Tuesday 17 June 2014

SABABU 18 ZA KUPUNGUZA UZITO




sababu 18 zinazokulazimu upunguze uzito wako na uogope unene na zote ni hizi zifuatazo:
1. Unene unaongeza kiwango cha mafuta mwilini, ambayo huongeza uwezekano wa kupata kansa.
2. Unene unaongeza mafuta mwilini, ambayo hufanya matibabu ya kansa kuwa magumu zaidi.
3. Unene huongeza mafuta mwilini ambayo huushinikiza na kuubana moyo. 
4. Mtu mnene huwa mvivu kufanya mazoezi, suala ambalo humuongezea zaidi unene.
5. Mafuta mengi mwilini yana madhara kwa ubongo.
6.Unene huathiri hata tabia na miamala ya mtu.
7. Unene huongeza uzito katika mifupa na viunga vya mifupa (bone joints).
8. Unene husababisha kibofu cha mkojo kibanwe suala linalosababisha matatizo mbalimbali ya mkojo.
9. Unene hupunguza uwezo wa kujamiiana wa mtu.
10. Unene hupunguza uwezo wa kuzaa na hata kusababisha utasa na ugumba.
11. Unene huweza kuufanya mwili upatwe kwa wepesi magonjwa mbalimbali kama vile kisukari na presha.
12. Watu wanene wanapofika hospitalini upimaji wao pia huwa wa matatizo.
13. Unene husababisha ujauzito kuwa wenye matatizo mengi.
14. Unene huathiri pia afya ya mtoto mchanga anayezaliwa.
15. Unene hufanya matibabu ya pumu (asthma) yawe magumu.
16. Unene hupelekea mtu asilale vizuri na wakati mwingine mtu mnene anapolala hubanwa na pumzi suala linalomfanya aamke mara kwa mara.
17. Unene humfanya mtu ashindwe kuwajibika vizuri kazini na hata kuathiri utendaji kazi wake.
18. Unene hufanya matumizi ya fedha kuwa makubwa unapokumbwa na magonjwa yasababishwayo na unene.

0 comments:

Post a Comment