Tuesday, 8 July 2014

ATHARI ZA CHAI, KAHAWA KWA VIUNGO VYA MWILI




madhara ya matumizi makubwa ya bidhaa zenye caffeine na kahawa ikiwa yenye kiwango kikubwa. Wasomaji wengi mliuliza maswali mengi mkitaka kujua zaidi kuhusu athari za caffeine, hasa kwa upande wa maumivu ya mifupa na nyonga.
Mlikuwa sahihi kwa kuwa ni kweli wengi wetu tunaumwa maradhi ya mifupa na hasa nyonga, magoti na mgongo. Kitaalamu binadamu yeyote mwenye umri wa miaka 40 na kuendelea ni muathirika wa ugonjwa wa mifupa uitwao ‘Osteoarthritis’ au kwa kifupi ‘OA’.
Ni rahisi kuwanyooshea vidole watu wenye ugonjwa huu kwa kuwatazama sura zao huku ukilinganisha na umri walionao. Unywaji na ulaji wa kiwango kingi cha caffeine huharakisha mtu kukumbwa na OA kwa kuwa caffeine hushambulia zaidi mifupa kuliko sehemu nyingine ya mwili. Utaona vijana wengi zama hizi, wake kwa waume, waliochini ya umri wa maiaka 40 wanasumbuliwa na kuumwa miguu.
‘OA’ humkumba mtu baada ya katileji (cartilage) kusagika na kuisha katika maungio ya mwili pamoja na uti wa mgongo. Maumivu ya mwili huwa makali kwa sababu ya mifupa kusuguana na kusababisha jointi kuvimba na kukakamaa. Kwa bahati mbaya sana ‘OA’ huwakumba zaidi wanawake, kutokana na maumbile yao.
OA huwapata kirahisi pia watu wanene na wajawazito. Ukipatwa na jeraha kwenye jointi au ukifanyiwa upasuaji mkubwa kwenye jointi huweza kupatwa na OA pia. Lakini pia makundi mengine yaliyo hatarini ni pamoja na wanamichezo ambao wanaweza kupatwa na matatizo ya viungo kwa kuumia michezoni au kwa mtu kupatwa na ajali nyingine.
NINI CHA KUFANYA?
Dawa ya matatizo haya ni kuzingatia lishe sahihi ambayo inakutaka kuhakikisha katika mlo wako wa kila siku, unakula matunda ya kila aina, mboga za majani, nafaka zisizokobolewa na kunywa maji ya kutosha kila siku kwa kiwango cha kutosha. Hii itakusaidia kuimarisha kinga asilia ya mwili wako.
Hata inapotokea umekunywa kinywaji chenye caffeine na vyakula vingine, sumu yake haiwezi kukaa mwilini na kuathiri viungo, bali itaingia na kutoka bila kuleta madhara makubwa. Halikadhalika ukiumia au ukifanyiwa upasuaji ni rahisi kupona haraka tofauti na mtu mwenye kinga dhaifu au aliyekwisha athirika na caffeine.
Nina imani kubwa kuwa mpaka hapo wengi wetu tumepata ufahamu wa kutosha juu ya madhara ya Caffeine, nakushauri  upunguze matumizi ya Caffeine na kuzingatia ulaji sahihi.

1 comments: