Saturday 3 May 2014

UVIMBE TUMBONI TISHIO KWA WANAWAKE/ ‘’UTERINE FIBROID’’


UVIMBE kwenye mfuko wa
uzazi au kama
unavyojulikana zaidi kwa
lugha ya kiingereza ‘Uterine
Fibroid’ ni moja kati ya
magonjwa ambayo
yameonekana kuwasumbua
wanawake wengi katika
siku za hivi karibuni.


Uvimbe huu unaojulikana
kwa jina jingine kama
Mayoma, katika miaka ya
hivi karibuni umeonekana
kuwa tishio kwa wanawake
wengi. Inaelezwa kuwa
zamani wanawake wenye
umri wa zaidi ya miaka 30,
ndio waliokuwa wakisumbuliwa na
ugonjwa huu, lakini sasa hali ni tofauti
kwani wasichana wadogo chini ya umri huo
nao wamejikuta wakiathirika na ugonjwa
huu.

Zipo sababu nyingi ambazo zimetajwa
kusababisha ugonjwa huu, lakini kubwa
kwa upande wa wanawake wenye umri wa
zaidi ya miaka 30, inatokana na kuchelewa
kuzaa.
Ugonjwa huu unawashambulia pia
wanawake ambao wana uzazi mdogo,
ambao wamezaa idadi ndogo ya watoto.

wataalamu wa Afya wanakiri
kuwa ugonjwa huo sasa ni tishio kwa
wanawake wote.
Dalili za ugonjwa kuwa
ni pamoja na kuvuja damu bila mpangilio
wa mzunguko wa mwanamke pindi
anapoingia kwenye hedhi.
Lakini uvimbe ukiwa mdogo
mgonjwa anaweza asione dalili zozote.

Pia, dalili hutegemea sehemu
uvimbe ulipo kwenye mfuko wa uzazi hii ni
pamoja na ukubwa wake.
Kwa mujibu wa Dk. Mmoja aliyehojiwa anasema mwanamke
ambaye amepata ugonjwa huu, hutokwa
damu nyingi pindi anapoingia kwenye
hedhi, hujisikia maumivu makali ya tumbo,
mgongo na hujisikia haja ndogo mara kwa
mara.

Wakati mwingine mwanamke hujisikia
maumivu makali wakati wa kujamiana na
mara nyingine husababisha mimba
kuharibika.

Uchunguzi
Mara mwanamke
asikiapo dalili hizi anashauri ni vyema
akaenda kwenye kituo cha afya na kuonana
na madaktari bingwa wa wanawake, ambao
wanaweza kumpima na kubaini tatizo
alilonalo.

Vipimo
Daktari anaweza kupima ugonjwa huu kwa

kutumia mikono miwili akapima tumbo,
lakini pia kipimo cha Ultrasound ndicho
hutumika zaidi kubaini ugonjwa huu
kwenye kizazi cha mwanamke.
Ugonjwa huu kabla ya kugundulika
huambatana na maradhi mengi ambayo
humtesa mwanamke kiasi cha kushindwa
kufanya shughuli zake za kijamii kama
ipasavyo.

Mara nyingi mgonjwa akikaa na tatizo hilo
kwa muda mrefu bila ya kupatiwa matibabu,
huishiwa damu, hupata matatizo ya figo,
kufunga choo na wengine huwasababishia
pia saratani.

Matibabu
Mgonjwa aliyepata
ugonjwa huu anaweza kusaidiwa kwa
kufanyiwa oparesheni ya kuutoa uvimbe
huo na anaweza kuzaa tena kama anahitaji
kufanya hivyo.
Lakini hata hivyo madaktari wanasema kama
ugonjwa utakuwa umeathiri kizazi kwa
kiasi kikubwa, njia kubwa ya kumsaidia
mgonjwa huyo ni kukitoa kizazi kama njia
ya kumuwezesha kumaliza tatizo hilo.

Hata hivyo daktari anashauri kwa
wanawake wanaopata ugonjwa huu na
kufanyiwa oparesheni ni vyema wakatafuta
ujauzito kama inafaa, ili kuepusha ugonjwa
huo kuendelea kuwaathiri zaidi kama
hawajawahi kupata watoto kwani
vinginevyo ugonjwa huo huwa na tabia ya
kurudia mara kwa mara.

Ushauri
Wanawake wanashauriwa kujenga
mazoea ya kujichunguza miili yao mara kwa
mara na kufanya uchunguzi, ili kuweza
kubaini matatizo waliyonayo ambayo
yakiachiwa yakomae zaidi huweza
kuwaletea madhara zaidi.


Vituo vya afya vya Serikali vipo namatibabu yanapatikana wakati wowote,hivyo ni vyema wanawake wakajengamazoea ya kuwachunguza hata watoto waowa kike, ili kuwaepusha na magonjwambalimbali.Ugonjwa huu ukiachiwaukakomaa kwa muda mrefu, huwezakusababisha ugumba na wakati mwingineukipasuka husababisha hata kifo.

Nawatakieni kila la kheri katika kujenga
maisha bora ya familia zenu, pamoja na afya
bora kwani bila afya mambo mengine yote
ya msingi hushindwa kufanyika na
kusababisha uchumi wa familia na nchi pia
kuyumba.

0 comments:

Post a Comment