Monday, 5 May 2014

VIJUE VYAKULA BORA NA FAIDA ZAKE MWILINI-2


Makala haya tumerudia kutokana na sababu maalum na inaangalia vyakula muhimu na umuhimu wake katika ustawi wa afya zetu. Kumbuka chakula ni uhai, lakini pia chaweza kuwa sumu kama hakiliwi ipasavyo.
Vitunguu saumu.


KITUNGUU SAUMU
Hiki ni kiungo cha mboga, licha ya kuonekana kama ni kiungo cha kuongezea ladha ya chakula, lakini ni miongoni mwa vyakula vyenye faida kubwa katika afya zetu. Kitunguu saumu husaidia kuyeyusha damu mwilini hivyo kumuepusha mlaji na ugonjwa wa moyo pamoja na presha. Kitunguu hiki pia hutoa kinga kwenye ini na huondoa maumivu ya viungo. Kula angalau kitunguu kimoja mara moja kwa wiki.
Mdalasini.

MDALASINI
Hiki nacho ni kiungo cha kuongezea ladha na rangi kwenye chakula, lakini nacho kina faida zaidi ya hiyo. Mdalasini ambayo inapatikana kwa wingi katika masoko mbalimbali nchini, hufaa  kutumiwa na wagonjwa wa kisukari, kwani hurekebisha kiwango cha sukari mwilini kwa kiwango cha hadi pointi 50. Inapendekezwa kutumiwa angalau nusu kijiko cha chai kila siku mara mbili.
Matango.

TANGO
Watu wengi hulipuuza tango na wengine hawajawahi kula kabisa kwa sababu siyo tamu mdomoni, hata linapochanganywa kwenye kachumbari huepukwa. Hii yote inatokana na kutokujua umuhimu wa tunda hili. Inaelezwa kuwa tango linapoliwa husaidia kusaga chakula tumboni hivyo 

kumuwezesha mlaji kupata choo laini. Halikadhalika, tango linaweza kutumika katika kuboresha ngozi ya uso kwa kupaka, kwani huondoa vipele na kuifanya ngozi kuwa nyororo. Ni zuri linapoliwa na maganda yake na unaweza kula kiasi utakacho.
Asali.

ASALI
Kama kuna chakula kitamu na kizuri duniani, basi ni asali. Hiki ni chakula cha asili ambacho kimekuwepo enzi na enzi na kimesifiwa hata katika vitabu vya Mungu. Asali ina uwezo wa kudhibiti sumu mwilini, ina uwezo wa kumfanya mtu mnene kupungua uzito na mtu mwembamba kuongezeka uzito hadi kufikia uzito wa kawaida.

Asali huupa nguvu mwili haraka, huifanya ngozi kuwa nyororo, huzuia asidi, husafisha damu na ina uwezo wa kuua vijidudu mwilini.
Lamba asali kijiko kimoja cha chai asubuhi kabla hujala kitu chochote. Kwa kuwa asali ni tamu lamba mara 3, wagonjwa wa kisukari wanashauriwa kuila kwa tahadhari.
 
Tende.
TENDE
Tende ambayo ni maarufu sana katika nchi za Arabuni na ukanda wa mwambao wa Tanzania ni miongoni mwa vyakula vyenye faida kubwa mwilini. Sifa ya kwanza ya tende ni uwezo wake wa kuupa nguvu moyo dhaifu na kuupa nguvu mwili (energizer). Wale wenye matatizo ya moyo kukosa nguvu tende zitawasaidia. Tende nayo ni mlo tosha unaopaswa kuwepo katika orodha ya milo yetu ya kila siku.

Related Posts:

  • UWEZO WA AJABU WA JUISI YA KITUNGUU Kuna magonjwa mengine yakikupata hujui hata namna ya kujitibu. Lakini kwa kutumia vyakula na matunda unaweza ukashangaa namna ambavyo unaweza kuliondoa tatizo ambalo pengine ulidhani halina tiba. Katika makala haya ya l… Read More
  • VIUNGO NA MATUMIZI YAKE KWA KILA SIKU KWA AFYA YAKO. Viungo ni kitu muhimu kwenye chakula na huleta ladha ya kufanya  chakula kiwe na hamu zaidi ya kuliwa. Lakini viungo ni si tu huleta  ladha katika chakula lakini pia ni muhimu kwa afya. Leo tuangalie baadhi y… Read More
  • CHOROKO HUIMARISHA AFYA YAKO Je wewe ni miongoni mwa wapenzi wa choroko? Kama unatumia utakuwa miongoni mwa wanaofaidika na virutubisho muhimu kwa afya mwilini. Wataalamu waliofanya uchunguzi kuhusu choroko ambayo ni jamii ya kunde, wanasema utam… Read More
  • UWEZO WA AJABU WA JUISI YA KITUNGUU-2 leo tunaendelea kufafanua faida zake hasa kwa nywele za binadamu. Jambo muhimu la kuzingatia wakati wa usiku ni muda wa kumaliza kula na kunywa juisi hiyo. Hakikisha unakunywa juisi yako angalau masaa mawili baada ya kul… Read More
  • VIUNGO NA MATUMIZI YAKE KWA KILA SIKU KWA AFYA YAKO PART 2 Leo nimeona tuangalie baadhi ya viungo, matumizi yake na faida zake kwa afya zetu. Viungo vimekua vikitumika sana kuleta ladha katika chakula au vinywaji mbalimbali,lakini pia huleta afya katika miili yetu.Endelea kusom… Read More

0 comments:

Post a Comment