Thursday, 8 May 2014

WADUDU NI CHAKULA BORA!


Repoti mpya ya Shirika la Chakula la Umoja wa Mataifa (FAO), limetoa taarifa hivi karibuni ikiwahimiza watu duniani kula wadudu kwa wingi kwani ni 
miongoni mwa vyakula bora, kutokana na kuwa na kiasi kingi cha virutubisho bora vya mwili.
Senene.

Wadudu ni chanzo kikubwa cha protini, mafuta mazuri kiafya, madini na kamba lishe. Aidha, wadudu wameelezwa kuwa ni rafiki wa mazingira na ni rahisi kuwafuga au kuwakamata.
Inakadiriwa na shirika hilo kuwa kiasi cha watu bilioni 2 duniani wanatumia wadudu kama sehemu ya milo yao ya kila siku. Imeshauriwa watu kupendelea 

kula wadudu kutokana na ukweli kwamba protini inayopatikana kwenye wadudu hao ni bora zaidi  kuliko ile inayopatikana kwenye nyama ya kuku, ng’ombe, nguruwe na samaki.


Mbali ya wadudu kuwa ni chanzo kikuu cha protini na mafuta mazuri kama ya samaki (fish oil), lakini pia ni chanzo kizuri cha madini ya kashiamu (calcium), chuma (iron), seleniamu (selenium), zinki (zinc) na Vitamini B.
Kumbikumbi.
WADUDU WA TANZANIA
Kuna aina zaidi ya elfu tisa ya wadudu wanaoliwa sehemu mbalimbali duniani. Lakini kwa nchini Tanzania, kuna aina kuu mbili za wadudu ambao wanajulikana na kutumiwa kama sehemu ya kitoweo katika familia nyingi nchini, hasa vijijini.


Aina hizo mbili maarufu nchini Tanzania ni Senene na Kumbikumbi, ambao hupatikana kwa wingi zaidi nyakati za masika sehemu za vijijini. Senene  na Kumbikumbi ni miongoni mwa vyakula vyenye faida nyingi mwilini na ni vitamu pia.


Kutokana na kuwa na faida nyingi za kiafya mwilini, ndiyo maana wamekuwa wakiliwa tangu enzi na enzi na mababu zetu. Ingawa idadi kubwa ya wadudu hao wanaoliwa hupatikana kwa kuwakamata kwenye makazi yao porini, lakini katika siku za hivi karibuni, mifumo ya kisasa ya kuwakamata wadudu hao imebuniwa na hivyo kurahisisha ukusanyaji kwa idadi kubwa na kwa mara moja.


Kwa kuona umuhimu na faida za kiafya zinazoweza kupatikana kwa kula wadudu, Shirika la Chakula la Umoja wa Mataifa limetoa wito kwa nchi zote duniani kufuga wadudu hao kwa wingi kibiashara, shirika linaamini nchi nyingi zikitilia mkazo suala hili, zinaweza kupunguza tatizo la njaa kwa kiasi kikubwa na wakati huo huo kuboresha afya za watu wengi.


Bila shaka hii ni habari njema na ya kutia moyo kwa watu ambao tayari wanafuga na kuvuna Senene kibiashara, kama ambavyo tunavyoona wakiuzwa baadhi ya sehemu za mijini. Nitoe wito kwa watu wengine ambao hawajawahi kuonja Senene au Kumbikumbi kufanya hivyo, kwani siyo tu wana faida kiafya mwilini, bali ni watamu sana. (so delicious)!

Related Posts:

  • 10 Unexpected Side Effects Of Peppermint Tea Peppermint—the word conjures up images of bubble gums, right? But, peppermint is also used to provide flavor to various other products. Some of them are toothpaste and tea. It is an active ingredient in various medicinal a… Read More
  • 10 Harmful Side Effects Of Ginseng Tea Ginseng is an ancient herb, which offers remedies for many diseases. It is also known as the king of all herbs. It protects our body and also helps our body fight innumerable diseases. Ginseng is an adaptogen, which is cap… Read More
  • 5 Side Effects Of Garlic You Should Be Aware Of Allium sativum, commonly known as garlic is a member of the onion genus species, Allium. It falls into the broad category of onions, shallots, leak and chive and is usually of a pungent nature in smell and taste. Originati… Read More
  • 10 Surprising Side Effects Of Watermelon Come summers and we can find watermelons everywhere! The perfect summer fruit, watermelons with high water content, make for great thirst quenchers. Watermelons are not just tasty and refreshing but are healthy too! They c… Read More
  • 12 Side Effects Of Aloe Vera Juice You Should Be Aware Of Aloe Vera is a succulent cactus plant, belonging to the family Liliaceae. It is widely known as “the Miracle plant” for its various medical, cosmetic and nutraceutical purposes. Aloe vera gel is a slick substance that is e… Read More

0 comments:

Post a Comment