INAKADIRIWA
kiasi cha watu milioni 1.6 watapatwa na ugonjwa wa saratani mwaka huu
nchini Marekani na inakadiriwa kuwa kati ya hao, watu laki 5 watapoteza
maisha kutokana na ugonjwa huo hatari. Pia kiasi cha watu laki 6
hufariki kwa ugonjwa wa moyo nchini humo kila mwaka.
Licha
ya maendeleo ya kisayansi yaliyopatikana kwa nusu karne iliyopita,
lakini makampuni ya kimagharibi yanayotengeneza dawa za binadamu,
yameshindwa kuvumbua dawa madhubuti ya kudhibiti magonjwa haya mawili
yanayouwa watu wengi zaidi duniani.
Inaelezwa na watafiti wa masuala ya afya nchini Marekani kuwa hivi
sasa imedhihirika kuwa mikakati mingi ya kisasa, kuanzia kwenye vipimo
hadi matibabu ya magonjwa ya moyo na saratani, imeshindwa kufanya vipimo
na kutoa matibabu sahihi, wakati mwingine kwa kukosea, tiba ya magonjwa
haya huwa na madhara zaidi kwa mgonjwa kuliko ahueni.
Soda na hatari ya saratani
Kwa mujibu wa utafiti wa hivi karibuni, wanawake wenye umri kuanzia miaka 40, ambao hunywa kwa wingi soda au vinywaji vingine baridi vyenye sukari nyingi, wako katika hatari kubwa ya kupatwa na saratani ya kizazi.
Kwa mujibu wa utafiti wa hivi karibuni, wanawake wenye umri kuanzia miaka 40, ambao hunywa kwa wingi soda au vinywaji vingine baridi vyenye sukari nyingi, wako katika hatari kubwa ya kupatwa na saratani ya kizazi.
Imeelezwa kuwa utafiti huo ni wa uhakika kwa sababu matokeo hayo
yamepatikana baada ya kuwafanyia utafiti wanawake waliofikia ukomo wa
hedhi (postmenopausal) wapatao 23,000 kwa kuwafuatilia kwa muda wa miaka
14.
Katika utafiti huo, ilibainika kuwa wanawake waliokuwa na matumizi
makubwa ya sukari walikuwa katika hatari kubwa ya kupatwa na saratani ya
kizazi kwa asilimia 78. Kwa mujibu wa mwandishi wa utafiti huo, Bw.
Maki Inoue-Choi, hakushangazwa na matokeo ya utafiti huo kwani imekuwa
ikisemwa kwa muda mrefu kuwa sukari nyingi ina madhara.
Aidha, utafiti mwingine unaonesha kuwa ‘fructose’ (aina ya sukari)
huimarisha ukuaji wa chembechembe hai za saratani na kuharibu mifumo
kadhaa mwilini kwa njia mbalimbali, ikiwemo kuharibu mfumo wa usagaji
chakula tumboni, ukuaji wa seli za DNA na kinga ya mwili.
Baada ya utafiti huo, wagonjwa wa saratani za aina zote hushauriwa
kutotumia kabisa vyakula vyoyote vyenye sukari, kwani kwa kufanya hivyo
huwa wanauimarisha zaidi ugonjwa badala ya kuudhibiti. Sukari ni
miongoni mwa vyakula vinavyoimarisha chembechembe hai za saratani, hivyo
kuvinyima sukari ni njia moja wapo ya kuviua na kuvipa sukari ni sawa
na kuvifuga.
Pamoja na utafiti huo kuonesha kuwa chakula cha seli za saratani ni
‘fructose’, haikukatazwa watu kula matunda ambayo huwa na ‘fructose’,
badala yake wameshauriwa kupendelea kula matunda zaidi kuliko juisi
yake. Kimsingi ‘fuctose’ asilia iliyomo kwenye matunda haiwezi kuwa na
madhara kwa mwili wa binadamu kama ilivyo kwa ‘fructose’ za kutengeza
zinazotumika zaidi kwenye vyakula na vinywaji mbalimbali baridi.
Mwisho, pamoja na kuwa kwamba sukari ni bidhaa muhimu kwa matumizi ya
binadamu ya kila kila siku na kwamba sukari pia ina faida mwilini,
lakini ni vyema ikaeleweka siyo bidhaa salama unayoweza kuitumia
utakavyo. Pale ambapo hatuna budi, basi tuitumie kwa uchache sana na
pale ambapo tunaweza kuiacha kuitumia kabisa, bora tukafanya hivyo.
0 comments:
Post a Comment