Thursday, 19 June 2014

AFYA YA NGOZI :HAMIRA JAMII YA FANGASI WENYE MADHARA MWILINI



  • Kwa kawaida, maradhi haya hushambulia zaidi vijana walio katika umri wa balehe na watoto.

  • Katika mwendelezo wa makala yetu ya maradhi ya ngozi tunaendelea kuangalia maradhi ya ngozi yatokanayo na fangasi, leo tukiangalia hamira (yeast) yanavyoshambulia sehemu mbalimbali za mwili. Maradhi haya kitaalamu huitwa tinea versicolor


    Utango tango (mba)


 



Mba ni maradhi maarufu zaidi kati ya magonjwa mengi yanayosambazwa na fangasi wanaoitwaMalassezia furfur ambao kwa kawaida huishi kwenye ngozi ya watu wazima bila kusababisha matatizo yoyote ya kiafya.

Vimelea hivi husababisha ngozi kwenye sehemu ndogo ya mwili kubadilika rangi ukilinganisha na rangi ya ngozi ya sehemu ya mwili iliyoizunguka.

Mba hushambulia nani?
Kwa kawaida, maradhi haya hushambulia zaidi vijana walio katika umri wa balehe na watoto.

Mwonekano wake
Maradhi haya hutambulika kwa namna mbalimbali, lakini ya muhimu zaidi ni mwonekano wake. Hutambulika kitaalamu kama ‘versicolor., neno la Kigiriki linalomaanisha kubadilika kwa rangi ya ngozi na hii humaanisha kuwa sehemu ya ngozi inayopata maambukizi ya maradhi haya hubadilika rangi yake kutoka ile ya asili.

Mfano rahisi ni mabadiliko ya rangi ya ngozi kutoka maji ya kunde na kuwa nyeusi zaidi au nyeupe zaidi ukilinganisha na sehemu za ngozi zilizozunguka eneo lenye maambukizi ya fangasi hao.

Ni sehemu gani hushambuliwa?
Maeneo ya ngozi yanayoathiriwa zaidi katika mwili ni mabega, shingo, mgongo na kifua.

Mara nyingine maradhi haya hushambulia maeneo ngozi inapojikunja kama vile maungo ya mikono, ngozi ya chini ya matiti, maeneo ya siri hasa pale miguu inapoanzia. Uso mara nyingi hauathiriki, ingawa kwa watoto wanaweza kupata maambukizi ya kwenye kidevu, pua, mashavu na hata paji la uso.

Mara nyingi, fangasi hawa wanaposhambulia uso hushambulia kwa wingi kiasi kwamba ukimtazama mgonjwa kwa haraka haraka unaweza kudhani kuwa hiyo ndiyo rangi yake halisi ya ngozi na kuwa maeneo ambayo hayajaathirika ndiyo yaliyoathirika.

Sababu za kutokea kwake
Sababu za maradhi haya bado zinafanyiwa uchunguzi, lakini kama nilivyosema kwenye makala za nyuma kuhusu namna fangasi wanavyosambaa, na kwamba, sababu hizi pia ni muhimu, nazo ni; 

-Hali ya majimaji kwenye ngozi (inaweza kuwa hata jasho)

-Hali ya hewa ya joto (fangasi wanakua vizuri kwenye hali ya joto)

-Kinga ya mwili ikiwa chini

-Mabadiliko ya homoni
Inawezekana pia maradhi haya kupata watu ambao wamekosa sababu zilizotajwa hapo juu. 

Usambaaji wake
Kwa vile vimelea vya fangasi vinavyosambaza maradhi haya kwa hali ya kawaida huishi kwenye ngozi si lazima mtu aambukizwe, bali kwa kawaida maradhi haya hutokea tu.

Related Posts:

  • NAMNA YA KUONDOA HARUFU MBAYA KWAPANI Hakikisha   unaoga kila siku ili kupunguza idadi ya bakteria kwapani kwani husababisha kuweka harufu mbaya kwenye mwili hasa majira ya joto kwa kuwa mara nyingi joto ndilo husababisha jasho na harufu kwapan… Read More
  • JINSI YA KUONDOA MAKOVU YA CHUNUSI MARA nyingi chunusi zikitumbuliwa mbichi husababisha makovu yanayoleta weusi mbaya kwenye ngozi. Ukiachana na njia za gharama za kuondoa makovu hayo, kuna njia rahisi za kuondoa tatizo hilo:  1. Paka ‘bleach cream’ … Read More
  • MAMBO YA KUFANYA ILI USIPATE CHUNUSI Hakuna njia sahihi ya kujizuia ila unaweza kufanya yafuatayo;1.Osha taratibu sehemu unayodhani ina chunusi kwa maji safi na sabuni angalau mara mbili kila siku huku ukisugua taratibu ,usikwaruze kwa kucha au kitu choicho… Read More
  • NJIA ZA KUONDOSHA HARUFU MBAYA MWILINI Kila mtu ana jasho au harufu ya kipekee mwilini na ndiyo maana kila mtu ana mahitaji ya kipekee katika kutunza mwili wake. Viungo vifuatavyo ndivyo hasa vinavyotoa harufu mbaya: Kinywa Kuna wakati kinywa hutoa harufu… Read More
  • FANYA MAMBO HAYA KUZUIA CHUNUSI NA MABAKA USONI Chunusi ni ugonjwa wa ngozi ambao hujit-okeza kama viuvimbe/vipele vidogo vidogo hasa sehemu za uso,kifuani na hata mgongoni.Vipele hivi hutokea wakati vishimo vya kupitisha jasho katika ngozi vinapozibwa kwa mafuta… Read More

1 comments:

  1. Dawa ya kutibu ugonjwa huu ni nini mwanangu amepata usoni

    ReplyDelete