Wednesday 20 August 2014

KITUNGUU SAUMU KINGA YA SARATANI NA MALARIA




Kwa baadhi ya watu kitunguu saumu kina harufu mbaya, wengine huweza kuharisha, kuamsha vidonda vya tumbo au kusababisha harufu mbaya mdomoni.


KWA UFUPI


  • Kitunguu saumu ni miongoni mwa viungo muhimu vya chakula hapa nchini, ingawa watu wengi hukitumia kwa kuongeza harufu kwenye chakula bila kufahamu matumizi yake yenye manufaa kiafya


Harufu yake siku za sikukuu, umuhimu wake kwenye chakula kipendwacho na wengi Tanzania yaani pilau, umekifanya kuwa kiungo muhimu cha chakula nchini.

Kwa sasa umaarufu wake umeenda mbali zaidi baada ya wanasayansi kubaini kuwa kitunguu saumu kina kinga muhimu katika mwili wa binadamu, kambayo huweza kuzuia maradhi ikiwemo saratani na malaria.

Wanasayansi walibaini kuwa kitunguu saumu kina kemikali ya ‘allicin’ ambayo hutoka baada ya kukatwa au kutafunwa na husaidia kuzuia maradhi ya saratani na malaria.

Inaaminiwa kwamba kitunguu saumu huweza kupunguza athari za kemikali nyingine zisizofaa mwilini hasa zitokanazo na moshi na kuimarisha uwezo wa seli za mwili.

Utafiti umeonyesha pia kwamba huweza kusaidia kwa wale wenye matatizo ya mafua na hata kuukinga mwili dhidi ya malaria na saratani.

Mkurugenzi wa Kituo cha Afya Tiba cha Neema Herbalist & Nutritional Foods Clinic Dk Africanus Boniface anasema, kitunguu swaumu ni jamii ya vitunguu ambavyo kwa kitaalamu huitwa Allium sativum. Jamii hii ilianza kutumika katika mabara mbalimbali duniani hususani Asia, Afrika na Ulaya takribani miaka 6000 iliyopita. Matumizi makuu nyakati hizo yakiwa viungo katika mboga na tiba.

“Kitunguu swaumu kimetajwa kwenye vitabu mbalimbali vya dini vikielezea faida zake katika kutibu maradhi mbalimbali yasababishwayo na bakteria, matatizo katika mapafu, matatizo katika mfumo wa umeng’enyaji chakula, na matatizo ya kuishiwa nguvu.

“Historia inaonyesha kuwa, vitunguu swaumu vilianza kutumika China mwaka 510 K.K na pia vilitumiwa na wanajeshi wa Ugiriki na Roma. Sifa kuu zinazokifanya kitunguu swaumu kuwa na uwezo na faida zilizoainishwa hapo juu ni kule kuwa kwake na viasili kadhaa (ingredients) ambavyo vinafanya kazi tofauti tofauti,” alisema Dk Boniface.

Uwezo wake kiutendaji;

“Dk Boniface anasema vitunguu swaumu vina uwezo wa kusababisha kutanuka kwa mishipa ya damu (vasodilation), kwa kubadilisha ‘polysulfides’ zilizopo ndani yake kuwa ‘hydrogen sulfides’ kwenye seli nyekundu za damu.

“Na pia husaidia udhibiti wa kiwango cha sukari mwilini kwa kushusha kiwango cha kemikali ya ‘homocystine’ na kupunguza madhara ya kisukari. Iwapo vitapondwa pondwa vizuri, vitunguu swaumu hutoa kemikali iitwayo Allicin ambayo ni dawa dhidi ya bateria, na ‘phytoncide’ ambayo huua fangasi wa aina mbalimbali,” alisema.

Alisema harufu mbaya au nzuri ya kitunguu swaumu hutokana na gesi aina ya ‘hydrogen sulfide’ ambayo hutolewa baada ya kuvila.Dk Boniface anasema, kitunguu kinatibu maradhi mbalimbali kama vile: Saratani ya tumbo na utumbo mkubwa, huzuia kusanyiko la chembe sahani zinazosaidia kuganda kwa damu (platelet aggregation), katika kupunguza kusanyiko la lijamu (cholesterol) pamoja na mafuta yasiyofaa mwilini (low density lipoproteins) katika mishipa ya damu.

Athari zake mwilini


Hata hivyo Mkurugenzi wa Kituo cha huduma ya ushauri nasaha, lishe na afya COUNSENUTH, Mary Materu yeye anasema kitunguu swaumu kina faida nyingi lakini kinaweza kuathiri mwili wa mwanadamu iwapo kikitumika wakati usiofaa.

“Ukiacha faida zake, vitunguu saumu pia vina hasara na madhara mbalimbali kwa mtumiaji. Madhara hayo ni pamoja na: Harufu mbaya mdomoni ambayo hutokana na kemikali ya AMS (allyl methyl sulfide). Harufu mbaya hii, hata hivyo, yaweza kupunguzwa kwa kunywa maziwa au kunywa maji mengi.

0 comments:

Post a Comment