Saturday, 10 May 2014
UTAFITI CHOKOLETI NYEUSI ZINA FAIDA KWA MOYO
Japokuwa kumekuwa na mjadala mkubwa kuhusu taarifa kuhusu faida za kiafya za chokoleti, lakini utafiti mpya umedhihirishwa kwamba kula chokoleti nyeusi kuna faida kwa moyo.
Utafiti huo uliochapishwa katika jarida la Moyo la Ulaya umeonyesha kwamba, kula kila siku gramu 7.5 za chokoleti, kiasi ambacho ni kidogo kuliko kipande mraba kidogo cha chokolati kunapunguza shinikizo la damu suala ambalo huondoa hatari ya kupatwa na mshituko wa moyo kwa asilimia 39.
Kula chokoleti kidogo huweza kumzuia mtu asipate ugonjwa wa moyo lakini iwapo tu italiwa badala ya vyakula vingine viliwavyo katikati ya mlo au asusa (snacks) vyenye kalori nyingi bila kuongeza uzito wa mwili.
Flavanols inayopatikana katika kakao huimarisha uwezo wa kiabiolojia wa seli wa kutengenezwa nitric oxide kuzunguka kuta za damu, suala ambalo hufanya mishipa laini ya damu ipumzike na kupanuka na hivyo kusaidia sana afya ya moyo.
Kwa kuwa katika chokoleti nyeusi kuna kakao nyingi, aina hiyo ya chokolati ina taathira kubwa katika kupunguza mfumuko wa mawazo na wasiwasi pamoja (stress) na kusaidia mzunguko wa damu na kiwango cha chinikizo la damu.
Lakini inaaminiwa kuwa chokoleti nyeupe hazina kabisa flavanol hivyo hazina faida hiyo.
Wataalamu wamesisitiza kwamba, watu wale chokolate nyeusi kila siku lakini kwa tahadhari kubwa kwani kiasi kidogo tu cha chokolati kina kiasi kikubwa cha kalori na mafuta ambavyo ni hatari kwa afya.
Related Posts:
WHO YATOA TAHADHARI KWA WANAOTUMIA SUKARI NYINGI WATAALAMU wa afya wametahadharisha kwamba juhudi zaidi zinahitajika kufanyika kupunguza kiwango cha sukari kinachotumiwa na watu. Shirika la Afya Duniani (WHO), kushirikiana na washauri wa masuala ya … Read More
CHAKULA NI TIBA NZURI, IJUE SIRI YAKE Watu wengi tuna desturi ya kula ili tushibe. Katika ulaji huo wakati mwingine tunajitendea ukatili wenyewe kwa kula vyakula visivyo sahihi ambavyo vinapoingia mwilini hugeuka kuwa sumu. Lakini vyakula pia ni dawa na leo… Read More
UBONGO WA MTU UNA SELI 100 BILLIONI ZA MAWASILIANO Ubongo una mfumo wa mawasiliano ya kustajabisha kama makala haya yanavyochambua. Ubongo ni kiungo cha aina yake katika mwili wa binadamu. Ubongo hutoa kila fikira, tendo, kumbukumbu, hisia na uzoefu wa kid… Read More
NI KWELI MAYAI HUSABABISHA UGONJWA WA MOYO? UTAFITI uliofanywa nchini Marekani hivi karibuni unaonesha kuwa katika miaka ya 1950, wastani wa ulaji wa mayai ya kuku ulikuwa mayai 375 kwa mtu mmoja, lakini hadi kufikia mwaka 2007, kiwango hicho kimepungua hadi … Read More
MIFUPA YA N'GOMBE TIBA YA KUONDOWA FLORAIDI MAJINI UTAFITI mbalimbali uliofanywa na Wizara ya Maji na Umwagiliaji, umebaini kwamba mifupa ya ng’ombe ina uwezo mkubwa wa kupunguza kiasi cha madini ya floraidi katika maji ya kunjwa. Akizungumza na waandishi wa habari jijin… Read More
0 comments:
Post a Comment