Tuesday, 8 July 2014

KUJUA MAANA YA NAMBA YAKO YA SIMU...........





Unapotaka kutafsiri namba yako ya simu tumia tarakimu nne za mwisho kwani hizi ndizo namba pekee ambazo ni tafauti na za watu wengine katika mtandao mmoja.
Jumlisha tarakimu hizo nne hadi ufikie jumla ya tarakimu moja (single digit) yaani jumla iwe kati ya 1 na 9.
Mfano:
kama namba yako ni 07xxxx1407.
Chukua 1407 
kisha jumlisha 1+4+0+7=12.
kisha chukua 12;1+2=3.
Kwahiyo jumla yako inakuwa  "3"
JUMLA IKIWA 1.
Hii ni namba yenye nguvu sanana ni namba ya kiume, ambayo inakuza nguvu zako binafsi ambayo inakuwezesha pia kuwashawishi watu wengine. Tahadhari usiwe mbabe kwa watu. Hii pia ni namba nzuri sana kwa biashara na kazi lakinisio namba nzuri ya aliye mpweke kumtafuta mpenzi.
JUMLA IKIWA 2.
Hii ni namba ya mapenzi, ni namba nzuri kwa walio wapweke kutafuta wapenzi. Namba hii inaashiria hisia, mawasiliano ya kibusara na ushirikiano, pia ni namba nzuri ya biashara ya huduma na sio nzuri kwa madalali na watu wabishi.
JUMLA IKIWA 3.
Namba hii inaashiria ubunifu, ucheshi, hii ni namba nzuri kwawasanii, wanamziki na vijana. Namba hii haina muelekeo lakini ina mvuto na ni asilia. Ni namba nzuri sana kwa waandishi na watunzi wa nyimbo sio namba nzuri sana kwa watu wanaojituma sana na wenye malengo makubwa.
JUMLA IKIWA 4.
Hii ni namba thabiti, iliyostawi,yenye kutegemewa na kuaminika, namba hii ni nzuri sana hasa kwa ma Benki, makampuni ya Uhasibu, Sheria na makampuni au masharika mengine kama hayo ambayo yanahitajika kua waaminifu na sifa za kuaminika. Pia ni nambanzuri kwa familia kubwa na wala sio nzuri kwa watu walio wapweke (Singles) vinginevyo wawe ni wanasharia au wahasibu au Wafanya kazi za kibenki.
JUMLA IKIWA 5.
Namba hii inaashiria matukio na mabadiliko ni namba liyo tulia. Tegemea usioyatarajia ni namba nzuri ya kufanya mauzo pia ni namba nzuri kwa wasafiri wanaopenda uhuru wao. Sio namba nzuri kwa familia kwani inakosa hadhi ya heshima na kuwajibika na vile vile sio namba nzuri kwa wanaopenda kula hovyo au wategemezi wa aina yoyote.
JUMLA IKIWA 6.
Hii ni namba nzuri sana kwa familia kwani ni namba inayoashiria kujali, ulinzi na inaunganisha familia na kudumisha uhusiano wa kirafikina kifamilia. Sio namba nzuri walio wa pweke.
JUMLA IKIWA 7.
Strong and spiritual, this number is ideal for scholars and free thinkers. Also improves mental health and stability. Not a good number for business.
JUMLA IKIWA 8.
Hii ni namba nzuri sana kwa biashara yoyote. Namba hii huvuta pesa na utiifu. Pia n namba nzuri sana kwa wanaojituma sana katika kazi huboresha wadhifa wako na kipato chako katika.
JUMLA IKIWA 9.
Hii ni namba nzuri sana katika kazi au huduma za kiafya au taasisi zisizo za kibiashara. Hii ni namba yeye bahati kuliko namba zote kwani wakati mwingine huweza kukuletea kipato cha juu usichokitegemeasio namba namba nzuri kwa wale wenye matatizo ya kiafya.

Related Posts:

  • MBINU ZA KUONGOZA FAMILIA KATIKA HALI DUNI KIMAISHA KATIKA moja ya masomo yangu ambayo yanapatika katika vitabu vyagu vya Saikolojia No1,2&3, niliwahi kuandika mada inayohusu mambo yanayochangia familia nzima kuwa maskini. Leo sitarudia hayo lakini nitafundisha somo la… Read More
  • NJIA 7 ZA KUONGEZA UWEZO WA KUMBUKUMBU NI jambo la wazi kwamba tunapozidi kuwa wazee huwa tunaanza kugundua mabadiliko kadhaa katika uwezo wetu wa kukumbuka mambo. Hali hii ni kama kujikuta uko jikoni lakini hukumbuki ni kwa nini ulikwenda humo, au kutoweza … Read More
  • TATIZO LA KUTOPATA RAHA WAKATI WA TENDO LA NDOA Wapo ambao wakati wanapofanya mapenzi badala ya kupata raha, husikia maumivu, mwanaume katika uume lakini ni mara chache sana kulinganisha na wanawake. Mwanamke ndiye husumbuliwa zaidi na tatizo hili. Mwanamke anaweza ku… Read More
  • JINSI YA KUISHINDA HOFU NA NGUVU YA UCHAWI-2 LAKINI jambo baya sana ambalo linawaponza watu wengi ni kwamba wanapogundua kuwa watu fulani ni maadui zao, wao nao huanza kushambulia kwa chuki.Kufanya hivyo huzifanya nguvu asili zitafutane na kushawishi mawazo yatilie… Read More
  • UMUHIMU WA KUJIFUNZA SAIKOLOJIA HUWEZI hata kidogo kutenganisha maisha ya mwanadamu na elimu ya saikolojia, elimu ambayo katika ulimwengu wa sasa wengi wanaisikia lakini ni wachache wanaotambua umuhimu wake, achilia mbali maana ya neno lenyewe. … Read More

0 comments:

Post a Comment