Tuesday, 24 June 2014

UMUHIMU MKUBWA WA KOMAMANGA (POMEGRANATE) JUU YA MARADHI YA KANSA



Uchunguzi mpya umeonyesha kwamba, katika tunda la komamanga kuna kemikali zinazozuia kansa ya matiti isitambae mwilini.

Uchunguzi huo uliochapishwa katika jarada la Utafiti la kuzuia Kansa umeonyesha kwamba, kemikali ziitwazo ellegitannins zinazopatikana kwa wingi kwenye komamanga, zinaweza kuzuia kimeng’enyo (enzyme) aina ya aromatase, suala ambalo huzuia kukua kwa Homoni ya estrogen inayopatikana katika kansa ya matiti.

Shiuan Chen Kiongozi wa uchunguzi huo amesema kwamba, kemikali hizo hupunguza uzalishwaji wa estrogen, na kusaidia kuzuia seli za kansa ya matiti zisizaliane mwilini, pamoja na tezi la ugonjwa huo lisikue.

Aromatase, ni kimeng’enyo ambacho hugeuza Homoni ya androgen kuwa estrogen, na kushambulia kimeng’enyo hicho ndio lengo kuu la dawa za kupambana na kansa za matiti zinazosababishwa na homoni ya etrogen.

Huko nyuma pia uchunguzi ulionyesha kwamba tunda la komamanga lina faida kubwa kiafya hasa kwa kuwa na  anti Oxidant nyingi na vitamin mbalimbali, ambalo huzifanya tunda hilo liweze kusaidia katika kupambana na magonjwa ya saratani, matatizo ya moyo na hata ugonjwa wa kusahau uzeeni au Alzheimer.

Anti Oxidant huzuiaradikali huru ambazo ni hatari sana kwa miili yetu. Uwezo huo hupelekea mwili kukabiliana na magonjwa mbalimbali hata ugonjwa wa homa ya mafua ya nguruwe. Kama huwezi kupata tunda la komamanga sokoni, basi unaweza kutumia juisi ya Komamanga na daima tutunze afya zetu!

FAIDA YA JUISI YA KOMAMANGA
  1. Huweza kuzuia maendeleo ya saratani ya mapafu.
  2. Hupambana na saratani ya matiti
  3. Hupunguza ukuaji wa saratani ya kibofu
  4. Inaweza kuzuia na kupunguza kasi ya ugonjwa wa Alzheimer
  5. Inapunguza kolesterol
  6. Hushusha shinikizo la damu
  7. Hulinda meno

Inasemekana ukinywa juisi ya komamanga (pomegranate) nusu lita kila siku kwa muda wa mwezi mmoja, inasaidia kupunguza mafuta tumboni kwa wale wenye vitambi. Jitahidi kuwa na matumizi ya haya matunda unufaike na uboreshe afya yako.

Related Posts:

  • MAAJABU YA KARAFUU (SYZYGIUM AROMATICUM) KUTIBU MAGONJWA MBALIMBALI. ​ Karafuu pamoja na Unga wa karafuu Karafuu ni tumba lililokauka la maua yasiyofunguka yanayopatikana kutoka mti mzuri wa kati na kijani. Mti huu una shina lilinyooka na hukua kufikia kimo cha mita 10 hadi 1… Read More
  • ZIJUE FAIDA TISA ZA MBEGU ZA MABOGA Unaweza kuzidharau mbegu za maboga, lakini ni miongoni mwa mbegu zenye faida kubwa mwilini, zinazoweza kuzuia na kutibu hata magonjwa hatari yaliyoshindikana hospitalini. Kwa mujibu wa utafiti wa kisayansi uliok… Read More
  • PILIPILI HUIMARISHA UJASIRI NA NGUVU MWILINI! Kama ilivyo kwa matunda na vyakula vingine kuwa na faida kiafya mwilini, pilipili nayo ni moja wapo. Licha ya kuogopwa na baadhi ya watu, lakini ina kiasi kingi cha vitamin C. Umuhimu wa Vitamin C mwilini,  … Read More
  • JINSI YA KUTIBU UGONJWA WA PUMU (ASTHMA) JINSI YA KUTIBU UGONJWA WA PUMU Mahitaji:   Karafuu 6  Karafuu  Maandalizi: Zitowe vichwa vyake kisha loweka hizo karafuu katika nusu gilasi ya maji usiku kucha   Matumizi: &nbs… Read More
  • TIBA ASILIA YA TUMBO Watu wengi wamekuwa wakisumbuliwa na tumbo lisilo la vidonda wala ugonjwa wowote ila utasikia anakwambia tumbo linanikata, huenda akawa anavurugikwa na tumbo au imetokea linasumbua tu. Tiba hii hapa Kwanza k… Read More

0 comments:

Post a Comment