Thursday 24 July 2014

MAAJABU YA TUNDA LA STAFERI KUPONYA MARADHI YA KANSA (CANCER)





MAAJABU YA STAFELI
TUNDA la stafeli linatibu
magonjwa kadhaa, ikiwamo
saratani kwa ubora wa karibu
mara 10,000 ya matibabu ya
kawaida yanayopatikana

kwenye vituo vya afya, utafiti umebaini. Utafiti huo uliofanyika katika
Chuo Kikuu cha Dawa cha Purdue
nchini Marekani, umeeleza kuwa
mbali na kutibu saratani, tunda
hilo pia ni tiba ya matatizo ya

Msongo na mfadhaiko. “Maajabu ya stafeli ni kwamba
lina uwezo wa kuangamiza
chembehai zenye saratani pasipo
kusababisha madhara katika

mwili kama zinavyofanya dawa
nyingine za ugonjwa huo au mionzi,” imesema sehemu ya
utafiti huo uliochapishwa kwa

mara ya kwanza katika Jarida la
Kemia na Madawa la nchini

Marekani, mwaka 2010. Taasisi ya utafiti wa Saratani ya
Nchini Uingereza(NIR) ilifanya
utafiti wa kwanza kuhusu

Maajabu ya stafeli mwaka 1976. Katika utafiti huo ilibainika kuwa
majani, mizizi na tunda la stafeli,
vina uwezo wa kutibu saratani,
lakini matokeo ya utafiti huo
hayakutangazwa kwa umma

kwa hofu ya kuua viwanda vya dawa za saratani. Inaelezwa kuwa kirutubisho
kilichopo katika stafeli kinatumia
jina la kibiashara la
‘Triamazon’ na kimepigwa
marufuku kutumika nchini

Uingereza na Marekani kutokana na uwezo wake mkubwa wa
kitiba. Utafiti mwingine uliofanywa na
Chuo Kikuu cha Kikatoliki nchini
Korea na kuchapishwa katika
jarida la Bidhaa Asilia ulibaini
kuwa stafeli lina uwezo wa

kuponya saratani ya tumbo. Utafiti wa chuo hicho ulienda
mbali na kusema kuwa tunda hilo
linaweza kulenga seli za saratani
tu, bila kushambulia seli muhimu
za mwili kama ambavyo tiba ya

mionzi ifanyavyo. Tunda la Stafeli lina kirutubisho
muhimu kiitwacho Annona
Muricata, ambacho ndicho chenye
uwezo wa kupigana na maradhi

ya saratani. Imeelezwa kuwa stafeli lina
uwezo wa kutibu aina 12 za
saratani ikiwemo ya matiti,
kongosho, mapafu na ya kibofu
cha mkojo. Pamoja na kutibu saratani,

kirutubisho hicho kilichopo katika
tunda hilo pia huweza kutibu
vimelea, shinikizo la damu,
msongo wa mawazo, matatizo ya

mfumo wa fahamu na sukari. Utafiti huo unaonyesha kuwa
kirutubisho kimegwacho katika
tunda hilo kinaweza kwa asilimia
kubwa kupambana na saratani
bila kumuacha mgonjwa na
madhara kama kusikia kichefuchefu, kutapika, kupungua
uzito na kunyonyoka nywele.

0 comments:

Post a Comment