Sunday, 13 July 2014

MAUMIVU KATIKA TITI (BREAST PAIN)



  • Karibu asilimia 20 hadi 40 ya wagonjwa maumivu hayo huweza kuisha yenyewe, iwapo vipimo havijaonyesha vivimbe au uvimbe kwenye titi basi dawa hutolewa ili kutoa maumivu hayo. Zipo dawa za kunywa au kuchoma katika ziwa, lakini pia dawa hizi husaidia kutuliza maumivu kwa muda, ingawa baadhi ya wagonjwa zimewasaidia kupona.


           


Tatizo hili huwapata zaidi wanawake kuliko wanaume,hujulikana kitaalamu kama mastalgia, takribani theluthi mbili ya wanawake hukumbwa na tatizo hili. Kwa ufafanuzi ni maumivu yenye ukali wa kumfanya mwanamke atafute matibabu.
Maumivu haya huweza kuhusisha titi moja au yote mawili, kuhusisha sehemu fulani na huweza kutokea wakati mwanamke yuko katika hedhi (cyclic mastalgia) au wakati wowote bila kujali hedhi au la (acyclic mastalgia).

Maumivu ya titi wakati wa hedhi huwapata zaidi wanawake kwenye kundi la miaka 30, huweza kuisha pale siku zake za kila mwezi zinapoanza kusimama (menopause) yaani miaka 45 au 50. Maumivu ya hayo yanayomtokea mwanamke bila kujali kipindi cha hedhi na huwakumba zaidi wanawake katika umri wa miaka 40 na kuendela. Kutumia dawa za kuongeza homoni za kike (hormonal replacement therapy) huongeza ukubwa wa tatizo, pia aina ya vyakula vyenye mafuta.

Ni vyema kwa mgonjwa kwenda kwa daktari. Muhimu pia. Mtoa matibabu atatumia njia tatu kumchunguza mgonjwa ili kubaini chanzo cha maumivu au ukubwa wa tatizo. Njia hizo ni kupima titi la mgonjwa, kumfanyia vipimo vya radiologia mfano altrasaundi au mamograf, kuchukua sehemu ya uvimbe kama upo kwa sindano maalumu au majimaji na kupima maabara. Hii husaidia kujua kama kuna saratani ya ziwa au hapana.

Karibu asilimia 20 hadi 40 ya wagonjwa maumivu hayo huweza kuisha yenyewe, iwapo vipimo havijaonyesha vivimbe au uvimbe kwenye titi basi dawa hutolewa ili kutoa maumivu hayo. Zipo dawa za kunywa au kuchoma katika ziwa, lakini pia dawa hizi husaidia kutuliza maumivu kwa muda, ingawa baadhi ya wagonjwa zimewasaidia kupona.

Maumivu katika titi husababisha mgonjwa kushindwa kufanyakazi hivyo kipato kupungua, kushindwa fanya tendo la ndoa, kushindwa kujumuika vyema na jamii inayomzunguka, nahata kuleta msongo mawazo. Ni rahisi kiasi kutibu maumivu ya ziwa yanayoambatana na siku za hedhi kuliko yale yayotokea muda wowote.

0 comments:

Post a Comment