekezwi kwa vijana ambao hawako tayari kupata mtoto.
USHAURI
Kwa bahati mbaya watu wengi hudhani kwamba kutoa uume kutoka ukeni, pindi tu kabla ya kufikia kilele, ni moja ya njia za kuzuia mimba.
Ieleweke kuwa mara nyingi mbegu za kiume hutangulia kutoka hata kabla ya kufikia kilele katika hali ya kufanya mapenzi. Hivyo basi hata ukitoa uume huenda umeshachelewa na mwanamke anaweza kupata mimba.

0 comments:

Post a Comment