Hepatitis B ni nini?
Ni ungojwa wa ini unaosababishwa na uambukizo wa
virusi vya hepatitis B. Mtu
anapopata uambukizo, virusi huvamia ba kuanza kuathiri chembechembe hai za Ini.
Baada ya hapo yafuatayo yanaweza
kutokea;
1. Kupata ugonjwa wa ini wa muda mfupi wa chini ya
miezi sita na kasha kupona kabisa (acute hepatitis B) au kupata ugonjwa mkali
(fulminant hepatitis) na hatimaye hata kufa
2. Kuendelea kuwa na virusi mwilini kwa muda mrefu
wa zaidi ya miezi sita na hapo baadae kusababisha kusinyaa kwa ini (Liver
cirrhosis) au
saratani ya ini ( liver cancer) na hatimae kifo.
NJIA KUU ZA
MAAMBUKIZO YA UGONJWA WA INI/ HEPATITIS B
Virusi vya Hepatitis B huingia mwilini kwa njia
ya damu au maji maji mengine ya mwilini kama vile maziwa, mate, maji maji ya
mbegu za kiume, maji maji ya ukeni n.k.
NJIA KUU ZA
KUENEA KWA UGONJWA HUU NI;
1. Kugusana ngozi kwa ngozi baina ya mwenye virusi
vya Hepatitis B na Asiye navyo kupitia kwenye vipele, vidonda, michumbuko,
mikwaruzo n;k (horizontal transmission)
2. Kutumia sindano na mambomba ambayo hayakutakaswa
(drcontaminated) na kuzuzwa ( sterilized) vizuri.
3. Kujamniiana na mtu mwenye virusi vya Hepatitis B
4. Kutoka kwa mama mwenye virusi vya Hepatitis B
kwenda kwa motto wakati wa kujifungua au wakati wa kumnyonyesha. (mother to
child transmission)
5. Kuongezewa damu yenye virusi vya hepatitis B
DALILI ZA UGONJWA WA INI (HEPATITIS B)
Mara nyingi
watu wenye ugonjwa huu hawaonyeshi dalili zozote. Karibu asilimia 90% ya watoto
wenye umri chini ya miaka mitano, asilimia 50% ya watoto wenye umri zaidi ya
miaka mitano na baadhi ya watu wazima huwa hawaonyeshi dalili zza ugonjwa huu;
Dalili za
ugonjwa wa Hepatitis B zinaweza kujitokeza wakati wowote kati ya wiki sita na
miezi sita tangu mtu apate ambukizo la virusi, kwa wastani huchukua muda wa
miezi mitatu.
DALILI ZA MWANZO.
Wagonjwa
huonyesha dalili zifuatazo;
·
Dalili za
mafua (flue like illness)
·
Kuumwa
kichwa
·
Homa
·
Uchovu
·
Kuishiwa
nguvu
·
Kupoteza
hamu ya kula
·
Kichefu
chefu
·
Kutapika
·
Maumivu ya
tumbo na hata kuharisha
DALILI ZA BAADAE.
Baada ya siku tatu hadi nne.
·
Macho na
ngozi (hasa viganja na nyanyo)
hubadilika rangi na kuwa njano.
·
Rangi ya
mkojo hubadilika na kuwa njano iliyokolea na kinyesi huwa cheupe cheupi.
Kwa Kawaida
dalili hizi hupotea katika muda wa wiki
mbili.
·
Asilimia 90%
ya wagonjwa watu wazima huweza kupona kabisa katiika muda wa miezi sita tangu
wapate uambukizo, na wachache wanaweza kufa katika kipindi Fulani hiki. Asilimia
5% hadi 10 huendelea na uambukizo sugu unaodumu zaidi ya miezi sita ambao
baadae huleta matatizo ya kusinyaa kwa ini, saratani ya ini na hatimae kifo.
·
Asilimia 70%
hadi 90% ya watoto wagonjwa baada yak upon huendelea kuwa na uambukizo sugu wa
Hepatitis B (hepatitis B carriers)
KUTHIBITISHA UGONJWA.
Ugonjwa
huthibitishwa kwa kupima damu ya mgonjwa katika maabara, kwa kuangalia
vitambulishi vya virusi vya Hepatitis B (
HBsAg, Anti-HBc, HbcAG)
TIBA
UGONJWA HUU HAUNA TIBA.
KINGA DHIDI
YA UGONJWA WA HEPATITIS B / UGONJWA WA INI.
CHANJO
Njia muhimu ya kujikinga na ugonjwa huu ni
kupata chanjo. Chanjo ya hepatitis B inaweza kuwa peke ya au ikichanganywa na
chanjo nyingine. Moja ya chanjo dhidi ya ugonjwa huu ambayo imechanganywa
tayari hujulikana kama DPT-HB. Chanjo hii ndiyo ilijumuiashwa katika mpango wa
chanjo wa Taifa.
NJIA NYINGINE ZA KUJIKINGA UAMBUKIZO
WA UGONJWA WA HEPATITIS B.
1. Kuepuka matumizi ya damu isiyopimwa virusi vya Hepatitis B/damu isiyo salama.
2. Kutotumia mabomba na sindano zisizotakaswa na
kuzuzwa(sterilized) vizuri
3. Kuepuka uasherati
4. Wafanyakazi wa afya kuwa waangalifu wakati wa
kutoa huduma hasa zinazohusiana na damu, sindano, upasuaji, uzalishaji n.k
CHANJO HII YA DPT-HB
Ni
mchanganyiko wa chanjo nne zinazomkinga motto asipatwe na magonjwa yafuatayo;
1. Dondakoo- Diptheria (D)
2. Kifaduro- Pirtussis (P)
3. PepoPunda- Tetanus (T)
4. Ugonjwa wa Ini- Hepatitis B (HB)
WANAOSTAHILI CHANJO YA DPT-HB.
Chanjo ya DPT-HB hutolewa kwa watoto wote walio na umri wa chini ya miaka mitano, hususani kati ya mwezi mmoja na miezi mitatu.
Kiasi cha chanjo kwa kila hudhurio ni 0.5ml,
ndani ya msuli wa paja la kushoto na chanjo hii hutolewa mara tatu kwa kila
mtoto.
MATATIZO YANAYOWEZA KUJITOKEZA BAADA YA CHANJO YA DPT-HB /Side effects)
Matatizo yanayoweza kujitokeza katika muda wa saa 48 baada ya chanjo ya DPT-HB ni;
·
Sehemu
iliyochanjwa inaweza kubadilika rangi kuwa nyekundu, kuvimba au kuuma kidogo.
Ø
Homa
Ø
Mtoto kulia
lia
Ø
Mtoto
kusinzia sinzia
Matatizo haya mara nyingi hutoweka yenyewe bila kupatiwa tiba na
si kupingamizi kwa chanjo.
0 comments:
Post a Comment