Wengi
wanafikiria kuwa unene ni fahari, heshima, lakini huenda wanasahau au hawajui
madhara mengi ambayo yamejificha nyuma yake
Imekuwa
ikidhaniwa kuwa unene wa mwili ni kufanikiwa kiuchumi au kuukata, kumbe
sivyo. Uchunguzi wa kitaalamu unaonyesha kuwa watu wanene wapo katika
hatari ya kupata maradhi ya kiharusi, kisukari na ugonjwa wa moyo.
Matumizi
ya baadhi ya vyakula na kutokujua chakula gani wale na kwa wakati gani bado ni
tatizo.
Baadhi yao
hula vyakula hivyo usiku, bila kujua athari kuwa vinazidisha unene na
kuhatarisha maisha.
Wataalamu
wanaeleza kuwa baadhi ya vyakula vikiliwa usiku husababisha athari kwa afya za
watumiaji wake.
Athari
kubwa zaidi ni kuongezeka uzito bila mpangilio, kukosa usingizi na kulala kama
mfu kutokana na tumbo kujaa, vilevile kulala kwa usingizi wenye kukatikakatika,
kujisaida haja ndogo kila mara. Madaktari na wataalamu wengine wa afya
wanashauri kwamba ili kujiepusha na athari hizi ni vyema watu wanene wakatumia
matunda, mbogamboga au vyakula vingine ambavyo vina kalori na mafuta kidogo au
visiwe navyo kabisa.
Hivi ni
baadhi ya vyakula ambavyo si vizuri kula wakati wa kwenda kulala kwa watu
wanene na wenye uzito mkubwa.
Vyakula
vilivyoandaliwa kwa mafuta mengi
Hii ni
aina ya chakula ambacho hupaswi kula usiku kwa sababu havikufanyi ujisikie
uchovu na uvivu asubuhi ya siku inayofuata, bali pia humpa msukosuko mtumiaji
wa kwenda kujisaidia mara kwa mara.
Pamoja na
vyakula vya mafuta, ice cream ni tatizo kwa kuwa ukila sukari unaongezeka
uzito bila sababu, pia hujipa msukosuko wakati wa kulala kwa kuwa baada ya muda
huyeyuka na kuzaa tatizo nyingine. Aina hii ya vyakula husababisha
magonjwa ya kiharusi, kisukari na ugonjwa wa moyo.
Kabohaidreti
(wanga) kwa wingi au vyakula vyenye sukari kupitiliza
Kundi hili
ndilo ambalo watu wengi hulichanganya kwa kuamini kuwa tambi ‘supagheti’ ni
chakula chepesi kuliwa usiku, kitu ambacho si sahihi.
Tambi ni
moja ya vyakula ambavyo havipaswi kuliwa usiku kwani ina wanga mwingi ambao
kutokana na kulala hakisagiki na kinaweza kuziba mirija ya damu na kusababisha
madhara kwa mtumiaji.
Kipande
kidogo cha keki kinaweza kuwa kizuri kwa mtumiaji, lakini akizidisha siyo nzuri
kutokana na kuwa na sukari nyingi. Vilevile mkate mweupe uepukwe una wanga
mwingi.
Nyama
nyekundu na vyakula vyenye protini nyingi
Kula nyama
nyekundu usiku kunamfanya mhusika asipate usingizi mzuri kwa kuwa tumbo
linashindwa kusaga vyakula vigumu uwapo usingizini.
Kama ni
lazima kula nyama, basi ni vyema ikawa ni nyama nyeupe kama vile kuku na
samaki na kuepuka vyakula vyenye protini. Ikishindikana, basi glasi ya
maziwa ya moto inaweza kukidhi haja bila kuwa na madhara.
Vyakula
vyenye viungo vingi
Hupaswi
kula vyakula vya aina hii kwa kuwa vina kemikali ambayo inaweza kukukosesha
usingizi.
Kahawa
Kwa
kawaida, kahawa ina kafeini ambayo inaweza kusababisha usumbufu wakati wa
kulala kwani hata dawa zenye kafeini hapaswi kupewa mgonjwa mwenye matatizo ya
kulala.
Vivyo
hivyo, kwa asiyekuwa mgonjwa ina madhara pia hapa hata soda ambazo zina
kafeini, pia zinasababisha mtumiaji kukosa usingizi wa kutosha, hivyo kushindwa
kufanya mambo katika mpangilio maalumu siku inayofuata.
Wataalamu
wa masuala ya chakula na lishe, Wanasema kuwa kama ni lazima kunywa kahawa,
basi iwe ni saa tano au nne kabla ya kwenda kulala.
wanasema
kuwa kuna baadhi ya vitu vina madhara kwa mtumiaji bila kujua kutokana na kuwa
na mazoea ya kutumia kitu hicho ambapo matokeo yake madhara yake huwa ni
mhusika kupata tatizo la kukosa usingizi.
Kula
chakula kingi
Madhara ya
kula chakula kingi ni mengi, mojawapo ni kukosa usingizi kutokana na kushiba
kupita kiasi.
Athari za
kufanya hivi ni pamoja na kuukosesha mwili uwezo wa kusaga chakula kwa kuwa
utakuwa umeshiba sana na mwili umepumzika.
“Ukiwa
katika hali hii hata usingizi unakuwa ni wa shaka kwa kuwa unakuwa umeshiba
sana, lakini hicho chakula hakifanyi kazi ipasavyo na ndiyo maana ni rahisi
kuongezeka uzito, hakimeng’enyeki kwa urahisi,”
Vyakula
vilivyokaangwa
Vyakula hivi
husababisha kiu, hivyo humlazimu mtumiaji kunywa maji mengi na kumlazimisha
kwenda msalani mara kwa mara.
Mwili unahitaji kupumzika kwa kulala kwa saa
sita hadi nane ili ufanye kazi na mhusika akiamka aanze upya.
“Kikubwa
hapa ni kupunguza kula vyakula ambavyo vitahitaji maji au vyenye maji maji
kuepuka kwenda msalani mara kwa mara au kuamka.
Pombe
Kunywa
pombe saa chache kabla ya kulala au kunywa na kulala huku ukiwa nazo kichwani
hata kama hujalewa siyo nzuri kiafya kwa kuwa huufanya mwili kulala kama mzigo
hivyo inakuwa siyo kupumzika bali kulazimika kulala kwa ulevi.
Mtaalamu
mmoja wa lishe anasema kuwa mwili unahitaji kupumzika ukiwa huru na siyo
kulazimishwa na kilevi, kwani kupumzika ni pamoja na kufahamu sasa naenda
kupumzika na mwili unauandaa kwa ajili hiyo, lakini ukiwa umelewa hali kama
hiyo haipo.
Daktari
Bingwa wa Magonjwa ya Ndani (Mfumo wa Chakula), Dk Raymond Mwenesano wa
Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH) anasema kuwa kwa kawaida mwili wa
binadamu unapohitaji mapumziko au unapofika muda wa kupumzika inabidi uwe
huru kwa maana ya kuwa katika hali ya kawaida, hususan sehemu za ndani kama
tumbo.
Anasema
kuwa kama utapumzika huku ukiwa na vitu vya ziada ambavyo vitakuwa na usumbufu
kwako kama kushiba, kulewa unakosa ile dhana nzima ya kupumzika na matokeo yake
ni kutimiza wajibu wa kulala na si kulala kwa ajili ya kupata mapumziko.
Mariam
Rashid, ambaye ni mnene kiwajihi anasema kuwa tangu aanze kupunguza kula
vyakula vyenye wanga wakati wa usiku amepungua uzito kwani alikuwa ni lazima ale
wali au chapati usiku na kujikuta ana uzito mkubwa akashauriwa na daktari
kupunguza uzito na kwa kuanza alianza kupunguza kula na kushiba usiku ikiwemo
kuacha vyakula vyenye wanga.
“Nakula
matunda na mboga mboga kabla ya kulala na huu ni ushauri niliopewa na daktari
wakati ambapo nilikuwa na uzito mkubwa ilikuwa karibu kilo 70 wakati urefu
wangu ni futi tano, ilikuwa ni hatari na daktari alinikemea na kunitaka
nipungue kwa kuwa nilikuwa nimeshaanza kupata tatizo la miguu na kukosa
usingizi,” anasema.
Mtaalamu
wa masuala ya Saikolojia wa Chuo Kikuu cha Dodoma, Modesta Kamongi amesema kuwa
si tu unene unaohatarisha afya ya mhusika, bali pia humfanya asijiamini.
Anasema ni
vyema kila mmoja akawa na mwili wa wastani kwani mara nyingi wamekuwa wakipata
malalamiko kwa watu wanene hujichukia na kutaka wapatiwe ushauri wa jinsi ya
kukabiliana na wale wanaowatania.
ah somo liko vizur tuendelee na kutuelumisha
ReplyDeleteSas ni chakul kipi kinafaa kula wakati wa usiku?
ReplyDeletembayabzaid ndo vyakula vinavyopatikana kwa wepesi zaid kwa hapa mjini sasa duuuh....ila somo limeeleweka.
ReplyDelete