Saturday 14 June 2014

TIBA YA KUTUMIA BAMIA KIMATIBABU



FAIDA YA KUTUMIA BAMIA KIMATIBABU.
Chimbuko la Bamia ni Abyssinia (Ethiopia)

Kisha ikaenea Duniani kote.

1. Michirizi na utonvu unaopatikana katika
Bamia, husaidia kusawazisha Kisukari kwa
kuzuia kiwango cha Sukari inayotumika katika
mwili kutoka kwenye utumbo mkubwa.

2. Utelezi wa bamia huchuja uchafu unaoingia
katika Kolestorali (cholesterol) na asidi ya
Nyongo unaoingia kutoka kwenye Ini ambao
usipo dhibitiwa huenda ikasababisha matatizo
ya ki-afya.

3. Bamia husaidia kulainisha Utumbo mkubwa
(large intestines) kutokana na kazi yake ya
kulainisha choo.

4. Bamia hutumika kwa kutibu vidonda vya
Tumbo inasaidia kusawazisha Asidi.

Magonjwa Maalum

Asidi ya Kujirudia rudia na Kufunga Choo
Tafuna vipande sita vya Bamia bila kutumia
dawa nyigine kilasiku na Asidi ya Kujirudia
rudia na kufunga choo kutakwisha, inashusha
Sukari kutoka 135 hadi 98

Pumu

Bamia ina Vitamin C ambayo inawafana
watoto wanaougua ugonjwa wa pumu
kupumua vizuri wanapoitumia. Nusu kikombe
ya Bamia iliyopikwa huwa na miligramu 13 ya
vitamin C.

Kidonda Ndugu (Cancer)
Bamia husaidia kuweka Utumbo kuwa na hali
nzuri hivyo kupunguza uwezakano wakuugua
ugonjwa huu wa Kansa hasa kwenye utumbo
mkubwa.

Mishipa midogo ya Damu Kula Bamia kwa
wingi kunasaidia kuimarisha Mishipa midogo
ya Damu.

Cataracts
Nusu kikombe cha Bamia iliyopikwa inakua na
kiwango cha 460 IU ya vitamin A.ambayo
inapunguza uwezakano wa kupata ugonjwa wa
mtoto wa jicho (cataracts).

Usongo (Depression) na Kukosa Nguvu. Bamia
ni mboga bora zaidi kwa wale wanaojisikia
dhaifu, Kuchoka na wanao athirika na Usongo
(depression)


0 comments:

Post a Comment