Thursday, 19 June 2014

HIVI NDIVYO FANGASI WANAVYOSHAMBULIA SEHEMU ZA SIRI!!



LEO tuangalie fangasi wanaoshambulia sehemu za siri, yaani Tinea cruris. Aina hii ya fangasi ndiyo inayofahamika na Watanzania wengi zaidi ya aina nyinginezo na waathirika huwashwa sana sehemu za siri.

Dalili zake
Kuna dalili nyingi sana za ugonjwa huu lakini kubwa kuliko zote ni kuwa fangasi hawa huambatana na muwasho mkali wa eneo lenye maambukizi hasa sehemu za siri, rangi ya ngozi ya eneo lenye maambukizi hubadilika na kuwa na muundo wa duara, mfano wa sarafu.

Dalili nyingine ni ngozi kukauka kisha kubanduka, na kama mgonjwa asipopata tiba mapema basi atatokwa na majimaji kwenye eneo la ngozi lililoathirika pamoja na kutoka kwa harufu mbaya kwenye eneo hilo.


UNAVYOAMBUKIZWA
Kuna njia nyingi zinazoweza kusababisha uambukizi wa maradhi haya, lakini ili uambukizaji huu uwezekane lazima kuwe na mazingira rafiki ya kuwezesha fangasi kuishi na kuhama kwa urahisi.

Mazingira haya rafiki kwa kuruhusu fangasi hawa kuweza kutoka kwa mtu mmoja au sehemu moja ya mwili kwenda kwa mwingine huhitaji uwepo wa hali ya joto pamoja na majimaji sehemu iliyoathirika na 
maambukizi hutokea kwa kugusana na mtu aliye na maambukizi tayari.

Mtu anaweza kupata maambukizi ya fangasi hawa kwa kushirikiana kimapenzi na mwenzake aliye na 
ugonjwa au kwa kushirikiana mavazi na mtu aliyekwisha pata maambukizi au kushirikiana taulo au hata 
sabuni na vifaa vya usafi wa mwili kwa mtu zaidi ya mmoja.

Watu ambao huweza kupata maambukizi ya fangasi wa sehemu za siri ni wale wanaofanya kazi 
zinazohusisha ukaaji kwenye maji yaliyotuama kwa muda mrefu, wanaoshiriki mapenzi na wenza wenye
maambukizi ya fangasi hao na wote ambao wana fangasi za kwenye vidole kwani fangasi wale wanaweza 
kuhamishwa kupitia kwenye kucha na kuhamia kwenye eneo hilo la siri;

Wengine wanaoweza kupata maradhi haya ni wale wanaofanya usafi wa mwili kwa kutumia maji yaliyobeba 

vimelea vya fangasi hao, wasiojikausha vizuri maungo ya sehemu za siri, watu wenye maradhi 
yanayosababisha kushuka kwa kinga, hususan kisukari, wanaovaa nguo zaidi ya moja hali inayosababisha 

mwili kushindwa kupunguza joto lake hivyo kutoa jasho, wanaovaa nguo za kubana sana hasa zile 
zinazobana sana kwenye maeneo ya maungo ya siri na wenye unene wa kupindukia;
Lakini watu wanaokunywa dawa za kuua vimelea (antibiotics) kwa muda mrefu au wenye ujauzito ambao 
huchangia kushuka kwa kinga ya mwili nao wanaweza kupata ugonjwa huu


Related Posts:

  • MAGONJWA YA FANGAZI SEHEMU ZA WAZI Eneo lenye maradhi pia hubadilika rangi na kuwa na rangi tofauti kidogo na rangi ya ngozi ya eneo ambalo halijaathirika na maambukizi. Kama mwendelezo wa makala yetu ya maradhi ya ngozi, tuendelee kuangalia maradhi ya n… Read More
  • PUMU YA NGOZI (ECZEMA) Pumu ya ngozi au kwa kitaalamu Eczema (atopic dermatitis au atopic eczema) ni maradhi ya ngozi ambayo yamefanyiwa utafiti muda mrefu sana na kusema ukweli andiko langu hili halitoweza hata kuandika robo ya yale yanayofaha… Read More
  • (WARTS) MARADHI YA NGOZI KWA NJIA YA NGONO Baadhi ya maswali tuliyopokea, mengi yalihusu maradhi ya sunzua ambayo kitaalmu yanajulikana kama warts. Sunzua ni ugonjwa wa ngozi unaofahamika na wengi. Ugonjwa huu husababishwa na virusi ambavyo kitaalamu huitwa humanp… Read More
  • FUKUZA VIDONDA VYA TUMBO FANGASI NA MAPUNYE NI mpapai! Mara nyingi nimekuwa nikiongea kuwa Tanzania tuna miti mingi sana kiasi kwamba bado hata robo yake hatujaijua majina yake, achilia mbali kitu muhimu kama kujua matumizi. Mungu alipomuumba binadamu na… Read More
  • KUTOKWA NA MAJIMAJI KWENYE MATITI (GALACTORRHEA) Tatizo hili husimama lenyewe kama ugonjwa ingawa pia inaweza kuwa ni dalili kama mwanamke ni mjamzito, ananyonyesha au ametoa mimba au ameharibikiwa na mimba.Kusimama kwake kama ugonjwa ni pale  yanapotoka wakati mwa… Read More

0 comments:

Post a Comment