Monday, 23 June 2014

KUTIBU KUNUKA MDOMO MTU


Mara nyingi mtu huwa hajijui kama anatoa harufu mbaya mdomoni mwake, hii ni kwasababu ya cells wa pua huwa tayari washajikubalisha na ile harufu ya mdomo na aghlabu humfanya mtu asijijue kuwa yeye anatoa harufu mbaya.
Kuna sababu nyingi zinazomfanya mtu atoe harufu mbaya ya mdomo miongoni mwao ni:-
Upungufu wa usafi
Mara nyingi mtu mwenye kutoa harufu mbaya huwa hashughuliki katika usuguaji mzuri wa meno,Hupiga mswaki juu juu tu.

Uutumiaji wa tumbaku na vitu kama hivo
Mtu mwenye kutumia tumbaku hufanya mdomo wake uwe na harufu mbaya hii ni juu ya bakteria wanaojijenga katika meno.

Matatizo ya Sinus (mvimbo/mzibo wa ndani ya pua)
Tatizo hili linaweza kumkuta mtu yeyote yule kwani maradhi haya yanatokana na allergies au enviromental situation.
Mara nyingi pua huziba na kusababisha makamasi kupita katika njia ya koo na huifanya koo kutoa harufu mbaya ambayo hupitia mdomoni.

Tonsis
Maradhi haya pia husababisha maradhi ya kutoa harufu mbaya mdomoni.

Na sababu nyengine ambazo husababisha maradhi ya harufu mbaya ni kama diabetes, kidney failure, Chronic Bronchitis & Decay teeth.
Lakini kama ilivyo kuwa hakuna maradhi bila dawa lakini dawa ya maradhi haya ni usafi wetu sisi wanaadamu.
Hizi ni njia ambazo zitamsadia mtu kuondosha harufu mbaya ya mdomo:
Mtu anapopiga mswaki ni lazima asugue ulimi wake mara tatu na kawaida ya kupiga mswaki upige kwa muda wa dakika 15.
Pia ni muhimu kwenda kumuona daktari wa meno muda baada muda
Tumia mswaki mmoja kwa muda wa miezi 3 tu baada ya hapo badilisha mswaki. Hii ni kuepuka kuumiza meno na mafizi kwa kutumia mswaki kwa muda mrefu.
Kila baada kumaliza chakula piga mswaki laa kama upo sehemu ambayo huwezi kupiga mswaki basi sukutua kinywa chako hadi uhakikishe huna mabaki ya chakula.
Kula Carrot kwa wingi baada kumaliza chakula
Kunywa maji mengi
Tumia mouthwash kwa kusukutua na hakikisha unapiga mswaki kabla ya kwenda kulala.
DAWA YA KUNUKA MDOMO
jaribu kila mara kwenye kinywa chake Uwe Unatafuna kitu kama hiliki,ubani vizuri 
inasaidia kukata harufu ya mdomo. 

Na Hizi dawa Ufanye kila mara Ufanye mara 2 kwa siku Asubuhi na jioni.

1.Tangawizi ya unga fresh
2.Pilipili manga ya unga
3.chumvi.

Vyote fanya kiasi uchanganyishe viwe pamoja tena utafanya wewe mwenyewe kiasi tia katika chupa uwe kila mara
unasugulia kwa kidole au unaweza ukanunua msuaki ukauweka kwa kupigia hiyo tangawizi jaribu na inshallah
Mwenyeezi Mungu atakusaidia hata ikiwa meno yako yanatoka damu hii dawa inasaidia pia.

Related Posts:

0 comments:

Post a Comment