Saturday, 7 June 2014

FAIDA ZA ZIPATIKANAZO KWA KULA TUNDA LA PERA





Pera

Mapera  ni  matunda  yanayo patikana  kwa wingi  lakini  mara  nyingi  huwa  hayapendelewi  sana  kutokana na  ugumu  wake  wakati  wa  kuyatafuna   pamoja  na  kuwa na  mbegu mbegu  nyingi.  Hata  hivyo  matunda  haya  yana  faida  kubwa sana  kwa afya  ya  mwili wa mwanadamu.
Zifuatazo  ni  faida  kumi za  mapera.

1. Utajiri  wa  Vitamin  C:


Mapera  ya  utajiri  mkubwa wa  Vitamin C ambayo  ni  muhimu  sana  katika  mwili  wa  mwanadamu. 


2. Ni  kinga  nzuri  ya  kisukari.



Ulaji wa  watu wengi  unawaweka  katika   hatari  ya  kupatwa  na  ugonjwa  wa  kisukari  lakini  matumizi  ya  mapera  yatakupunguzia   hatari  ya  kupatwa na  ugonjwa  wa  kisukari Hii  ni  kwa  sababu mapera  yana  utajiri  mkubwa  sana  wa  Fibre.  
Fibre  ni  muhimu  sana  katika  kupunguza  kiasi  cha  sukari  kwenye  damu.  Vilevile   ni  muhimu sana  katika kuusafisha  mfumo wa  usagaji  

3. Kuimarisha  Uwezo  Wa  Kuona 


Mapera  yana  utajiri  mkubwa  sana  wa  Vitamin  A  au  Retinol  ambayo ni  muhimu  sana  katika  kusaidia  kuona  vizuri.
Hivyo  basi  kama  ilivyo  kwa  karoti, mapera  yanasaidia   sana  katika  kuongeza  na  kuimarisha  uwezo w a  mtu  kuona.


4. Kusaidia  katika  Uzazi


Mapera  yana  madini  yaitwayo  Folate  ambayo husaidia  katika  kurutubisha  mayai ya  uzazi..


5. Kurekebisha   Kiwango Cha  Shinikizo  La  Damu


Madini  ya  Potassium  yaliyomo  ndani  ya  mapera  yanasaidia  katika   ku-normalise  shinikizo  la damu ( Blood  Pressure )
Ndizi na  mapera  vina  kiwango  cha  potassium sawa. 


6.  Utajiri  mkubwa  wa  Madini  Ya Shaba


Mapera  yana madini  ya shaba  ( Trace  element copper )  ambayo  ni  mazuri  sana  katika  ku- maintain  ufanyaji  kazi  wa   tezi  ziitwazo  thyroid.
Tezi  za  thyroid  zisipo  fanya kazi  vizuri  zinaweza  kusababisha matatizo  mengi  ya  kiafya  kwa mwanadamu.


7. Utajiri  wa  Madini  Ya  Manganese


Mapera  yana  utajiri  mkubwa  wa madini  ya  manganese  ambayo  yanausaidia  mwili   katika  kunyonya  ama  kupata virutubisho  muhimu  kutoka  kwenye  vyakula tunavyo kula.
Chakula  tunacho tumia  kikitumika vizuri mwilini, tunapata  virutubisho  vyote  muhimu  kama  vile biotini, vitamin  nakadhalika..

8.  Kuusadia  mwili  na  akili  katika  ku-relax

Mapeara  yana  utajiri  mkubwa  wa  madini  ya  magnesium ambayo   hufanya  kazi  ya  kuvifanya  akili  na  mwili  wa  mwanadamu  viweze  ku  relax.   Unashauriwa   kutumia  mapera  baada  ya  kazi  nzito. Hii itasaidia  katika  kuufanya  mwili  na akili  yako  kupumzika 


9.  Mapera  ni  muhimu  katika  afya  ya akili ya mwanadamu.



Vitamin B3, Vitamin B6  ambazo  zinapatikana  ndani  ya  tunda  la  mpera   muhimu  katika  kuimarisha  afya  ya  akili ya mwanadamu.
Mapera  yatasaidia  kuufanya  ubongo wako   u  relax.


10. NI MUHIMU  KATIKA  NGOZI  YA MWANADAMU. 

Vitamin C, viondoa  sumu  na  karotini   ambavyo  vyote  vinapatikana  ndani  ya  tunda  la  mpera  ni  muhimu  sana  katika  kuimarisha  afya  ya  ngozi.
Kama  hiyo haitoshi, kokwa  la  mpera  huwa  linatumika  katika  kutengeneza  vipodozi na  losheni  kwa  ajili  ya  matumizi  ya  mwanadamu. 


Related Posts:

  • FAIDA YA MBEGU ZA TIKITIMAJI Faida ya kutafuna mbegu za tikiti maji TIKITI MAJI ni moja ya matunda yanayolimwa sana  katika maeneo mbalimbali nchini Tanzania tofauti na miaka iliyopita. Hii inaashiria kwamba tunda la tikiti maji l… Read More
  • FAIDA YA TUNDA LA APPLE (TUFAHA) KIAFYA "Apple" kwa kiswahili nafikiri linaitwa tunda damu, Tunda hili liko la aina tofauti yako ya kijani yako mekundu na haya mekundu ndio yaliyo mazuri zaidi na pia yanasemakana matunda mazuri zaidi ni yale ya Euro… Read More
  • FAIDA ZA KIAFYA ZA KULA NYANYA.... FAIDA ZA KIAFYA ZA KULA NYANYA.... Hili ni tunda mashuhuri na lenye virutubisho ambalo kwa kawaida hutumika kama mbogamboga. Kwa wastani, watu hula takribani kilo 8 za nyanya kwa mwaka. Nyanya zina aina mbalimbali z… Read More
  • FAIDA ZIPATIKANAZO KWA KUTUMIA TUNGUJA PORI,NYANYA ZA MSHUMAA/CHUNGU/NGOGWE KIAFYA. Wengi tumekuwa tukitumia kama mboga au kiungo kimoja wapo katika kunogesha mboga lakini wachache mno wanaojua faida za nyanya chungu kiafya. Pamoja na kufanya mboga kuwa na ladha na harufu ya aina yake, nyanya chu… Read More
  • SIRI YA PAPAI KATIKA UREMBO WAKO TUNDA la papai lina vitamini C na E,  lina siri kubwa ya urembo na hutumika kutengeneza facial za aina mbalimbali. Papai limekuwa likitumiwa kama tunda kwa kula lakini pia kwa kupaka na humfanya mtu awe na ngozi ya a… Read More

1 comments:

  1. Mko vzur wakuu tuleteeni vitu ving vya kutusaidia mwilin kwetu

    ReplyDelete