Thursday 8 May 2014

VYAKULA VINAVYOEPUSHA UNENE

LEO  nawaletea elimu ya jinsi ya kupunguza unene na kuepuka kunenepa zaidi kwa kula vyakula husika.
Zipo njia nyingi za kumfanya mtu apunguze unene
miongoni mwa njia hizo ni pamoja na vyakula, kujua aina ya vyakula unavyotakiwa kula na kuvila kama inavyoelekezwa.
Vifuatavyo ni vyakula, mboga na matunda ambayo vikiliwa kwa mpangilio mzuri huondoa mafuta ya ziada mwilini na hivyo kupunguza unene:
MATUNDA
Matunda ni miongoni mwa vyakula vinavyoyeyusha mafuta mwilini, idadi kubwa ya mtunda huwa na kiwango kidogo cha ‘calories’ lakini yana kiasi kingi cha kamba lishe (fiber).
Hivyo, unaweza kuchanganya ulaji wa matunda na vyakula vyenye mafuta bila kuongezeka unene. Matunda kama epo, machungwa, zabibu, mapera ni miongoni mwa matunda yenye kiasi kingi cha kamba lishe.
Vilevile, tikitimaji lina faida kubwa mwilini, kwani lina uwezo wa kuondoa sumu mwilini (toxins) ambayo huingia mwilini kwa njia ya chakula na hewa tunayoivuta kutokana na hali halisi ya maisha ilivyo.

MBOGA ZA MAJANI
Mboga nyingi za majani huwa na kiasi fulani cha kamba lishe, na kamba lishe iko katika makundi mawili, ya kwanza ikiwa ni ile inayoyeyuka mapema na ile isiyoyeyuka mapema, mbogamboga zinazochukua muda kuyeyuka tumboni lakini zinasaidia sana usagaji wa chakula haraka ni pamoja na mchicha, spinachi, kabeji, maharage ya kijani na nyingine jamii ya majani kibichi.

PROTINI
Idadi kubwa ya vyakula vinavyoyeyusha mafuta haraka mwilini katika jamii ya vyakula vya protini ni vyakula vya baharini. Ingawa samaki huhitaji nishati nyingi kuyeyushwa mwilini, lakini ni miongoni mwa vyakula vinavyosaidia uyeyushaji wa mafuta mwilini kwa haraka zaidi. Ili kupata matokeo mazuri na ya haraka, pendelea kula vyakula vya baharini sambamba na mboga za 

Majani 
kama vile kabichi au saladi ya mbogamboga mchanganyiko.
Vyakula vingine ni vile vitokanavyo na maziwa, ngano isiyokobolewa, wali, ambavyo wakati wa kutayarisha unatakiwa kuhakikisha vinakuwa na kiwango kidogo cha mafuta asilia bila kuongezewa ya ziada.
Kwa leo tuishie hapa kama una swali nipigie kupitia namba hiyo hapo juu.

0 comments:

Post a Comment