Saturday, 7 June 2014

UFAHAMU UGONJWA WA UKOMA



Ugonjwa wa ukoma unaambukiza, kama mtu ataambatana na mtu mwenye ugonjwa huo kwa muda mrefu sana, na ambaye hajapatiwa matibabu, mtu huyo inawezekana naye akaambukizwa ugonjwa huo.
 Dalili:
Dalili za ugonjwa huu zinatofautiana sana kutegemeana na kinga ya kibinafsi ya mtu dhidi ya ugonjwa huu.
Kwa kawaida, dalili kuu huwa ni zile za kupoteza hisia. Mara nyingi ugonjwa wa ukoma huanzia mashambulizi yake mikononi na miguuni. Mara kwa mara wagonjwa wa ukoma huugua bila kufahamu.
Dalili nyingine ya ugonjwa huu ni kufa ganzi (vidonda) na ngozi ya uso kuwa yenye vinundu vinundu.
Dalili katika ngozi zinatofautiana, nazo ni mabaka ambayo hayawashi wala hayaumi, na yasiyokua na hisia ya mguso. Kuvimba kwa mishipa ya fahamu (nerves) ngozi, na vidonda vikubwa ambavyo haviumi wala kuwasha.
 

Tiba ya ugonjwa wa Ukoma:
Ugonjwa wa ukoma unatibika bila ya malipo yoyote lakini unahitaji dawa zitumike kwa muda wa miezi 6 hadi 12 na kwa mpangilio maalum utakaoelekezwa na muhudumu wa afya.

Athari zinazotokana na ugonjwa wa ukoma
Majeraha makubwa ambayo hupelekea ulemavu wa kudumu wa mikono na miguu. Mara nyingi majeraha hayo yanatokana na sehemu iliyokufa ganzi iwapo mgonjwa mwenyewe hajikingi na vitu vyenye kumdhuru. Kwa njia hiyo, vijidudu vitapenya taratibu mpaka kwenye mifupa na kuiharibu na kusababisha ulemavu.
 

Ulemavu huo unaweza kuepukwa kwa kufanya yafuatayo;
  • Kuhifadhi mikono na miguu kutokana na vitu vyenye kudhuru (kukata, kutoa malengelenge au kuchoma) na wala usitembee miguu wazi hasa mahali ambako kuna mawe au miba.
  • Kuvaa viatu wakati wote
  • Unapotumia mikono yako ikiwemo kupika chakula, hifadhi mikono hiyo vizuri (matambara) na usinyanyue sufuria au chochote kilicho na joto bila kufanya hivyo. Hii ni kuepuka uwezekano wa kuungua bila kuhisi kuwa umeungua.
  • Ikiwezekana, epuka kazi zinazohitaji kushika vitu vikali au vyenye joto.
  • Kila siku baada ya kazi au kutembea, tazama mikono na miguu yako kwa uangalifu au ikiwezekana mwambie mtu mwingine akusaidie kutazama. Hakikisha unatazama hasa kuona kama kuna majeraha, malengelenge au miba.
  • Kama una jeraha au linaanza kutokeza, hakikisha sehemu hiyo inawekwa katika hali ya usafi na kupumzishwa mpaka iwe imepona kabisa.
“HIVYO NI VYEMA KILA MWANA JAMII AWE MAKINI”.

0 comments:

Post a Comment