Monday, 23 June 2014
JINSI YA KUONDOA HARUFU MBAYA KWAPANI
Hakikisha unaoga kila siku ili kupunguza idadi ya bakteria kwapani kwani husababisha kuweka harufu mbaya kwenye mwili hasa majira ya joto kwa kuwa mara nyingi joto ndilo husababisha jasho na harufu kwapani hivyo unahitaji kuoga mara mbili kila siku, unaweza kutumia sabuni au anti-bacterial na maji ya moto.
Safisha nguo katika maji ya moto na sabuni ya kuondoa uchafu na mafuta, vaa mashati safi. Inapendekeza kuvaa mavazi yenye nyuzi za asili, kama vile pamba na hariri ili kusaidia kunyonya unyevunyevu na kuruhusu ngozi kupumua.
Wakati unafanya mazoezi, tumia nguo zenye vitambaa ambavyo vitanyonya unyevunyevu kwapani ili kuzuia harufu mbaya.
Vinega ‘siki’ na mafuta ya chai ‘ tea tree oil’
Apple cider siki na vinega nyeupe, hupunguza harufu kwapani. Ili kukabiliana na harufu, loweka pamba katika vinega, paka kwenye makwapa badala ya deodorant. Mbali na tiba hiyo, tumia tea tree oil, inaweza pia kuwa na manufaa kwa sababu ni anti-bacterial.
Limao
Kata limao au ndimu nusu kwa kisu. Paka kipande cha limao ulichokata kwenye kwapa lako na hakikisha unalisugua mpaka litoe maji yake. Weka kwapa lako lipate hewa ili hiyo juice ya limao uliyopaka ikauke.
Asidi citric katika maji ya limao inasaidia kutoa tezi ya jasho hivyo kuondoa harufu.
Makala hii ni kwa msaada wa Bongo urembo, wiki ijayo nitajibu maswali yenu yote, asanteni kwa kunisoma.
Related Posts:
TIBA YA MBA KWA KUTUMIA MBEGU ZA MPAPAI Mbegu Za Papai Tiba ya Mba Pia mapapai yaliyoiva yanatibu mapunye (ringworm), mabichi yanatibu msukumo mkuu wa damu (high blood pressure), mapapai yanatumika kama mkuyati (aphrodisiac), yanatumika kama kituliza maumivu… Read More
BAMIA INAWEZA KUTIBU TATIZO LA KISUKARI Wanasayansi nchini Marekani wamegundua kuwa Bamia ina virutibisho vinavyo weza kumsaidia mtu mwenye tatizo la Sukari.… Read More
DAWA YA KUTIBU UGONJWA WA TETEKUWANGA (CHICKEN POX) Tetekuwanga ni ugonjwa unasababishwa na virusi viitwavyo Varicel Zoster. Ugonjwa huu una ambukizwa kwa haraka sana. Vipele hufanana na malengelenge; na vinawasha sana. Ugonjwa huu ni wa hatari zaidi kwa watoto wachang… Read More
VYAKULA VYA KULA KILA SIKU ILI KUITHIBITI PRESHA YA KUPANDA Foods to eat to control high blood pressure 1) (Garlic is natural medcine for treating high blood pressure) KULA KITUNGUU SAUMU JAPO PUNJE MOJA KILA SIKU ASUBUHI NA USIKU. 2) (Don't add salt) … Read More
UGONJWA WA MAFINDOFINDO (TONSILS) Tonsil husababishwa na sababu nyingi tu . Pia husababishwa na upungufu wa white blood Cells katika mwili ambazo cells hizi ndio hupigana na vidudu vyote venye kuleta maradhi ndani ya mwili sasa vinaposhindwa kufanya kaz… Read More
0 comments:
Post a Comment